A
Anonymous
Guest
Naomba kuwasilisha kilio cha wafanyakazi wa afya kutoka mikoa ya pembezoni kama Kigoma, Mara, Kagera, na Katavi, ambao wamepata nafasi ya kujiendeleza kimasomo lakini wanakutana na changamoto kubwa sana ya kifedha.
Wafanyakazi hawa, wakiwemo manesi, madaktari, na hata wanaosomea udaktari bingwa na ubingwa bobezi, wamekuwa wakijigharamia masomo yao kwa hali ngumu sana. Licha ya wao kuwa chini ya Wizara ya Afya na kufanya kazi katika hospitali za serikali, hawapati msaada wowote wa kifedha wanapokuwa masomoni.
Kinachoumiza zaidi ni kwamba:
Wanapoomba hata msaada mdogo (mfano laki 5 kwa mwezi), hujibiwa kwa barua kuwa hospitali haina fedha.
Wakati huohuo, kuna taarifa kuwa bajeti hutengwa kwa ajili ya kusaidia wafanyakazi walioko masomoni—lakini haijulikani fedha hizo zinaenda wapi.
Baadhi ya hospitali hizi pia zimekuwa zikilalamikiwa kwa ubadhirifu wa rasilimali na uongozi usio na uwajibikaji.
Matokeo ya hali hii ni mabaya kwa mfumo mzima wa afya:
- Wafanyakazi wengi wanasoma kwa tabu kubwa, wakikopa au kuuza mali zao.
- Wanapomaliza masomo, wanashindwa kurudi kwenye vituo vyao vya kazi kutokana na madeni na mazingira magumu waliokutana nayo.
- Wengi wanakimbilia sekta binafsi ambako wanaweza kupata kipato cha haraka ili kulipa madeni yao.
Hii inaleta upungufu mkubwa wa wataalamu katika mikoa ambayo tayari ina uhaba mkubwa wa watumishi wa afya.
Cha kushangaza zaidi, wakati wafanyakazi hawa wanapomaliza masomo:
- Wanatarajiwa kurudi kazini mara moja,
Na kuna msimamo unaojitokeza wa kuzuia hata likizo bila malipo baada ya masomo.
Swali la kujiuliza:
Ni haki kwa mfanyakazi kujisomesha kwa gharama kubwa bila msaada wowote, halafu bado abebeshwe mzigo wa kurejea mara moja bila kupewa nafasi ya kujipanga kifedha?
Wito kwa Serikali (Wizara ya Afya):
Serikali kupitia Wizara ya Afya inapaswa Kufanya uchunguzi wa kina katika hospitali za mikoa ya pembezoni kubaini matumizi ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya wafanyakazi walioko masomoni.
Kuweka mfumo wa wazi na wa haki wa kusaidia wafanyakazi wanaojiendeleza kimasomo.
Kuwawajibisha viongozi wa hospitali wanaoshindwa au kukataa kutoa msaada kwa wafanyakazi wao.
Kutoa motisha ya kurejea kazini, ikiwemo angalau muda wa mpito au msaada wa kifedha baada ya masomo.
Kurahisisha upatikanaji wa ruhusa ya kwenda kusoma, badala ya wafanyakazi kupambana kwa muda mrefu kupata nafasi hiyo.
Kama taifa tunahitaji wataalamu wa afya waliobobea—lakini hatuwezi kuwategemea ikiwa tunawaacha wapambane peke yao wakati wa kujifunza.
Serikali ichunguze na kuwasiliana na watumishi hawa kutoka mikoa ya Mara, Katavi, Kagera,Rukwa, Ruvuma kwa taarifa zaidi.
Ni wakati sasa wa kuchukua hatua.