Amani ya Mungu
Member
- Sep 1, 2011
- 47
- 95
Kumekuwa na malalamiko mengi kuhusu ugumu wa kupata nafasi ya kuwasilisha maombi ya Visa ya China nchini Tanzania. Watu wengi huilaumu Ubalozi wa China, lakini kwa mtazamo wangu, tatizo kubwa si ubalozi wenyewe, bali ni mtandao wa madalali na watu wa kati ambao wamejijengea mfumo wa kujipatia fedha kupitia foleni za waombaji.
Kwa kawaida, Ubalozi wa China huruhusu waombaji kuanza kupanga foleni nje ya ubalozi kuanzia saa 12 asubuhi, ingawa huduma rasmi huanza saa 2 asubuhi. Kutokana na ushindani wa nafasi, watu wengi hufika hata saa 8 au saa 10 usiku na kusubiri eneo la Toure Drive hadi saa 12 walinzi wanaporuhusu waombaji kuelekea kwenye eneo la ubalozi.
Hapo ndipo mchezo wa madalali unapoanzia.
Madalali hawa hukesha eneo hilo usiku kucha. Wengine huonekana wakiwa na madaftari wakidai wanaandika majina ya watu waliowahi kufika, lakini mara nyingi hayo si majina ya waombaji waliopo eneo hilo. Wanachofanya ni kuhifadhi nafasi za mbele kwa ajili ya wateja wao.
Kwa mfano, unaweza kufika saa 8 usiku ukakuta unaambiwa kuna watu takribani 30 mbele yako. Na wakat mwingine huwa wamewaandika kwenye daftari. Kwa kawaida utaamini hao ndio waombaji waliowahi kufika. Lakini ukweli ni kwamba sehemu kubwa yao ni madalali wanaoshikilia nafasi.
Asubuhi, walinzi wanaporuhusu watu kuelekea kwenye foleni rasmi ya ubalozi, ndipo mchezo halisi huanza. Madalali huanza kuwaingiza wateja wao katikati ya foleni. Ndiyo maana foleni ambayo awali ilikuwa na watu 30, ghafla unakuta imefika watu 50 au hata 60. Watu wengi walioingia mbele hawakuwa wamefika usiku au alfajiri sana kama wananchi wengine walivyokuwa wamefika.
Baada ya hapo, baadhi ya madalali huondoka kabisa kwenye foleni kwa sababu hawakuwa waombaji wa visa. Nafasi walizokuwa wamezishikilia hukabidhiwa wateja wao waliokuja baadaye au watu wengine walionunua nafasi hizo. Kwa kifupi, madalali hutumia miili yao kuhifadhi nafasi mapema, halafu baadaye huziuza au kuwapa waliowalipa.
Inasemekana nafasi hizo huuzwa kwa kati ya shilingi 50,000 hadi 200,000, na wakati mwingine zaidi, kutegemeana na mahitaji ya siku hiyo. Pia kumbuka wapo wanaotoza complete package hadi shilingi 600,000 kwa huduma ya kuandaa nyaraka, kupata invitation na kushughulikia mchakato mzima wa maombi ya visa. Wateja wao ndio hupewa kipaumbele kupitia mfumo huu wa foleni.
Mbali na hilo, kuna siku ambazo ubalozi hulazimika kuwahudumia pia watu wenye kipaumbele maalum, kama baadhi ya watumishi wa serikali au wenye dharura muhimu. Hivyo, kama siku hiyo kuna watu wa kipaumbele 10, nao huongezeka maana hawa hawapangi kabisa foleni.
Kwa kuwa kwa siku ubalozi hupokea takribani waombaji 70 hadi 100 pekee wa kuwasilisha pasipoti zao, utagundua kuwa nafasi nyingi tayari zinakuwa zimechukuliwa na madalali pamoja na watu wenye kipaumbele. Mwombaji wa kawaida anayefuata utaratibu hubaki kupigania nafasi chache zinazobaki. May be nafasi 30 tu
Ndiyo maana utakuta mtu amefika saa 9 au saa 10 usiku, lakini bado hafanikiwi kuingia siku hiyo maana amefika mapema kuzipigania nafasi pengine ni 20 au 30 tu ambapo nyingine tayari madali wamekaba. Wengine hulazimika kurudi tena kwa siku nyingine kadhaa, hata wiki nzima, bila mafanikio. Si kwa sababu walichelewa, bali kwa sababu mfumo wa udalali tayari unakuwa umehodhi nafasi nyingi za mwanzo.
Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba wakati mwingine madalali wakiona wateja wao hawajapata nafasi walizotarajia, huzuka vurugu na mabishano yanayovuruga utaratibu wa foleni. Pia, yapo malalamiko kwamba baadhi ya walinzi wanaonekana kuwapa ushirikiano madalali hawa, jambo linalozua maswali kuhusu uadilifu wa mfumo uliopo.
Awali kulikuwa na mfumo wa online appointment kwa maombi ya Visa ya China. Hata hivyo, inaelezwa kuwa madalali walikuwa wanajaza nafasi zote za miadi kwa mwezi mzima, hivyo waombaji wa kawaida walishindwa kupata nafasi. Cha kushangaza, siku za huduma zilipofika, ubalozi ulikuwa unakuta miadi imejaa lakini waombaji wengi hawafiki. Inaaminika hali hiyo ndiyo iliyopelekea mfumo huo kusitishwa nchini Tanzania.
MAPENDEKEZO
1. Serikali ichukue hatua dhidi ya madalali.
Mtu yeyote asiyehusika moja kwa moja na maombi ya visa asiruhusiwe kukaa au kufanya shughuli yoyote nje ya ubalozi. Hii itapunguza biashara ya kuuza nafasi.
2. Kampuni zinazotoa huduma za visa na usafirishaji zipangiwe maeneo mengine.
Makampuni yanayokwenda kujitangaza na kukusanya wateja nje ya ubalozi yasiruhusiwe kufanya shughuli zao eneo hilo ili kupunguza msongamano na mazingira yanayochochea udalali.
3. Kurejesha mfumo wa online appointment kwa maboresho.
Badala ya kutumia mfumo unaoweza kujazwa na madalali, miadi ihusishwe na application number, taarifa za pasipoti au uthibitisho wa mwombaji ili mtu mmoja asiweze kuhifadhi nafasi nyingi.
4. Kuchunguza ushiriki wa walinzi.
Ikiwa kuna walinzi wanaoshirikiana na madalali, hatua kali za kinidhamu zichukuliwe ili kurejesha imani ya wananchi kwenye mfumo.
5. Kuongeza idadi ya waombaji wanaohudumiwa.
Ikiwezekana, ubalozi uangalie uwezekano wa kuongeza idadi ya watu wanaopokelewa kwa siku ili kupunguza msongamano.
Lengo si kuilaumu Serikali au Ubalozi wa China, bali kuondoa mfumo wa udalali unaowaumiza Watanzania. Mtu anayefuata taratibu hapaswi kulazimika kukesha kwa siku nyingi, kulipa fedha za udalali au kukosa huduma kwa sababu nafasi zimehodhiwa na watu wachache. Endapo Serikali ya Tanzania na Ubalozi wa China watashirikiana kufunga mianya hii, tatizo linaweza kupungua kwa kiwango kikubwa na kila mwombaji akapata haki yake kwa usawa.
Pia soma ~ Wizara: Ubalozi wa China umesema hakuna vikwazo vya kisera kwa Watanzania wanaoomba visa za China