#COVID19 Chanjo - Mrejesho: Wizara tambueni changamoto hizi

Wewe unafikiri hivyo vidonge havitokani ni miti shamba? Hujawahi kuugua wewe siku ukiugua na dawa za kizungu zikadunda na ikabidi uponyeshwe na miti shamba ndiyo akili zitakurudia.
 
Wewe unafikiri hivyo vidonge havitokani ni miti shamba? Hujawahi kuugua wewe siku ukiugua na dawa za kizungu zikadunda na ikabidi uponyeshwe na miti shamba ndiyo akili zitakurudia.

Haijulikani unataka au hutaki nini. Chawa wa mwendazake proper
 
Nimefanya booking ya kuchanjwa tarehe 7 lkn Leo ndio Nina nafasi nzuri hivi naweza enda leo kituoni na nikapokelewa?
 
I don't talk with demons
 
Ukipata madhara uje tukuchangie wale vimbelembele 10 wa mwanzo tutawachangia
Hapo ulipo tu lazima kuna kitu kina madhara kwako. Hata hiyo simu unayotumia, ina mionzi yenye madhara. Wanaotaka chanjo waacheni ni hiyari yao, nyie mnaoamini kuwa kuna wazungu wanataka kuwaua mkajifiche, hata chini ya mawe!
 
Upate chanjo kutoka wapi zimekuja 1M tupo almost 65M. Ukifanikiwa kupata mshukuru sana Mungu wako.
 
Mrejesho - day 2 (3rd Aug):

Hatukupokea simu yoyote tofauti na tulivyo ahidiwa. Kama tulivyodhamiria tukaamua kivyetu vyetu tukatia timu.

"Mambo bado" --- mtoto mzuri Tshimanga Assosa.

Tumeambiwa tutapigiwa simu tuwe na subira, kwani hata wafanyakazi wa afya wote wa mkoa huu na hata wa mikoa yote ya jirani pia bado hawajachanjwa na haijulikani watachanjwa lini.

Hivyo tuendelee tu kusubiri simu. Haijulikani simu zitakuja lini.

Tumedhamiria kufuata wayasemayo hadi mwisho. Labda nyama ziko chini, nani ajuaye?

Kwa kweli kama ilivyokuwa kwa magoma moto moto ya disko agwaya - "mambo bado!"
 
Upate chanjo kutoka wapi zimekuja 1M tupo almost 65M. Ukifanikiwa kupata mshukuru sana Mungu wako.

Chanjo naitaka si mimi tu bali na jamaa zangu. Ndiyo maana nimefika kuliko na the down trodden. Hawa si wa Mzena tu bali hata simu na vitambulisho hawana.

Hata hivyo mimi ni nani kulazimishana kupata chanjo kama haipo? Kwangu mimi kuuona utopolo wote kama ulivyo, inatosha sana.

Kwani utalii wa ndani ni Burigi peke yake?

Wewe hujui kuwa tuko uchumi wa kati, tozo za miamala na kodi juu?

Hawa wanaozidi kukamuliwa ndiyo hao hao ambao pia kwenye chanjo labda ni daraja la 2.

Unasomeka vyema mkuu.
 
Mrejesho - day 3 (4th Aug):

Tunaendelea kusubiria. Bado hakuna simu wala updates.



Kama hata wafanyakazi Bugando mambo bado kwani sisi nani?
 
Sisi tuliochanja Mbagala Jumanne 03 hakukuwa na tatizo lolote, wote waliofika walichanjwa
 
Mrejesho - hatimaye napata chanjo:

Hatimaye tulipata simu kufika kwa ajili ya chanjo. La msingi tulichanjwa. Chanjo ni muhimu. Changamoto zake haziizidi thamani yake.

Yaliyojiri na yatokanayo kwa hakika yanastahili uzi kamili.
 
Sikufanya buking'i, nilienda nikaunga foleni na nilipoifikia meza ya kujiandikisha nikaandikwa kisha nikaenda kuchanja fyuiiiiiii.
 
Sikufanya buking'i, nilienda nikaunga foleni na nilipoifikia meza ya kujiandikisha nikaandikwa kisha nikaenda kuchanja fyuiiiiiii.View attachment 1887128

Bongo darisalama haiwezi kuwa sawa buseresere Chatto.

Kulikosemekana buking'i ilikuwa kununua muda. Chanjo zilisafirishwa kwa takribani gari moja moja kwa kila kanda.

Baada ya recuperate na ka aftermath ka hii chanjo si mbaya kuleta mrejesho funga wa hili zoezi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…