G
guest-1787677786
Guest
Na declare interest. Mi ni Baba wa watoto 4 wote wa kike. Mtoto Mkubwa yupo Form 3 na mdogo yupo Class four.
Kwanza nashukuru Mungu kwa kunipa mabinti 4. Kimsingi baada ya wawili wa kwanza kuwa wa kike, nikiongea hao wengine niliamini nitapata kidume nyumbani kwangu.
Hawana changamoto yoyote na wanaendelea na masomo vizuri tu wakiwa na afya na ukuaji mzuri ila kama baba kuna muda napata mawazo kwa kukosa mtoto wa kiume. Naogopa kuongeza kwa huyu mama kwani tunaweza ambulia wa kike tena.
Kimsingi sasa natafuta niweke mbegu huko Pembeni nipate kidume na nimlete kumlea na hawa wenzake. Kuna changamoto nyingi kwa nyumba kukosa mtoto wa kiume.
Changamoto ya Kwanza ndio mrithi wa familia na atakayeendeleza Jina na damu yangu. So kukosa mtoto wa kiume hadi sasa sina mrithi wa mali yangu na atakayeendeleza jina langu.
Pili, kushindwa kufanyika kwa baadhi ya kazi nyumbani kama utunzaji wa mifugo na mbwa ninazofuga, kukosa wa kunichinjia mbuzi au kuku.
Changamoto ya tatu, kukosa wa kuniuguza uzeeni ambaye atanisaidia pia kama mwanaume mwenzake.
Changamoto ya nne kukosa mlinzi na msimamizi wa nyumba kipindi nasafiri kwani huwa nasafiri sana kikazi na kibiashara.
Kimsingi, ni ngumu sana nyumba kukosa mtoro wa kiume. Sasa natafuta mwanamke ambaye atakuwa tayari kuzaa nami na nitamfungulia na kumjengea alee mwanangu na akiwa na miaka 7, nachukua mwanangu.
Ni raha sana kuwa na jamaa anayecheza mpira hapa nyumbani na atakayeniletea kesi za kutia mimba huko nje.
Je wewe mwenye watoto wa kike tu, una changamoto zipi?