Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

Changamoto za kupata mtoto mchanga ukiwa umri wa kustaafu, unakuwa ni Baba Babu. Dawa ni kujipanga kabla, vinginevyo ni kubebesha watu mizigo yako

Namuwazia huyu Mrembo aliyejitokeza kukupenda ukiwa kwa wheel chair,

sijui hata ulimpatia wapi Pascal,zawadi uliyompa naona ni kubwa ila bado
she deserves more...

Hapo kwenye watoto safi,its my plan wangu wafike 10 "watafikaje"? sijui! ninachojua

lazima niwe na watoto 10 na wote nitawapata angali ni Kijana, "biblia itanisamehe eneo hili"

Akili na mawazo yangu ni kwa huyo malkia uliyem bahatsha,ukskia one in a million ndio huyo sasa!

Happy Birthday Pascal.
Siku hizi vijana hawatoi mbegu zao.tunazaa tu na wahenga
 
Wewe bana tu sperm zako bna.wacha watu watoe mbegu
It's not even about that.

It's about unataka kuzaa bila kufikiri kama sungura ama unataka kufikiri dunia ijayo itakuwaje?

Ni haki yake, hilo halina mjadala.

Ila, kwa kuwa kaleta "humble brag" yake hapa, ni wajibu kutoa tunayofikiri.

Watoto 9 dunia ya leo kwani kuna mashindano ya kuzalisha?
 
Pasco., na hao wengine wengi waliobaki zaidi ya hao uliowataja? Unaishi nao nyumba moja leo hii?.
Yes wote niliishi nao nyumba moja but they are in different stages. Wale wakubwa wawili wa mwanzo, both are independent na both family zao na nina wajukuu.
Bongo 2, wote watatu wako university level, wanakaa hostel na wakimaliza ni independent.

Bongo 3 ndio waliopo home kwa sasa,
ndiyo maana hata teuzi hupewi.
Kuna uhusiano gani wa teuzi na familia kubwa?!. Was there any moment Pasco Mayalla aliwahi kufukuzia teuzi?.
Na Freemason membership sahau kama ulikuwa una mpango nayo.
Freemasonry what for?!.
Why have all these kids, with 3-4 different moms? .
Mimi ni devout Christian, jee kwenye Bible, is there any limit number ya how many women a man should have?.
Hata ku-bond nao inakuwa taabu.
Kuna vitu huwezi jua kuhusu bonding, kuna bonding za kizungu na bonding za kiafrika. Ukikatana na an African man who can date several ladies, ujue he can also bond with 10 kids!.
Ungekuwa USA ungefungwa sababu ungeshindwa kulipa child support kwa watoto wote hao.
Nimeishi UK na US, hata hiyo fellowship yake bado pesa ya nyumba na kuendeshea familia nimelipa mimi!. Hao watoto wote 8, hakuna aliyesoma St. Kayumba!. Kila aliyefika 21 years among the present ni driving license with...(naomba nisiendelee nikaonekana na brag), sasa ni child support gani hiyo ningeshindwa kuilipa hadi nifungwe?.

Watu humu tunajuana ki jf jf, but very few we hardly know one another for real.

Tutendee kujuana tuu hivi hivi ki jeiefu jeiefu.
P
 
Leo Ijumaa ya Tarehe 8 April, ni siku yangu ya kuzaliwa, nikiwa nimeipiga mingi nikikaribia 60! ambao ndio umri rasmi wa kustaafu, nikiwa tayari ni father of 8 +1= 9, Grand Pa of 6, and about to retire!.

Sababu ya makala hii ya leo sio kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, bali kutoa mbinu za changamoto za ulezi katika umri mkubwa kwa huku unajiandaa kustaafu, huku vichanga vinaendelea kuzaliwa!.

Naomba kutoa taarifa ya ujio wa mgeni mwingine kwenye familia yangu, ujio wa mgeni huyu, ume concide na tarehe yangu ya kuzaliwa, mgeni huyu mpya, amebisha hodi Duniani Leo, 8 April, 2022 majira ya saa 4:00 asubuhi, katika hospital ya Aga Khan, na kwa vile mgeni mwenyewe ni kidume, hivyo nimetoa jina langu la Pascal, hivyo ataitwa Pascal Mayalla, Jnr na kuanzia leo mimi nimebadili jina na kuwa Pascal Mayalla Snr baada ya ujio wa Pascal Mayalla Jnr.

