Changamoto za Malezi: Ukigundua umemkosea mtoto wako mdogo huwa unafanya nini? Unamnunulia anachokipenda (chips), unamuomba msamaha au unapotezea tu?

Changamoto za Malezi: Ukigundua umemkosea mtoto wako mdogo huwa unafanya nini? Unamnunulia anachokipenda (chips), unamuomba msamaha au unapotezea tu?

Just imagine umemchapa mtoto kwa kumhisi anang'ata buttons za remote controller ya TV kumbe sio yeye bali ni panya ndio wanaharibu...
Aiseee! Jana tu nimenunua remote nyingine sababu hiyo ila kujua nan ameng'ata ni mtihani
 
Siwezi kumuadhibu mtoto pasipo kuwa na kikao Cha maongezi Kati yangu na yeye..lazima niongee Naye na nijue Kama amekosea au lah..Kama amekosea nitamkanya au kumdunda kabisa na kumwambia alichofanya si sahihi..uzuri huyu kijana wangu anaelewa Sana na hata akikosea Ni mwepesi kukubali kakosea.
Bado sijakutana na hali ya kuomba msamaha kwa mtoto.
 
Siwezi kumuadhibu mtoto pasipo kuwa na kikao Cha maongezi Kati yangu na yeye..lazima niongee Naye na nijue Kama amekosea au lah..Kama amekosea nitamkanya au kumdunda kabisa na kumwambia alichofanya si sahihi..uzuri huyu kijana wangu anaelewa Sana na hata akikosea Ni mwepesi kukubali kakosea.
Bado sijakutana na hali ya kuomba msamaha kwa mtoto.
Mkuu,unapomlea mtutu,unapomuadhibu mtoto,unpoongea mtoto,lengo lako la msingi ni nini?Mimi Mtoto wangu kuanzia umri wa 0- 5 ni bakora kisha aongezi then 6-10hapo maongezi kisha bakora.Akifika 10+ ni maongezi na kofi moja akifika 3+ tunajadiliana akiwa na uwezo wa kubuild case yake,akawa muwaza na akaonesha kujiamini basi tunarekebishana vizuri tu.Binafsi naamini kwamba Katika malezi bakora ni muhimu ila sio lazima.ILA NAAMINI KWA ASILIMIA 1000 kwamba mzazi hakosei katika malezi.NEVER.Ukiona umemuadhibu mtoto kwa kosa ambalo hajafanya ujue ana role ameplay kwenye hilo kosa ila huna ushahidi.Malezi sio kuhusu ushahidi ni kuhusu PRINCIPLES.

Kazi yako mzazi ni kumfundisha MTOTO wako PRINCIPLES haki,na ushahidi atajifunza mwenyewe.
 
Muombe msamaha na kwa kufanya hivyo utakuwa umemfundisha maisha ya kuomba msamaha wengine atakapojua amewakosea na itakuwa faida kwa mtoto na kwa wewe mzazi na ndipo sasa atakuwa ktk kimo na akili akimpendeza Mungu na wanadamu!
 
Mtoto akikosewa anaombwa msamaha kabisa,yeye ndipo anapojifunza kuwa akikosea naye aombe msamaha.maisha ya famiia ni uwazi na ukweli ndiyo hunogesha mahusiano,hata km ni mtoto wa kindergaten unamwomba tuu.mf ohh mwanangu nilikosea nilipokugombeza kumbe siyo wewe uliyemwaga maziwa,nisamehe mwanangu,then una mb
mzazi hakosei? Kwani kuna mzazi malaika? Hapo tunajifariji kwa ajili ya kuogopa kushuka,shuka ndugu hapo ndipo penye unyenyekevu
Mkuu hapana mkuu.

Mtoto haombwi msamaha aisee,

Kwanza kwa nini umkosee mtoto ?


Yaani haiwezekani kabisa unampiga mtoto kwa sababu remote imetafunwa kwa hiyo moja kwa moja ukajua kuwa ni yeye.

Kwa nini uhisi kwamba ni yeye moja kwa moja ?

Wazazi wanaokosea kuwaadhibu watoto wao wanakuwa wakorofi ama wana shida fulani katika malezi.

Na inakuwaje umpige mtoto hata kama anakuambia kuwa hilo sijafanya mimi.

Lazima uchukue hatua kadhaa kuchunguza jambo.

Unapoomba omba msamaha kwa kumkosea mwanao na yeye unamjengea mindset ya KUKURUPUKA KURUPUKA TU na kukosea kosea tu.

Mimi mpaka natoka home sikumbuki kama niliwahi kupigwa kwa kosa la kusingiziwa.

Katika moja ya misingi ya malezi niliyojifunza kwa wazee wangu ni kuwa
MARUFUKU KUMUADHIBU MTOTO KWA KOSA AMBALO HUJAMKAMATA NALO,HUNA USHAHIDI WA MOJA KWA MOJA.

Hapa yunaweza kumuonya tuu kwamba kitu hiki asifanye
 
Rais Magufuli atatufikisha tu kama ndani ya miaka minne ametufikisha uchumi wa kati haitachukua muda kumfikia USA.
 
Rais Magufuli anafanya kazi kubwa wazo la kumuongezea muda ni wazo zuri sana.
 
Lini hii nchi iliwahi kuwa na maadili mazuri?

Ndio maana tuna taifa la viongozi na wananchi waongo, wakaidi, wanafiki na makatili kwa sababu walifanyiwa ukatili utotoni. Walipuuzwa na kusiginwa akili zao.

Mtoto anapaswa kujua maana na thamani ya kuomba msamaha na kuwajibika kwa makosa aliyoyafanya. Atambue kosa ni nini na kwanini naadhibiwa!

Sio kupiga piga tu watoto hovyo kama ng'ombe. Wakiwa wakubwa wanageuka kuwa haya majambazi yasiyotaka hata kukosolewa.

Kumbe chanzo ni udikteta wa baba nyumbani!
Nadhani umetumia hisia sana kuandika hapa. Kunywa maji ya kutosha relax.

La kukuongezea tu siku hizi akiharibika samaki mmoja si wote pia hatupwi anika ule samaki mkavu (ng'onda)

Viongozi waongo wapo na wakweli pia wapo hivyo hivyo kwa raia wengine ndani ya Tanzania hii.
 
Back
Top Bottom