mtimawachi
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 2,108
- 3,155
Mkuu MBOWE wetu yupo selo,tuchangishane tukamtoe!Hii inaitwa kisebu sebu na kiroho papo.
Tokeni Lumumba mkasome!
Hoja mkononi imewazidi kimo.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu MBOWE wetu yupo selo,tuchangishane tukamtoe!Hii inaitwa kisebu sebu na kiroho papo.
Tokeni Lumumba mkasome!
Hoja mkononi imewazidi kimo.
Mkuu siasa naiona itaingia pale ambapo chanjo itaanza kutolewa kiulazima, Mbowe kwa maneno yake mwenyewe amesema "chanjo haitakiwi kuwa hiari, huo sio utaratibu wa WHO"...huo ni upotoshaji, chanjo ni hiari, kinachotakiwa ni kutengenezwa mazingira ya kuwafanya raia wengi wawe tayari kupokea hiyo chanjo, tukianza kutafutana tupigwe sindano mwisho wa siku huko vijijini wahudumu wa afya wanaweza kuingia matatizoni kama kuuwawa kwa maana hoja potofu nyingi kuhusiana na hii chanjo zimeshaenea nchi nzima. Ni bora nguvu kubwa itumike kuelimisha jamii, kuishawishi jamii kuona manufaa ya chanjo ya corona...ni kama sera ya uzazi wa mpango, ni muhimu kwa mustakabali wataifa ...lakini kwa taratibu za kiafya haijafanywa kuwa ni lazima kila mtu aifuate, elimu ndio hutolewa zaidi vinginevyo wangekuwa wanawinda watu kuwadunga sindano, kufanya vasectomy ama kuwamezesha vidonge. Kwenye suala la chanjo ninasisitiza iwe ni hiari, tuna uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa kupitia njia hiyo kuliko kulazimishana.Mkuu siasa unaiona wapi kwenye nukuu hii?
View attachment 1861894
Hata hivyo nisiache kukueleza hatimaye nimekuja kufahamu kuna upotoshaji mkubwa wa makusudi kwenye aliyosema Mbowe:
Hotuba ya Mbowe Mwanza Ilivyopotoshwa ili Kuuficha Ukweli
Ninalazimika kuuleta uzi huu baada ya hatimaye kupata nafasi kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mheshimiwa Mbowe: Katika hotuba hii, sioni popote penye tatizo lolote na mtanzania yeyote: 1. Kwamba kuna wagonjwa wa Corona na watu wanakufa nchini kote? 2. Kwamba wahanga hawa wanalazimika...www.jamiiforums.com
Nimelazimika kuondoka uzi huo sasa baada ya kumsikiliza msemaji mwenyewe.
Hakika tuna watu waovu sana baina yetu!
Mandatory vaccination ni nini?Hahaha!
Mkuu, ni kweli haufahamu kabisa kwamba kuna mataifa ambayo yana sera ya mandatory vaccination inayofahamika duniani kote?
Ni kwamba haufahamu kabisa kuhusu sera ya afya ya chanjo ya lazima ama unafanya mzaha tu?
Mimi ni mhanga mtarajiwa wa wazi wa upuuzi unaoendelea hapa. Naweza kugeuka mfu dakika yoyote kwa sababu ya watu hawa. Unaniuliza ya wamarekani? Give me a break!
Wewe ulipo si umeshanjwa?
Ulipo wewe Corona haikuhusu. Ama kweli hawakukosea waswahili waliosema mzigo wa mwenzio kwako ni kanda la sufu(Sufi). Tuko kati ya janga wewe unadhani we are enjoying ourselves?! Tunapambana wenyewe kwani hata kuna hata tulichowaomba?
Iko wapi shida kwenye speech ya Mbowe kwa nchi hii?
Acheni unafiki huku nyie mkiwa salama.
Hatuko wajinga kiasi hicho.
Nonsense!Kwani mna hoja? Kumbe ungali hujaona?
Hotuba ya Mbowe Mwanza Ilivyopotoshwa ili Kuuficha Ukweli
Ninalazimika kuuleta uzi huu baada ya hatimaye kupata nafasi kuisikiliza sehemu ya hotuba ya mheshimiwa Mbowe: Katika hotuba hii, sioni popote penye tatizo lolote na mtanzania yeyote: 1. Kwamba kuna wagonjwa wa Corona na watu wanakufa nchini kote? 2. Kwamba wahanga hawa wanalazimika...www.jamiiforums.com
Huu upumbavu wa kuja na vi ID uchwara vipya vya msimu haulipi tena:
View attachment 1861891
Nendeni shule. Mnasumbuliwa na ujinga zaidi.