Kupata mtoto katika umri mkubwa kama huu, kuna changamoto zake, changamoto ya kwanza, ni watoto wangu wakubwa tayari wana watoto, yaani mimi ni Babu, halafu unapata mtoto mdogo kuliko mjukuu, hivyo kwa wajukuu wa watoto wangu wa kiume, huyu Pascal Mayalla Jnr ni baba yao mdogo na wajukuu wa mabinti huyu ni mjomba wao, baba mdogo na mjomba kuwa ni mdogo kuliko wajukuu, haupendezei kivile!.

Kuna watu wataona ni ajabu kwa mtu over 50 kupata mtoto, japo nikweli sio kawaida sana, watu wanajenga familia wakiwa vijana, ukifika miaka 50 ni umri wa kujiandaa kustaafu na sio tena kuanza kulea na kuitwaa baba wakati umri ni wa babu, lakini amini usiamini, kupata mtoto at 50 plus ni kawaida sana, tuna mfano mingi tuu, ukitafuta umri wa Chief Burito wakati Julius Kambarage Nyerere anazaliwa, hutashangaa!. Hata Nabii Ibrahim alipomzaa Isaka alikuwa na miaka 90!. Mfano mzuri wa karibu ni yule Mzee wetu fulani, Al maarufu na mashuhuri, alipata watoto twins at 74 years!, hivyo mimi kupata mtoto at 50 plus, mimi ni bado sana!, ila huyu ni last born!.

lengo la makala hii ya leo ni kutoa somo la kujiandaa kustaafu, ili ustaafu bila stress. Kitendo tuu cha mstaafu mtarajiwa kupata mtoto at 50 +, hiyo peke yake tayari ni stress tosha, kwasababu mtoto anatakiwa kutimiza the age of majority, akiwa total dependant. Pesa za mstaafu, haziwezi kumlipia shule nzuri mtoto, unless nikubali akasome St. Kayumba!. Kama hao wenzake 8, hakuna aliyesoma St. Kayumba, hivyo huyu kitinda mimba wa Baba Babu, needs a little bit kujipanga zaidi. Hivyo makala hii, itakuwa ni msaada mkubwa sana kwa wale wote wenye umri mkubwa, huku wakikabiliwa na changamoto za ulezi.

Kutokana na maandalizi duni ya kustaafu, wastaafu wengi hujikuta hawana vitega uchumi vya kutosha kuwa sustain baada ya kustaafu, hivyo kuishi maisha ya stress, wengine kusumbua watoto kwa kupiga muzinga, hali inayopelekea ikiona tuu simu ya dingi, unahisi ni mzinga, hivyo ukijiona uko apeche alolo, unaogopa hata kupokea simu ya dingi ukidhani ni mzinga!, kumbe simu nyingine wala sio mizinga, ni dingi amekukumbuka tuu na anakupigia ili kukusalimia tuu.

Kitu kinacholeta stress kubwa Kwa wastaafu wengi, ni wengi kutofanya biashara yoyote wakati wa utumishi wao, halafu akiisha staafu yale malipo ya pensheni ya mkupuo kuyatumia kama mtaji wa kuanzisha biashara, biashara isipokwenda vizuri, matoi yake ni kupata stress, kuchoka mapema na kuchakaa, na hapo hapo maradhi ya depression na mwisho ni kufa mapema kwa ma pressure, heart attacks, maumivu ya viungo, organ failure etc.

Ili kuzuia stress za kustaafu, kama unapanga kufanya biashara fulani baada ya kustaafu, start small!, anza kidogo kidogo ukingali kazini kupata uzoefu wa kutosha ukiona unaweza ndipo ukistaafu ujikite zaidi.

Ushauri wangu wa the best way ya kustaafu, ni zile fedha za mafao yako ya kustaafu ambayo umelipwa kupitia benki, wastaafu wengi huziweka fedha hizo Benki kama akiba, na kuzitumia kidogo kidogo.

