Naomba unipe maana halis kwann mtu anachomwa chanjo?...tuanzie hapo...na chanzo maana yake nin...
Mfano mim nishaumwa korona.wadudu walishaingia mwilin mwangu...mwili ukatengeneza kinga ukapambana nikapona...maana yake nina kinga tayar..
Chanjo nijuavyo mim ni kwamba unaingiziwa wadudu mfu ili mwilk wako utambue na kutengeneza kinga dhid ya hao wadudu...
Sasa kwasisi ambao tushaumwa korona tukapona..mnatulazimishaje tudungwe chanjo?
Mkuu sikuwa nimeiona comment yako hii kabla. Bila shaka kutokana na kuwa imekuwa ni siku ndefu yenye uhitaji mkubwa na kuweka kumbukumbu nyingi sawa sawa.
Kujibu maswali yako:
1. Kwa nini mtu anahitaji kuchomwa chanjo?:
-- kwa kawaida mwili una namna kujikinga (antibodies) na viingiavyo mwilini vyenye kuweza kuleta magonjwa (antigens).
-- kila antigen inahitaji antibody yake.
-- mwili unaposhambuliwa na antigen fulani, huugua wakati ukipambana kutengeneza antibody husika.
-- mwili ukisha tengeneza antibody husika sasa unakuwa unaijua antigen hiyo na kuwa uko tayari kwa mpambano.
-- si antibodies zote zinabakia mwilini siku zote.
-- antibodies za Corona kwa mfano hubakia mwilini kwa takribani miezi 5.
-- antibodies za ebola hubakia kwa muda mrefu zaidi ambapo hata ni sahihi kusema mtu akiugua ebola hawezi kuugua tena.
2. Kwa nini mtu anachomwa chanjo?:
-- mtu anachomwa chanjo ili kuufanya mwili kutengeneza antibodies kabla ya hatari.
-- hii huwa si tu kuwa ni wadudu waliodhoofu peke yake.
-- wanaweza kuwa ni wadudu dhoofu yaani walioodhofishwa, au waliokufa, au hata vipande (au kipande chao) yaani inactivated, attenuated, particles au wakiwa wafu.
-- si haba kukubali kuwa beberu yuko mbali na si mwenzetu.
-- hivi vikiingizwa mwilini, mwili huhamasishwa kutambua ujio wa antigen mwenye ufanano nao ili kutengeneza antibody stahiki kumsubiria.
-- antigen huyo akija mwili huwa katika nafasi nzuri zaidi ya kupambana naye ukiwa katika afya njema.
3. Kama ulishaugua Corona kwanini kuchanjwa tena?
-- kama ilivyo elezwa kabla antibody kwa Corona kutokana na ugonjwa zinakaa kwa takribani miezi 5.
-- ikumbukwe hizi zinakuja kukiwemo na kusukwa sukwa na ugonjwa wenyewe, kama vita kamili.
-- haiyumkiniki kuuacha mwili ukiwa pia na irreparable damages.
-- ipo tofauti ya maisha ya antibodies za kutokana na chanjo na za kutokana na maambukizi ya ugonjwa mwilini.
-- tofauti hii ikutokana na sababu mbalimbali zikiwamo technologies, dozi na labda pia ile kuwa mwili unapokea kichocheo ukiwa uko mzima.
-- kumbuka chanjo nyingi zina dozi 2 - 3.
-- antibody ya chanjo ina nafasi ya kuwapo kwa muda zaidi ikiwamo hata vikorombwezo zaidi.
Kulikuwa na uzi huu humu jamvini labda pia ungeupitia kwa kumbukumbu zaidi:
Corona: Tunavyongopeana kwenye hili la tiba na chanjo