Rudini mkawaambie mada mkononi imewazidi kimo. Mlichokuwa mmepanga kimeparaganyika!
Habari ndiyo hiyo.
Hiyo Chanjo nzuri ni ipi?Wewe unayetaka chanjo wasiotaka chanjo wakikulazimisha usipate chanjo utafurahi?
Wewe dai chanjo nzuri uchanjwe.
Mkuu siasa naiona itaingia pale ambapo chanjo itaanza kutolewa kiulazima, Mbowe kwa maneno yake mwenyewe amesema "chanjo haitakiwi kuwa hiari, huo sio utaratibu wa WHO"...huo ni upotoshaji, chanjo ni hiari, kinachotakiwa ni kutengenezwa mazingira ya kuwafanya raia wengi wawe tayari kupokea hiyo chanjo, tukianza kutafutana tupigwe sindano mwisho wa siku huko vijijini wahudumu wa afya wanaweza kuingia matatizoni kama kuuwawa kwa maana hoja potofu nyingi kuhusiana na hii chanjo zimeshaenea nchi nzima. Ni bora nguvu kubwa itumike kuelimisha jamii, kuishawishi jamii kuona manufaa ya chanjo ya corona...ni kama sera ya uzazi wa mpango, ni muhimu kwa mustakabali wataifa ...lakini kwa taratibu za kiafya haijafanywa kuwa ni lazima kila mtu aifuate, elimu ndio hutolewa zaidi vinginevyo wangekuwa wanawinda watu kuwadunga sindano, kufanya vasectomy ama kuwamezesha vidonge. Kwenye suala la chanjo ninasisitiza iwe ni hiari, tuna uwezekano mkubwa zaidi wa kufanikiwa kupitia njia hiyo kuliko kulazimishana.
Hivi hii nchi mbona watu hawajitambui? eti chanjo ni lazima! kachanje wewe siyo uwaamulie watu afya zao. Eti mbowe kasema yeye ni daktari? anajua nini kuhusu huo ugonjwa? harafu nyie mlikuwa wapi awamu ya 5? maana awamu hii mna kihere2 kweli! lazima muwe na mipaka ya kusema, serikali iwadhibiti maana mmekuwa wajinga kupitiliza sasa!
Wanaotaka kuchanjwa wachanjwe....hata hivyo hakuna nguvu ya kuchanja Watu milioni 60.
Utoaji wa lazima wa chanjo ndio huo unaoitwa mandatory vaccination au pia compulsory vaccination. Ni utaratibu ambao umekuwepo miaka mingi.Mandatory vaccination ni nini?
Mbowe kasema Watanzania wote walazimishwe chanjo.
Ndiyo hiyo mandatory vaccination unayoongelea?
Nchi gani inalazimisha watu wote wachanjwe?
Unaelewa kwamba hizi chanjo mpaka sasa hazijapata final approval (mfqno chanjo za Marekani hazijqpqtq final approval kutoka CDC) na zinatolewa kwa ememergency approval tu?
Hao Wamarekani wenyewe ambao wametengeneza chanjo zao hawalazimishi watu wao chanjo. Sisi tunaopewa tu chanjo ndiyo tumewazidi ujanja kutaka watu wote wachanjwe?
Wewe unaelewa kwamba si kila mtu ana hali inayofaa kupewa chanjo? Kuna wengine wenye low immunityna ukiwapa chanjo ndiyo unaongeza risk yao kufa? Tanzania wako wangapi hawa? Ukilazimisha wachanjwe halafu wakafa kutokana na chanjo utakuwa umewasaidia?
Umeitaja Marekani.Utoaji wa lazima wa chanjo ndio huo unaoitwa mandatory vaccination au pia compulsory vaccination. Ni utaratibu ambao umekuwepo miaka mingi.
Ukisema kuwa ni uongo, utaonekana kuwa wewe ndio muongo sababu hiyo sera inafahamika duniani kote. Ndio maana nikakuuliza kwamba hujui ama unaleta utani tu?
Kama ni suala la utani tu halina shida!
Hata huyo Mbowe kwenye hiyo video uliyoileta hapa amezungumza kuhusu hiyo sera. Kuna sehemu ameitaja kabisa "mandatory". Umefanya jambo zuri sana kuileta hiyo video.
