Mayor of kingstown
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 2,920
- 4,216
WITO KWA VIONGOZI: JIFUNZENI KUZUNGUMZA BILA KUTEGEMEA MAANDISHI
Ni jambo la kusikitisha kuona baadhi ya viongozi wakishindwa kabisa kuwasiliana kwa ufasaha mbele ya umma bila kutegemea karatasi au "vi-memo". Mfano wa karibu ni Kiongozi wa Kisiwa cha Comoro ambaye hata salamu au pole za kawaida analazimika kuzisoma kwenye karatasi. Hili linaonyesha udhaifu mkubwa wa kujieleza na kutotumia uwezo wa kawaida wa kiakili katika mazingira ya hadhara.
Ni kweli kwamba maandalizi ya hotuba ni muhimu, lakini kiongozi mzuri anapaswa kuwa na uwezo wa kuwasilisha mawazo yake kwa ufasaha, kuonyesha ushiriki wa dhati wa akili na hisia kwa watu anaowaongoza. Kila mara kuinama kusoma hotuba, hata kwa ujumbe mfupi wa pole, kunachosha na kunapoteza mvuto wa ujumbe kwa wasikilizaji. Kwa hakika, hali hii huondoa kabisa ile "connection" ya kihisia kati ya kiongozi na wananchi wake.
Tunajitahidi kumbeba, lakini habebeki. Uongozi siyo nafasi ya kusoma maandiko kila dakika – ni nafasi ya kuwasilisha dira, matumaini na msukumo kwa waliochini yako. Kiongozi anayeshindwa hata kuzungumza kutoka moyoni anapoteza hadhi na heshima machoni pa walio wengi.
Tunaomba viongozi wetu wajifunze: matamko yenu yawe ya dhati, yaakisi fikra zenu binafsi, na siyo kuonekana kama mashine za kusoma maandiko. Taifa linahitaji viongozi wenye uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja, wanaojua nguvu ya maneno ya mdomo na si maandiko pekee.
MWISHO tuendelee kudumisha amani na upendo kwa nchi yetu, NO REFORMS NO ELECTION