Chapati ya Kichina, mmea unaoishi kwenye maji, Kombucha/tea mushroom

Weka hata picha basi nasi tulijue sio maneno mengi tu
 
Tuwekeeni picha basi ili na sisi tuufaidi hata kwa macho tu.

Mmmh! Mkuu, bahati mbaya sikubahatika kuupiga picha wakati bado niko nao!

Pia miaka hiyo simu hazija eneo sana, kama zilikuwepo basi kwa watu wachache sana, nakumbuka simu yangu ya kwanza kumiliki nilikuwa SIEMENS C 25 kubwa kama kipande cha Sabuni enzi hizo tunaziita "MSHINDI" (aina ya sabuni) tena nilikuwa hazina camera! Miaka ya mwanzoni mwa 2000! Kabla ya kumilika NOKIA enzi hizo tunaziita "JENEZA" aha aha haaa! Hatari sana mkuu!

Ingekuwa ninalo sasa mbona tayari picha muda mrefu tu!
 
Weka hata picha basi nasi tulijue sio maneno mengi tu

Picha sina mkuu, ni miaka mingi imepita!

Ningekuwa nayo mbona tayari ningeshaiweka mkuu! Wanasema kuona nikiamini!
Lakini kwa shuhuda za watu hapa nadhani umepata picha japo kidogo. Kama kuna mtu bado analo au hata picha yake basi atusaidie kuiweka itapendeza zaidi.
 
Hii kitu alikuja nayo shangazi kama sio dingi kutoka mkoani mbeya.

Huu mmea hata Tanzania tunao sababu tuna utajiri wa species nyingi sana za mimea.

Ngoja nikutafutie jina na ukipatikana nitashare na ninyi hapa jina na ikibidi tugawane mbegu ni mzuri sana ile kitu tulikuwa tunaigida sana juice yake.

Tuliweka kwenye zaidi ya vyomba sita tukilina maji yake. Alikuja kuharibu bi mkubwa alipookoka akaambiwa na pastor wake kuwa kile kitu ni mapepo na ni maagano ya mizimu. Yule pastor choko sana hadi leo namind kichizi nikimuona natamani nimlabue makofi na mitama maaana ndie alimchanganya bi mkubwa akaona ule m'mea una uhausiano na maswala ya giza na kumbe ni ukosefu tu wa elimu ya mimea na tiba asili.

Bi mkubwa aliyamwaga yale masufuria yote kimya kimya ndo hadi leo sijuagi pa kuupata.
 
Ungekuwa unashare na wengine now usingepata shida ya kupata mbegu.
 
Kabisa inasikitisha sana. Lishe tiba ni kitu muhimu sana.
 
Yaan huo mmea nautafuta kwa gharama yoyote, nakumbuka miaka ya 90 mzee alikuwa anatuletea, unatoa juice juice moja nzuri sana ambayo ni dawa na kinga ya maradhi mbali mbali, ni vizuri ukiwa nao ndani na kuizoesha familia kutumia juice yake badala ya kutumia juice za viwandani.
 
Daa zamani sana huo mmea niliuona. Kuna jamaa alikuwa nao kama sikosei alikuwa anauita "mybao/mibao/maibao". Si na hakika na matamshi ya hilo jina ila mnaweza kuanzia hapo. Enzi hizo kila tukimuona jamaa ametoka kazini akiingia tu kwake kabla hajakaa tumeshafika na vikombe vyetu vya plastiki kujimiminia ilikuwa kama chai ya rangi hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…