Kitendo cha fedha hizo kukaa Benki kwenye account ya savings, faida yake ni kiduchu Sana. Zingekaa kwenye a fixed deposit account, FDA, zingezalisha faida kubwa kidogo, lakini mpango mzima wa ukweli na wa uhakika wa uwekezaji wa mafao yako ni Kwa kuwekeza Kwa ununuzi wa dhamana za serikali, yaani Government Bonds, ambazo huuzwa na Benki Kuu ya Tanzania ambapo hutoa riba ya mpaka asilimia 16%!.

Sasa tupige hesabu ya Pamoja.
Tuseme mafao yangu ya kustaafu ya mkupuo ni milioni 100. Nikinunulia Government Bonds za miaka 25, kila mwaka nitapata shilingi milioni 16. Bonds wanalipa gawio mara 2 Kwa mwaka, kila baada ya miezi 6. Hivyo nitalipwa shilingi milioni 8 kila miezi 6.

Ukiisha nunua bonds zile Bondi certificate ni dhamana ya uhakika ya kupata mkopo Benki yoyote kufanyia biashara yoyote.

Nakushauri, fanya utaratibu na Benki yako, badala ya kusubiri kupokea gawio lako la milioni 16 kwa mwaka, unaomba ulipwe shilingi milioni 1,300,000 kila mwezi kwa muda wa miaka 25, bado wewe mstaafu utakuwa na stress au kusumbua kupiga mizinga watoto?.

Wastaafu wenzangu watarajiwa, ni muhimu sana kupanga uzazi, ni muhimu kupanga familia, ni muhimu kujipanga kustaafu bila stress, ila ikitokea umepata ugeni kama wa Pascal Mayalla Jnr, mida ya machweo, mpokee tuu mgeni with positivism after all kila mtoto anakuja na rizki yake,
Karibu Pascal Mayalla Jnr.
Happy Born Day Pascal Mayalla Jnr
Happy Birthday Pascal Mayalla Snr
Paskali
Update ya Kilichopelekea Kuendelea Kutengeneza Watoto Post 50 Years!.

Mkuu Goldschmidt , kwanza asante sana kwa kuwa mkweli, bonafide genuine, watu huwa hatupendi kuambiwa ukweli mchungu, hiki ulichosema hapa ni ukweli mchungu!.

It's true watoto 8, now 9 ni wengi. Mimi ni a modern man, niliao a classmate sweetheart Mimi nikiwa at 25 years mwenzagu 21, tukahama nchi kwenda UK tukapata mtoto wa kwanza a girl then tukahamia US tukapata mtoto wa pili, a boy tukaamua that is it. Hatuhihitaji tena kuongeza watoto.

Wife akapata full sponsored fellowship ya 4 years US mimi ndio niwe house husband na babysitter wa watoto wetu wawili. Very unfortunately, nilishindwa nikamwacha wife US na kurudi Bongo.

Long distance relationships doesn't work well Kwa baadhi ya makabila, so does maisha ya u Marioo, yaani mke ndio mwenye kazi, pesa, mimi niwe Marioo. Wasukuma ni one of such tribes.

Hivyo niliporudi kuishi bongo huku wife US, nikajikuta wametokelezea watoto 3. 2 boys and a girl hivyo I had 5 kids. (naomba usiulize ufafanuzi wowote kuhusu hawa watoto 3).

Wife baada ya kumaliza shule with news ya uwepo wa watoto 3, wife akaamua kugomea US hivyo mimi nikawa sina jinsi bali kurudi Bongo na kuendeshea na life.

Mwaka 2008 I suffered a bad motor accident, I was confirmed to a wheelchair!. Hapa akajitokeza kabinti fulani with a heart of gold, she came with love and care , kiukweli mtu ukiwa invalid confined to a wheelchair, akatokea mtu kupenda hivyo ulivyo, ni very rare and amaizing love.

She told me something was telling her tukijaribu pengine, nitaweza kupona. She made some efforts tukahangaika huku na kule, tukaenda South gharama zikatushinda , tukaenda India, ndiko nilikoponea na kusimama tena!.

Baada ya kupona na kurudi Bongo,
kwanza nitoa shukrani kwa yote niliyopitia

nikajikuta zawadi pekee kwa huyu binti ni ndoa, hivyo 2010 nikaoa tena, by then nikiwa over 40!.

Kabinti kakanizalia 3 beautiful daughters the number was 8, ilipotokea tena dalili ya ugeni, we didn't say no, then ndio hiyo jana kaleta kidume, na kiukweli hapo sasa ndio mwisho.
P
Hongera sana , lakini hakukuwa na haja ya kuandika essay.
 
