#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:

"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."

Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.

Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.

Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.

Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.

Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.

Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.

Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.

Hiiiiii bagosha!

Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.

Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?

Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.

Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.

Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.

Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.

Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!
Naomba unipe maana halis kwann mtu anachomwa chanjo?...tuanzie hapo...na chanzo maana yake nin...

Mfano mim nishaumwa korona.wadudu walishaingia mwilin mwangu...mwili ukatengeneza kinga ukapambana nikapona...maana yake nina kinga tayar..

Chanjo nijuavyo mim ni kwamba unaingiziwa wadudu mfu ili mwilk wako utambue na kutengeneza kinga dhid ya hao wadudu...

Sasa kwasisi ambao tushaumwa korona tukapona..mnatulazimishaje tudungwe chanjo?
 
Mleta hoja,mbowe na wengine wote mnaleta ujinga wenu kusema chanjo eti iwe ni lazima, Ubongo wenu umejaa nduwi,

chanjo humlinda aliyechanjwa, hofu yako nini na wasiochanjwa?

Jinga kabisa

Kutokuelewa kwako hakukufanyi wewe kuwa mwerevu na wengine kuwa wajinga kwa maoni yako tu.

No wonder babu Loliondo leo ana kikombe cha kutibu na kuzuia Corona na mamlaka zimeingiwa ganzi wasijue cha kufanya.

Yule babu mnyazi Mungu apishilie mbali ni muhimu kwa uhai wake apate chanjo, avae barakoa na awe mtumiaji mwaminifu wa vipikuzi haraka sana, vinginevyo atakuwa hatarini mno.

Ni bahati mbaya sana kuwa, kwa maslahi binafsi ya kisiasa, wanasiasa wameamua kuukumbatia ujinga wakiacha watu kufa mithili ya kuwatoa kafara.
 
Mkuu huo ni uchaguzi wako. Mapema kwa mwuungwana kama wewe niliandika hii:

View attachment 1860294

Kwamba sana sana Mbowe hakuwa na haja ya kuingia huku kisiasa, lakini si morally au kiuhalisia.

Kwamba hata aliingia huku inaonesha ni kiwango kipi huyu bwana ni a real selfless individual.

Cc: Salary Slip technically @erythrocytes
Haya mawazo yanatazamiwa yawe ktk kipindi cha miaka mingapi ijayo?

Je miaka kumi?

Kama ndivyo, basi haina maaana kabisa ya chanjo!

Unachanjwa na unaishi sawa tu wasiochanjwa kipindi cha miaka miiingi kiasi hiko, halafu bado unatazamia kuna watu wasio chanjwa watakufa, na wakati wewe mwenye chanjo ukiwa na hofu na chanjo yako ikiwa itakubakisha sawa kama ulivyokuwa kabla hujachanjwa ama la!!
 
Chanjwa usiambukizwe, mnahofu gani na maisha yenu na wakati mna kinga ya chanjo? eti, unahofu ipi bwana mbowe

Tuseme mara ngapi?

IMG_20210720_094159_438.jpg
 
Kutokuelewa kwako hakukufanyi wewe kuwa mwerevu na wengine kuwa wajinga kwa maoni yako tu.

No wonder babu Loliondo leo ana kikombe cha kutibu na kuzuia Corona na mamlaka zimeingiwa ganzi wasijue cha kufanya.

Yule babu mnyazi Mungu apishilie mbali ni muhimu kwa uhai wake apate chanjo, avae barakoa na awe mtumiaji mwaminifu wa vipikuzi haraka sana, vinginevyo atakuwa hatarini mno.

Ni bahati mbaya sana kuwa, kwa maslahi binafsi ya kisiasa, wanasiasa wameamua kuukumbatia ujinga wakiacha watu kufa mithili ya kuwatoa kafara.
Chanjwa ili usiambukizwe na wasiochanjwa, mbona unahasira kama siasa za Chadema bhana
 
Usiyasahau mahaba niue ya Corona kwa wanaume, wazee na hasa wenye magonjwa mengine bila ya kuwasau waliowahi kupata kikombe cha babu enzi hizo.

Au nasema uongo ndugu yangu?
Kuna magonjwa sugu ya miaka nenda rudi hayajaenda likizo ya kuua watu, nina babu zangu watano ktk mlela clan wamezaliwa mwaka 1928-1932 hawana habari na mibarakoa na wanapeta hadi Leo tangu ujio wa corona.
 
Haya mawazo yanatazamiwa yawe ktk kipindi cha miaka mingapi ijayo?

Je miaka kumi?

Kama ndivyo, basi haina maaana kabisa ya chanjo!

Unachanjwa na unaishi sawa tu wasiochanjwa kipindi cha miaka miiingi kiasi hiko, halafu bado unatazamia kuna watu wasio chanjwa watakufa, na wakati wewe mwenye chanjo ukiwa na hofu na chanjo yako ikiwa itakubakisha sawa kama ulivyokuwa kabla hujachanjwa ama la!!

Kama ni nia ni majadiliano ya hoja, basi shika kitu kimoja kimoja. Siyo kuruka ruka kama bisi kikaangoni.

Chagua tuanzie ipi?
 
Kama ni nia ni majadiliano ya hoja, basi shika kitu kimoja kimoja. Siyo kuruka ruka kama bisi kikaangoni.

Chagua tuanzie ipi?
Ujinga wa chanjo za korona, Unachanjwa halafu bado unakuwa na hifu ya kuambukizwa, Tofauti kabisa na chanjo zingine

Ni upotevu wa fedha za umma kuagiza chanjo hizi
 
Kuna magonjwa sugu ya miaka nenda rudi hayajaenda likizo ya kuua watu, nina babu zangu watano ktk mlela clan wamezaliwa mwaka 1928-1932 hawana habari na mibarakoa na wanapeta hadi Leo tangu ujio wa corona.

