#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

#COVID19 Chanjo ni Lazima: Hoja ya Mbowe ina Mashiko

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:

"Chanjo ina maana kama tu idadi kubwa na ya kutosha katika jamii inakuwa imeipokea. Vinginevyo inakuwa haina maana."

Kiuhalisia chanjo ni kwa manufaa ya wanayoipokea. Serikali zina wajibu wa kuona watu wake wananufaika chanjo husika.

Kuweza kuwapata idadi kubwa kadri iwezekanavyo mbinu mbali mbali hutumika zikiwamo kutoa elimu, ushawishi na hata kutumia nguvu ikibidi.

Kwa wanaume wa shoka, pande za Rwanda na Uganda, huko hakuna cha lele mama au mswalia mtume. Huko kuchanjwa ni lazima na bakora kumhusu mtu anayeleta ujuaji wala si issue.

Kwingine uthibitisho wa chanjo huhitajika kabla ya kupata huduma kama vile usajili, usafiri, ruhusa nk kama kishawishi hutumika. Chanjo inakuwa hiari, lakini ni lazima kabla ya huduma husika.

Kwa jamii zilizostaarabika vilivyo na zenye kujitambua, huko chanjo ni vitu vinavyoeleweka.

Rejelea hali halisi ya kwetu ambapo tokea Apr 2020 hazipo takwimu mpya za Corona. Yaani tokea hapo hakuna mgonjwa wala aliyekufa kwa Corona isipokuwa kaka yake Mbowe.

Katika kipindi hicho pia watu wameaminishwa kuwa huu ugonjwa haupo. Bali Corona ni vita vya kiuchumi na chanjo hizi ni sehemu tu katika kuwaangamiza wao.

Hiiiiii bagosha!

Waliowaaminisha hivyo ni Rais wa nchi akishirikiana na wizara yenye dhamana na afya za watu. Katika walioaminishwa hivyo, wengi wao ni "the ignorant mass" vijijini; wakiwamo sungu sungu, wapiga debe, machinga, vibaka vibaka na wa namna hiyo.

Una ibadili vipi mitizamo ya watu kama hao, huku watu wakiendelea kufa?

Ikumbukwe kuwa hadi sasa serikali yetu haitoi takwimu zozote na hayupo ajuaye hali ni njema au mbaya kiasi gani.

Kwa hakika mwenye kujua faida za chanjo na kuthamimi maisha ya watu hatachelea kutumia nguvu kuwataka watu kuchanjwa ambayo aghalabu ni kwa faida yao.

Ama kwa hakika itakuwa jambo la kushangaza kwa serikali yoyote, kama itakaa kimya iache watu kufa iwapo matumizi ya nguvu tu yangali nusuru maisha dhidi ya ujinga wao.

Viva Museveni na viva Kagame kwa kuyajali maisha ya watu wenu vilivyo kiasi cha kutumia nguvu stahiki inapobidi katika kuwanusuru.

Kwa hakika waja nyie mnayo thwawabu kubwa huko mbinguni, Inshallah!
 
Chanjo haipaswi kua shuruti kwa wananchi, inapaswa kua ya hiari na si vinginevyo. Mpaka sasa kunaviashiria vyote vinavyotia shaka chanjo biashara za UVIKO-19 kuanzia hatua za uzalishaji wake na usambazaji wake duniani.

Tafiti bado zinahitajika sana kung'amua kitendawili cha huu ugonjwa vinginevyo, tutarajie madhara makubwa kiafya siku za usoni kwa maamuzi yasiyo na mustakabali kwa taifa. Mfano rejea matokeo ya historia chanjo za awali za Polio na uhusiano wake na UKIMWI.
 
Kwa hiyo mbowe katumwa na upande wa pili kwa sababu upande wa pili unaona watu hawataki kuchanjwa?

Hapana. Mbowe alichofanya ni kutoa rai yake kama mtu aliyeuguliwa na mtu wake wa karibu na akafariki.

Kifo ambacho kingeweza kuepukika kwa chanjo tu.