Mkuu Goldschmidt , kwanza naomba kukubali nina watoto 9, sio kutamba, it's just kuwa open and honest.

Kuna vitu sikusema, mimi sio wale ma baba wanao dump watoto, hao wa US wameishi na mimi muda wote mama yao akisoma. Hao Bongo 2, nimewalea mimi mwenyewe as a single parent father kabla Bongo 3 hajatokea.

Hili la nitakufaje sio lako, sio langu ni lake YEYE!.
P
Huwezi kuwa na watoto 9 na wamama tofautitofauti, halafu wote ukawapa same headstart in life kwa maana ya huduma, malezi, upendo, ukaribu nao, etc. kwa kipato chako hicho hicho unachokitegemea miaka na miaka. Utawaachia nini siku ukifa watoto wote hao?
 
It's not even about that.

It's about unataka kuzaa bila kufikiri kama sungura ama unataka kufikiri dunia ijayo itakuwaje?

Ni haki yake, hilo halina mjadala.

Ila, kwa kuwa kaleta "humble brag" yake hapa, ni wajibu kutoa tunayofikiri.

Watoto 9 dunia ya leo kwani kuna mashindano ya kuzalisha?
Watoto 9?? Ana nafasi yake special mbinguni.ni kutesa watoto
 
Happy Birthday Mayalla na hongera kwa kupata kijana, history yako ni nzuri Ila Kuna mwaka Pamba sport ya Mwanza kulikuwa na mchezaji akiitwa Pasco Mayalla je ni wewe au majina kufanana tu?
 
Huwezi kuwa na watoto 9 na wamama tofautitofauti, halafu wote ukawapa same headstart in life kwa maana ya huduma, malezi, upendo, ukaribu nao, etc. kwa kipato chako hicho hicho unachokitegemea miaka na miaka. Utawaachia nini siku ukifa watoto wote hao?
This is where masikini wa roho kama wewe go wrong!. Unaamini kuwaachia watoto mali, ndio kuwasaidia!. Mimi mwenyewe kwetu tumezaliwa 8, na hakuna yeyote aliyefanikiwa Kwa kutegemea kaachiwa nini!. Urithi pekee wa kuwaachia watoto sio mali, ni elimu. Baada ya kueleza wale 8, hakuna aliyesoma St.Kayumba, naomba itoshe ili nisi brag!. Maadam mimi jina langu ni brand name, just keep listening to brand Pascal Mayalla, utawajua tuu wako wapi and who are they!, hakuna anayeachiwa mali yoyote zaidi ya good education, the rest watajibeba!, hata huyu Pascal Mayalla Jnr, hatasoma St. Kayumba, kwa kipato hicho hicho unachodhani nakitegemea!.
P
 
This is where masikini wa roho kama wewe go wrong!. Unaamini kuwaachia watoto mali, ndio kuwasaidia!. Mimi mwenyewe kwetu tumezaliwa 8, na hakuna yeyote aliyefanikiwa Kwa kutegemea kaachiwa nini!. Urithi pekee wa kuwaachia watoto sio mali, ni elimu. Baada ya kueleza wale 8, hakuna aliyesoma St.Kayumba, naomba itoshe ili nisi brag!. Maadam mimi jina langu ni brand name, just keep listening to brand Pascal Mayalla, utawajua tuu wako wapi and who are they!, hakuna anayeachiwa mali yoyote zaidi ya good education, the rest watajibeba!, hata huyu Pascal Mayalla Jnr, hatasoma St. Kayumba, kwa kipato hicho hicho unachodhani nakitegemea!.
P
Watu tumeona vivid examples jinsi wanaume waliozaa uzeeni wanavyohangaika na watoto wadogo...anyway utajiju its your life,its your choice
 
Watu tumeona vivid examples jinsi wanaume waliozaa uzeeni wanavyohangaika na watoto wadogo...anyway utajiju its your life,its your choice
This is the reason behind kupandisha bandiko hili, limefuatiwa na makala ya kina kwenye Nipashe la Leo, na kipindi cha TV cha uelimishaji umma kuhusu secure investment kwa wastaafu watarajiwa kitafuata na naamini kitasaidia wengi.

P
 
Back
Top Bottom