Kuna kinasaba kingine muhimu cha kuongezea pale kwenye ugonjwa huu:

"Hiki kirusi kina mahaba zaidi mijini, majiji, na hasa kunako mazingira ya safari na mikusanyiko ya watu."

Hiki si kirusi cha shamba kwa sasa. Japo tukizembea kitafika huko pia.

Bila shaka majibu ya mbio za mwenge na Nandy festival Mwanza umeyasikia. Bila shaka majibu ya miingiliano ya safari kati ya Moshi na Dar pia utakuwa umeyasikia. Huko ndiko nduguye Mbowe (rip) yaliko mfika.

Au kwa vile hawatoi takwimu ndiyo maana hujui wapi hiki kirusi kina tambaa?

Kumbuka kirusi hiki kimekuja kwa ndege.

Waliko wazee wako (mola awajalie maisha marefu) waache huko huko. Kwa kuwaleta mjini, unaweza kulazimika kumlaani mwendazake badala ya kumwacha akapumzika kwa amani.
 
Uganda na Rwanda hapana kuendekeza ujinga. Huko wala si ukuda bali utachezea kichapo!

Kumbuka ujinga si tusi. Ni suala la kutokuelewa tu. Ujinga dawa yake ni elimu dunia tu mkuu.

Huku kwetu tutabembelezana kwanza, ila baadaye kutakuwa na vikwazo hapa na pale. Mdogo mdogo tutafika tu.

Hiyo ndiyo sayansi ya chanjo.
Acha uongo mkuu! Rwanda na Uganda kote huko hakuna anayelazimishwa kuchanja isipokuwa vurnerable groups kama wafanyakazi sekta ya afya.

Hakuna nchi inayolazimisha chanjo, Indonesia ilitaka kulazimisha lakini sijui ilikuwaje hawajafanikisha. Kusema Mbowe anauchungu wa kufiwa na kaka yake na kuuguliwa na mtoto wake basi alazimishe ukoo wake wote na watu wake wa karibu (Ikiwemo wafuasi wake) ndiyo wachanjwe ili asifiwe tena kama anaamini hizo chanzo zinazuia vifo vya Corona. Hawezi kusema nchi nzima ichanjwe kisa kafiwa na kaka yake huo ni uzwazwa.
 
Ujinga wa chanjo za korona, Unachanjwa halafu bado unakuwa na hifu ya kuambukizwa, Tofauti kabisa na chanjo zingine

Ni upotevu wa fedha za umma kuagiza chanjo hizi

Na unathubutu kuuita "ujinga wa chanjo ya Corona" kwa werevu upi mkuu?

😂😂😂😂😂😂😂!

Kwa hali hizi nawaelewa jabisa akina Museveni na bwana Kagame. Wanaume wa shoka hawa.

Kwa hakika maendeleo hayawezi kuwasubiri wakaramojong au wamasai kuvaa suruali.

Kwamba hata ukichanjwa waweza ambukizwa?

IMG_20210718_063653_881.jpg

Ukishachanjwa hata ukiambukizwa tena hali inakuwa na unafuu mkubwa.
 
Kwa hiyo mbowe katumwa na upande wa pili kwa sababu upande wa pili unaona watu hawataki kuchanjwa? Anatumika kama kisemeo tu na upande wa pili. Mbowe ni mtu makini haya hayatoko moyoni bali yanatoka upande wa pili
Boooo! Boooo! Boooo!
 
Kama ukichanjwa huambukizwi, hofu yako ni ipi kwa wasiochanjwa?

Tuandike mara ngapi?

IMG_20210720_094159_438.jpg

Hiyo hofu unaisoma wapi?

Rudini shule. Elimu haina mwisho. Na elimu ni uhuru!
 
Tatizo sio chanjo tatizo ni hao waliotengeneza hiki kirusi kwa makusudi kabisa je wanalengo lipi na wanadamu???

Kama suala ni kifo mbona ni jambo la muda tu na kila mmoja atakionja!!

Ni kweli ugonjwa upo na unaua bahati nzuri ni kwamba kila kitu kimeshawekwa wazi juu ya madhumuni na lengo la hili gonjwa pamoja na chanjo yake

Hivyo kuanza kulazimishana chanjo ni upuuzi na kila mtu aishi maisha yake ilimradi hauvunji sheria na kanuni za nchi

Mkuu hii ni hatua sana kwamba unatambua:

"Ni kweli ugonjwa upo na unaua."

Ila sasa, kwamba?

".. bahati nzuri ni kwamba kila kitu kimeshawekwa wazi juu ya madhumuni na lengo la hili gonjwa pamoja na chanjo yake .."

Hahahaa haa 😂😂!

Nani ameyaweka wazi madhumuni hayo na ni yapi ikiwamo lengo la chanjo yake?

Mwongozo wako tafadhali.

😂😂😂😂😂😂

NB: Nimelazimika kucheka muda wote nikiandika haya kama mazuri vile.

Hiiiiii bagosha!

Hata hivyo nisiache kumalizia:

IMG_20210719_183108_460.jpg
 
View attachment 1860722
Labda unacheka kwa sababu unajua ila unajitoa ufahamu kwa maana kama wewe ni mtu wa kusoma nakala mbalimbali mtandaoni na nje ya mtandao unafahamu fika kwamba huu ni mchezo wa hatari ambao unachezwa na maisha ya watu ndio dhamana yake kuu

Soma mkuu
 
Back
Top Bottom