#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

EEti Chairman Mao?🤣🤣🤣 Yule mchina aliacha mamilioni wanakufa kwA njaa huku yy akizunguka nchi na pleasure squad iliyoundwa na vigori
 
EEti Chairman Mao?🤣🤣🤣 Yule mchina aliacha mamilioni wanakufa kwA njaa huku yy akizunguka nchi na pleasure squad iliyoundwa na vigori

Akili za kuambiwa changanya na za kwako:

Usipofanya hivyo ukiitwa kichwa panzi usijesema umetukanwa 😂😂😂😂!
 
Mimi ni mhanga mtarajiwa wa wazi wa upuuzi unaoendelea hapa. Naweza kugeuka mfu dakika yoyote kwa sababu ya watu hawa. Unaniuliza ya wamarekani? Give me a break!

Wewe ulipo si umeshanjwa?

Ulipo wewe Corona haikuhusu. Ama kweli hawakukosea waswahili waliosema mzigo wa mwenzio kwako ni kanda la sufu(Sufi). Tuko kati ya janga wewe unadhani we are enjoying ourselves?! Tunapambana wenyewe kwani hata kuna hata tulichowaomba?

Iko wapi shida kwenye speech ya Mbowe kwa nchi hii?

Acheni unafiki huku nyie mkiwa salama.

Hatuko wajinga kiasi hicho.
Nonsense!

Umeulizwa nchi gani inalazimisha chanjo?

Umebaki kuhara tu.... manenoo meeengii... upuuzi mtupu!
 
Msikilize Chairman Mao kuanzia dakika ya 6 hapo. Kwanza anadanganya kusema kwenye nchi za wenzetu chanjo ni lazima, nchi gani hizo?

Hahaha!

Mkuu, ni kweli haufahamu kabisa kwamba kuna mataifa ambayo yana sera ya mandatory vaccination inayofahamika duniani kote?

Ni kwamba haufahamu kabisa kuhusu sera ya afya ya chanjo ya lazima ama unafanya mzaha tu?
 
Acheni ukuda wenu.
Mimi nikifa wewe unaumia nini? Lazima lazima ndio sitakufa au?

Acheni mambo ya ajabu bana. Hata wakisema leo lazima, sichanji ni bora waniue kuliko kuchanja.

Et unachanja kisa li ugonjwa la kutunga. Ujinga bana. Nikichanja then what? Sitaumwa? Sitakufa? I fear nothing to die when right time comes..
Watu wanaogopa kufa ilhali wanajua watakufa.
Na wapo walochanjwa na bado wamekufa kwa mambo mengine
 
Watu wanaogopa kufa ilhali wanajua watakufa.
Na wapo walochanjwa na bado wamekufa kwa mambo mengine
Chakula kinaliwa kila siku ingawa watu watakufa.

Watu hutibiwa hospitalini mara kwa mara ingawa watakufa.

Kifo hakiwafanyi watu wagome kula ama kwenda kutibiwa hospitalini.

Ni ujinga tu, tena wa hali ya juu ndiyo ambao unaweza kuwafanya watu wagome kula ama kutibiwa eti kwa sababu hata wakila ama kutibiwa bado watakufa.
 
Mkuu kama kula hata miti inakula,kama kutibiwa hata mimea na wanyama hutibiwa.
Kula ni nature,ila hata chanjo ni tiba.Tunachopinga ni mazingira ya chanjo hii,yaani hadi MBOWE kawa waziri wa afya
 
Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:

"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."

Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.

Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.

Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.

Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.

Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.

Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.

Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.

Hiiiiii bagosha!

Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.

Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?

Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.

Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.

Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.

Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.

Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!
Mwenye AKILI TU ndio WATAMWELEWA MBOWE

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Watu wanaogopa kufa ilhali wanajua watakufa.
Na wapo walochanjwa na bado wamekufa kwa mambo mengine

Hatutaki kufa kijinga ila kufa hatuogopi:

IMG_20210720_163541_767.jpg

Mkuu kama kula hata miti inakula,kama kutibiwa hata mimea na wanyama hutibiwa.
Kula ni nature,ila hata chanjo ni tiba.Tunachopinga ni mazingira ya chanjo hii,yaani hadi MBOWE kawa waziri wa afya

Kuna upotoshaji mkubwa wa makusudi na wenye maslahi binafsi ya kisiasa kwenye suala hili:

Hii bila kujali kuwa maisha ya watu wasio na hatia yanapotea. Mbaya zaidi wanaofanya hivi wao wako salama.

Ndiyo, ubinafsi uliopitiliza.
 
Mwenye AKILI TU ndio WATAMWELEWA MBOWE

Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app

Kuna upotoshaji zaidi. Msikilize mwenyewe kuona:

Tunayoyasikia kumbe ni kelele za vyura tu.
 
Mkuu unamuonea tu,uwezo wake wa kupambanua mambo ndio ulipofikia na kwa upande ule yeye ndo akili kubwa

Hii inaitwa kisebu sebu na kiroho papo.

Tokeni Lumumba mkasome!

Hoja mkononi imewazidi kimo.
 
Mkuu tukiacha wanasiasa walazimishe masuala ya afya ndipo tunapotengeneza matatizo makubwa zaidi, ni kama Makonda alivyotaka kuwapima wanaume wa Dar Tezi dume, hiyo si sawa ! Chanjo ibaki kuwa hiari
 
Nonsense!

Umeulizwa nchi gani inalazimisha chanjo?

Umebaki kuhara tu.... manenoo meeengii... upuuzi mtupu!

Kwani mna hoja? Kumbe ungali hujaona?

Huu upumbavu wa kuja na vi ID uchwara vipya vya msimu haulipi tena:

IMG_20210714_085240_006.jpg

Nendeni shule. Mnasumbuliwa na ujinga zaidi.

Rudini mkawaambie mada mkononi imewazidi kimo. Mlichokuwa mmepanga kimeparaganyika!

Habari ndiyo hiyo.
 
Waungwana wanadadavuwa kuwa sababu za vifo ni 4:

View attachment 1861636

Kwa mujibu wa:

Sina taabu na kufa au ndugu na jamaa yangu yeyote kufa kwa sababu yoyote isipokuwa #2 na #4.

#2 na #4 tutawajibishana tu hata kama nitakuwa binafsi zipo duniani:

Kama kwenu maisha hayana thamani si kwa wote.

Chanjo ni hiari.
Naona umekubali kuwa chanjo ni hiyari
 
Mkuu tukiacha wanasiasa walazimishe masuala ya afya ndipo tunapotengeneza matatizo makubwa zaidi, ni kama Makonda alivyotaka kuwapima wanaume wa Dar Tezi dume, hiyo si sawa ! Chanjo ibaki kuwa hiari

Mkuu siasa unaiona wapi kwenye nukuu hii?

IMG_20210720_094159_438.jpg

Hata hivyo nisiache kukueleza hatimaye nimekuja kufahamu kuna upotoshaji mkubwa wa makusudi kwenye aliyosema Mbowe:

Nimelazimika kuondoka uzi huo sasa baada ya kumsikiliza msemaji mwenyewe.

Hakika tuna watu waovu sana baina yetu!
 
Naona umekubali kuwa chanjo ni hiyari

Lini hatujasema hivyo?!

Uko nyuma sana ya matukio mkuu 😂😂😂😂 !!

IMG_20210720_114420_251.jpg

Someni vijana. Ni aibu kutokea kama umekurupuka kutokea chooni na suruali mkononi 😂😂😂😂!
 
Back
Top Bottom