Changamoto za mfumo wa maombi ya ajira za Elimu na Afya 2022

Kwa hiyo ni kosa la nani
Vipi kuhusu mitandao kama Google', facebook, jamiiforums nk yenye watumiaji wengi kuliko hiyo ya tamisemi?
Sasa ndugu yangu huoni kama unataka ufananishe mbigu na ardhi kama wasemavyo waswahili

Yani unataka upambanishe servers za makampuni kama facebook na google na servers za TAMISEMI kweli?

Kosa sio la mtu wa IT ndugu ,sema jaribu kupeleka hizi lawama kidogo kwa wizara yako kwanza

Naomba niulize swali dogo la kizushi, hivi walimu huwa wananua vitabu vya kufundishia vingine pale wanapogundua vilivyopo havikizi mahitaji ya mtaala?
 
NIDA nimeweka yangu, naulizwa maswali najibu kwa ufasaha ila kila swali wanasema nimekosa.
Sijui tatizo huenda likawa wapi?
 
Wakuu barua ya maombi inaandikwa kwa mkono au inabidi itypiwe?
Kuwa serious basi kijana.... Yani uandike kwa mkono maombi ya kazi katika ulimwengu wa sasa?[emoji23][emoji23][emoji23]

Type hiyo barua, print kisha weka saini, kisha scan upate soft copy ya ku upload kwenye sehemu yake.
 
Naomba kuuliza wapendwa mbona Kwenye kuselect kozi bachelor of education in arts Hamna??? Au hiyo kozi haipo kwenye maombi??
 

tunaelewa. Ila kuna form hazikulishwa options, ambapo bila option fulani kuchaguliwa haiendelei mbele. hatujasoma IT ila mfumo huu tunaufananisha na (Google forms) kuna wakati ukilazimisha mandatory fields kwamba bila hizo kujazwa haifungui kipengele nkinachofuata.


mfumo ulikosa baadhi ya taarifa za msingi
Sasa kama kwa kifupi sana jambo liko hivi kosa la IT wa bongo ni lipi sasa hapa?

natamani nikujibu. ila ngoja tu ninyamale
 
Mimi nahisi wanataka walim wa science, early childhood education na adult education wajaze wao pwanza afu ndio tufuate sie tusiokipaumbele . Mwisho wa siku waseme mfumo ulimchagua aliyewah kuomba
 
Naomba kuuliza wapendwa mbona Kwenye kuselect kozi bachelor of education in arts Hamna??? Au hiyo kozi haipo kwenye maombi??
Haaa sio iyo tu ata kwa Science wanakuletea Bachelor of Science with Education Chemistry na Biology tu kwa Udsm
 
WUNGWANA NAOMBA KUULIZA VIPI CHETI CHA KUZALIWA WANACHOTAKA KIWE UPLOADED PALE MWANZONI TUNAWEKA pdf YA CHETI ORIGINAL AU COPY?... NA VIPI NA CHENYEWE KINATAKIWA KUWA CERTIFIED?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…