Ni ubinafsi uliopitiliza ukijua na bado ukakaa kimya ati kwa kuwa kujaribu kuwaepusha wengine, hakukuhusu.

Kumshutumu Mbowe out of ignorance ni kutojitendea haki wenyewe.
 
Mbowe yupo sahihi ila kwa Tanzania iliyojaa vilaza ataonekana kituko.

Watu wamedanganywa chanjo ni vita ya kiuchumi hivyo wazungu wanataka kutuangamiza.

Makanisani kina Gwajima wanasema chanjo ni alama ya mpinga Kristo 666 hivyo huu ni ujio wa NEW WORLD ORDER.
 
Chanjo haipaswi kua shuruti kwa wananchi, inapaswa kua ya hiari na si vinginevyo. Mpaka sasa kunaviashiria vyote vinavyotia shaka chanjo biashara za UVIKO-19 kuanzia hatua za uzalishaji wake na usambazaji wake duniani.

Tafiti bado zinahitajika sana kung'amua kitendawili cha huu ugonjwa vinginevyo, tutarajie madhara makubwa kiafya siku za usoni kwa maamuzi yasiyo na mustakabali kwa taifa. Mfano rejea matokeo ya historia chanjo za awali za Polio na uhusiano wake na UKIMWI.

Umesoma mada au ume-comment tu?

Kwingine ulazima hauko kwenye kulazimishana kwenda kuchanjwa. Ila ulazima utakuja hivi:

1. Kusafiri onyesha proof ya chanjo
2. Kusajiliwa mahali onyesha proof ya chanjo
3. Kuingia hapa onyesha proof ya chanjo
4. Nk nk.

Hapo ndipo mzizi wa fitna ulipo.

Utajikuta mwenyewe kwenye fix tu, kama kwenye barakoa ambazo pia ni hiari.
 
Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote, nina lazimika kutia neno juu ya maneno ya hekima yake Mwamba Aboubakar Laigwanan Mbowe (Mola amjalie maisha marefu).

Uhalisia kuhusiana na chanjo yoyote ni huu hapa:
Admin unganisheni huu Uzi na Uzi mama

Hakuna sababu ya multiple threads
 
Umesoma mada au umeongezeka comment tu?

Kwingine ulazima hauko kwenye kulazimishana kwenda kuchanjwa. Ila ulazima utakuja hivi:

1. Kusafiri onyesha proof ya chanjo
2. Kusajiliwa mahali onyesha proof ya chanjo
3. Kuingia hapa onyesha proof ya chanjo
4. Nk nk.

Hapo ndipo mzizi wa fitna ulipo.

Utajikuta mwenyewe kwenye fix tu, kama kwenye barakoa ambazo pia ni hiari.
Sawa Mdau! Basi wahi ukachanjwe chanjo unao uhuru wa kufanya hivyo.
 
Mbowe yupo sahihi ila kwa Tanzania iliyojaa vilaza ataonekana kituko.

Watu wamedanganywa chanjo ni vita ya kiuchumi hivyo wazungu wanataka kutuangamiza.

Makanisani kina Gwajima wanasema chanjo ni alama ya mpinga Kristo 666 hivyo huu ni ujio wa NEW WORLD ORDER.
Kwani NEW WORLD ORDER ni nini?
 
Sawa Mdau! Basi wahi ukachanjwe chanjo unao uhuru wa kufanya hivyo.

Kama nilivyoandika mwanzo kwenye mada na kwa uthabiti kabisa:

"Kama mwuungwana tokea pande za Pwani niliyeukataa ukanjanja katika nyanja zote."

Nitakuwapo kuchanjwa day 1.

Ila chanjo iwe kutoka kwa beberu.
 
Acheni ukuda wenu.
Mimi nikifa wewe unaumia nini? Lazima lazima ndio sitakufa au?

Acheni mambo ya ajabu bana. Hata wakisema leo lazima, sichanji ni bora waniue kuliko kuchanja.

Et unachanja kisa li ugonjwa la kutunga. Ujinga bana. Nikichanja then what? Sitaumwa? Sitakufa? I fear nothing to die when right time comes..
 
Back
Top Bottom