Suala la chanjo ya corona sio la kukurupuka. Kwa maoni yangu linahitaji muda wa kutosha kujielimisha na kujiridhisha ndipo mtu aamue kuchanjwa au kusubiri zaidi...
Uamuzi wao sii ,uamuzi huru ila wakusikia kwa wengine au wakushawishiwa, kwa kuwa kaongea fulani asiye amini katika ugonjwa husika na hata chanjo yake. Hapa ndio pakuwaambia akili za kuambiwa wachanganyie na zakwao.
 
Japo siko kwenye hiyo Ligi ya mkubali chanjo au mkataa chanjo ila wakati mnatoa hoja jaribu uwe na uhakika. Huko marekani unakosema wanagomea chanjo, je wafaham zaidi ya Asilimia 50 mpaka sasa wamechanja?...
Udogo wa elimu ni kwa wasiotaka kuchanjwa tu au hata hao wanaochanjwa pia?
 
Msingi wa wanaoikataa ni kwamba hii inaitwa ya majaribio na madhara yake hayajulikani hapo baadae
 
Kuna nchi zishachanja asilimia 80 ya watu wake, hao wasiojielewa watatengwa. Sisi watanzania tunakataa kwa kufuata mkumbo wa mfu.
 
Kuna nchi zishachanja asilimia 80 ya watu wake, hao wasiojielewa watatengwa. Sisi watanzania tunakataa kwa kufuata mkumbo wa mfu.
Hao waliyochanja hivyo sio kwa sababu watu hawajagomea bali ni uwezo waliyonao, huku afrika hata wote tukitaka kuchanja bado hatuna uwezo wa kupata hizo chanjo na kuchanja kwa asilimia hiyo.
 
Nataka kuuliza hivi hapa kwetu Tanzania wanakupa chanjo bila kupima au wanakupima kwanza ndio wanakuchanja? Na kama hawatupimi kwann wanatupa chanjo wakati wakijua hathari ya kufanya hivyo, je kama mtu ana corona alafu akapewa chanjo kweli hakuna madhara?
 
Japo siko kwenye hiyo Ligi ya mkubali chanjo au mkataa chanjo ila wakati mnatoa hoja jaribu uwe na uhakika. Huko marekani unakosema wanagomea chanjo, je wafaham zaidi ya Asilimia 50 mpaka sasa wamechanja?...
ko unaamin dini ni utumwa sio?
 
Udogo wa elimu ni kwa wasiotaka kuchanjwa tu au hata hao wanaochanjwa pia?
Udogo wa Elimu ni pale unapolinganisha vitu viwili visivyotakiwa kulinganishwa. Tanzania katika suala la chanjo, labda ulinganishe na Burundi na Haiti, ja siyo na Marekani au nchi yoyote ya Ulaya.

Nchi za America na Ulaya, hakuna nchi ambayo waliochanjwa ni chinibya 50%.
 
Sasa hoja ni ipi ni uwezo wa hizo nchi au kipi? maana wao wana uwezo na ndio wenye hizo chanjo wamejilimbikizia huko sasa ulizani tutakuwa sawa? hata hivyo bado watu wengi hawajachanjwa pamoja na kuwa na chanjo za kutosha na kuanza hilo kwa muda mrefu ndio maana bado wanaangaika na maambukizi.
 
Hao waliyochanja hivyo sio kwa sababu watu hawajagomea bali ni uwezo waliyonao, huku afrika hata wote tukitaka kuchanja bado hatuna uwezo wa kupata hizo chanjo na kuchanja kwa asilimia hiyo.
Unataka kusema Tanzania tukipata dose kwa ajili ya watu wote tutachanja? Kwa mentality tuliyonayo?
 
Wabongo ni wavivu sana kusoma na kun'gamua mambo magumu wao ni kupinga tu na kuishi kwa mazoea
Kupinga sio ujinga ni mwanzo wa kutaka kujua/kuelewa! Lipi bora ukubali ili upate ufafanuzi au upinge ili upate ufafanuzi uelewe?
 
Nimeona kuna orodha ya kutosha ya chanjo tofauti kwenye nchi mbalimbali tofauti na hii inayotolewa hapa kwetu, mwenye uelewa mpana naomba clarification ya tofauti hiyo na chanjo ipi ni bora kuliko nyingine?
 
Unataka kusema Tanzania tukipata dose kwa ajili ya watu wote tutachanja? Kwa mentality tuliyonayo?
Nimezungumzia suala la uwezo ambalo ni moja ya changamoto zetu afrika katika hili zoezi la chanjo ukiacha hiyo mentality, ndio maana nikasema hata kama wote watanzania tutakubali kuchanjwa ila haitowezekana kutokana na uwezo hivyo sikuwa na maana kwamba tukipewa chanjo za watanzania wote basi tutaweza kuwachanja wote, issue ya mentality hata huko kwa wenzetu ipo ndio maana Marekani sasa hivi anagawa hela kwa atakaye kubali kuchanjwa.
 
Tumalize doses tulizonazo ndo tutaanza kuongea kuhusu kuongeza, na Marekani hagawi hela bali ni bahati nasibu ambayo hata bongo twaweza fuata kuongeza motisha.
 
Maoni yangu mkianza kuchanja basi bora mchanje wote.

Maana watakawo chanja ndio watakawo leta Variant na kuwa ambukiza waso chanja.
Tanzani chanjo iloletwa ni kwa watu millioni 1 na hadi sasa wamechanja 105000. Angalau tupate chanjo za watu 30 millioni
 
Kuna vitu vinashangaza sana Tanzania ni kama watu hawataki mtu awe na mtazamo tofauti na wao au wakubwa zao. Inashangaza kuona Selikari imesema chanjo ni hiari ya mtu ama achanje ama akatae kuchanjwa.

Wapo watu waliosema hadharani kwamba wao wamechanjwa hata kabla Selikari haijaingiza chanjo nchini hakuna aliyewahukumu.

Chanjo zimeingia viongozi wamechanjwa mbele ya kamera wengine wanaendelea kuchanjwa na kampeni za kuhamisisha watu inaendelea nchi nzima ni vizuri sana sasa tatizo linakuja mtu anaposema hadharani mimi sitochanjwa kama alivyosema Mh Polepole watu wamemjia juu kwanini aweke msimamo wake hadharani. Kwani hao wanaochanjwa si wanaweka misimamo yao hadharani mbona hawaulizwi?

Kama chanjo ni hiari basi tukubali kampeni za pande zote mbili wanaotaka kuchanjwa na wasiotaka kuchanjwa kisha muda na Mungu waamue asiwepo mtu akajiona anachoamini yeye ni bora zaidi kuliko cha wenzie.




Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…