Ukimsikiliza, anasema kuwa nchi za wenzetu chanjo ni lazima, ila wameanzia kutoa kwanza kwa wahudumu wa afya walio mstari wa mbele wa mapambano, wakifuatiwa na makundi maalumu, taasisi na kuendelea.
Hicho ndicho kinachoendelea kwa nchi kama Ufaransa, Uingereza, Italia, Ugiriki, Urusi na hata Marekani hivi sasa.
Marekani hivi sasa kuna vaccine mandates katika ngazi za taasisi na kampuni. Nafikiri, jana tumejadili hili na nikasema kuhusu hilo suala la "final approval" ya chanjo. Nikakuambia kwamba, tusubiri chanjo zipate full approval kutoka FDA. Isitoshe, siku si nyingi hilo litakamilika jambo litakalochochea kuongezeka kwa chanjo za lazima (vaccine mandates).
Suala la chanjo kuwa lazima nchi nzima kwa utaratibu unaofaa linaanzia kwa makundi ambayo yametajwa na Mbowe katika hiyo video. Isitoshe chanjo kuwa lazima haimaanishi kwamba serikali itatumia nguvu ya dola kulazimisha watu watoke kwenye nyumba zao kwenda kuchanjwa. La hasha!
Serikali inatunga sera ya kuhakikisha kwamba:
1) Chanjo zinapatikana kwa urahisi mahali pote nchini.
2) Kunakuwepo na vikwazo laini kwa wale wasiochanjwa kama vile kutoruhusiwa kuingia katika maeneo fulani yenye mikusanyiko ama kufanya kazi katika taasisi mbalimbali n.k.
3) Anayegoma kuchanjwa halazimishwi kwa nguvu ila tu atahitaji kufanya hivyo kama atataka kupata ajira mahali fulani ama kupata huduma fulani ya kiserikali.
Hiyo ndiyo maana ya mandatory vaccination na hii inafanyika katika hali ya dharura ambayo ni moral justifiable kama nilivyosema. Isitoshe, kabla zoezi la chanjo kufikia nchi nzima (population-wide), lazima lianzie kwa makundi fulani yaliyo hatarini zaidi kama alivyosema Mbowe.
Naweza nisikubaliane naye katika masuala kadhaa ila kuhusu hilo suala la chanjo za lazima ni suala halisi na linafanyika kwa utaratibu maalumu unaokubalika kimataifa.
Nimalizie kwa kusema kuwa, ninakushukuru tena kwa hiyo video uliyoileta. Nafikiri imesaidia pakubwa sana kutujibia maswali kadhaa kuhusiana na mjadala huu ambao tumeujadili hapa kwa muda sasa.
Maadili ya kitabibu yenyewe yanakataza kulazimisha chanjo.Hivi mfano chanjo ikawa inaleta complications za kiafya kwa raia , ni nani atawajibika na maisha yao na afya (assume hizo complications ni irreversible)?!
Huwezi lazimisha mtu kuweka makitu kwenye mwili wake na hajui yataleta shida gani.
Mkiendelea kulazimisha hivi siku mtalazimisha watu kushare personal info zao au kuwalazimisha wale vyakula wasivyotumia.....
Kwa nini swali liwe mimi au wanasayansi wa Ulaya?Hiyo Chanjo nzuri ni ipi?
Ni nani anayeamua kwamba chanjo hii ni nzuri au mbaya?
Wewe ama wanasayansi wa ulaya?
Mkuu, umesoma lakini kile nilichoandika?Umeitaja Marekani.
Marekani imelazimisha wananchi wote wachanjwe?
Mbowe karopoka kwamba Watanzania walazimishwe chanjo.Mkuu, umesoma lakini kile nilichoandika?
Nimeeleza kuhusu hiyo sera anayoisema Mbowe ya mandatory vaccination pamoja na vaccine mandates. Sera hiyo pia inatumika nchini Marekani.
Kuropoka ama kutokuropoka si hoja hapa.Mbowe karopoka kwamba Watanzania walazimishwe chanjo.
Hajatoa nuanced position.
Marekani uliyoitaja haina utaratibu wa chanjo kuwa ya lazima kwa watu wote.Kuropoka ama kutokuropoka si hoja hapa.
Yeye amesema kuwa, uwekwe utaratibu wa chanjo kuwa lazima kwa watu wote.
Lakini, hajaishia hapo tu, pia amesema kuwa utaratibu wa chanjo hizo kama ulivyo kwa nchi zingine, unaanzia kwa makundi yaliyo katika hatari zaidi katika nchi, na ameyataja.
Nuanced position gani hajatoa?