Charles Hilary ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu - Zanzibar

Charles Hilary ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu - Zanzibar

Charkes Hilary ni mtu wa Malinyi mkoa wa Morogoro Zanzibar aliishi wakati baba yake akiwa Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
Inawezeka nina rafiki zangu baba yao pia alikuwa polisi na wao walikuwa wanakaa morogoro. Walikuwa wanafanya biashara ya kuchukua nguo zanzibar na kuleta huku, kuna kipindi walienda wakati wa mfungo na wao ni wakiristo hotel zote zilikuwa zimefungwa baada ya kuzunguka bila mafanikio ndio wakakumbuka kina charles walikuwa wanaishi huko ndio wakaenda kula na biashara ikaishia hapo
 
Wakuu Kuna Mabadiliko Ya Nafasi kule Ikulu Zanzibar.

Charles Hilary ameteuliwa na Rais Mwinyi Kuwa DG mpya Wa Mawasiliano ya Rais Ikulu Zanzibar..

Kulikoni Wa Kwetu Huyu Van Mohammed Tena Kuliwa Kichwa?View attachment 2063000

Sent using Jamii Forums mobile app
Duu tutaimiss sana couple yake na Ivona Kamuntu!
Kila lakheri Charles Hilary! Pole pia kwa Kamuntu!
 
Achaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu ZanzibarView attachment 2063046
Hongera zake sana kwa teuzi hii ambayo ni moja ya nafasi nyeti sana. Huyu ni mwandishi wa habari mmbobezi aliyedumu katika uandishi wa habari na utangazaji. Alikuwa kivutio kikubwa sana RTD katika utangazaji wake wa mpira kwa uwezo mkubwa wa kushika majina na kuyatamka ya wachezaji na namna ya kipekee kufanya hata kama haupo uwanjani unajiona kama upo.

Charles alizidi kupanda mpaka BBC kuweza kumkubali na kufanya kazi BBC na ilizidi mjengea CV yake na ndipo Azam nao waliweza kumchukua kwa kujua uwezo na kipaji chake.

Na uhakika vigezo vichache nilivyoweza vitaja vimefanya Mh Raisi Mwinyi kumteua na nina imani kwa nafasi hiyo ataiweza na ni teuzi sahihi kabisa.

Katika teuzi tuipende sana jadili dini ya mtu kwani nafasi za serikali ni kwa ajili ya kutumikia wananchi na siyo imani za watu.

Hongera sana kwake Charles mzee wa nani zaidi enzi hizo Redio One kipindi kilichokuwa bora ,
 
Huyo mwamba miaka ya 2011 nikiwa kachalii nilikua namsikiliza akitangaza mpira wa Epl kwa radio enzi akiwa BBC ilikua inanoga sana kuliko kuangalia live timu ilikua ikisawazisha utaskia "Moja Moja" Sasa jinsi anavyoisema kwa mbwembwe Hadi Wana wakawa wanamuita mzee wa Moja Moja
 
Charkes Hilary ni mtu wa Malinyi mkoa wa Morogoro Zanzibar aliishi wakati baba yake akiwa Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar.
Ww na yy mwenyw nani anajifahamu zaid? mana mwenyw anasema kazaliwa Zanzibar kaondoka Zanzibar akiwa na miaka 9
 
Upo sahihi kabisa, wanaosema Charles Hilary ni Mzanzibari ni vijana tu wa kwenye huu mtandao ambao kila mmoja anataka ajifanye anajua. Majina yake kamili ni Charles Martin Hilary Mkwanga. Sekondari alisoma Kinondoni Muslim na kumaliza kidato cha nne 1979 na kujiunga RTD 1982. Zilizofuata ni kozi mbalimbali za utangazaji na uzoefu wa kazi. Kazi walianza mwaka mmoja na Betty Mkwassa wakati huo akiitwa Betty Chalamila. Kwa hiyo ukweli ni kuwa Bwn Charles Hilary ni Mpogoro ( kabila dogo la Kindamba), hana uhusiano na Uzanzibari hata kidogo na wala lafudhi yake ya kuongea siyo ya Kizanzibari,.
Nenda kaangalie Nyundo ya Baruan Muhunza, mwenyew anasema kazaliwa Zanzibar, ww na yy nani anajifaham zaid?
 
Mada imejaa upotofu na majuha
Humjui mtu unapiga kimya.
Hawa wanaosema jamaa mzenji, ndio hawahawa waliokua miaka nenda rudi wanadhani Mwinyi ni mzenji pia. Kuishi sehemu tofauti na origin ya baba yako hakufuti asili ya mtu nyie watoto wa juzi mliojazana humu JF.
huyu kwa mujibu wa yy mwenyw si wa kuhamia, kazaliwa Zanzibar, baba yake ndo alihamia kikazi
 
Huyu ni kama alivyokuwa Jaji Agostino Ramadhani.
Ni miongoni mwa wazazimbari wachache ambao ni wakristo. Wakkristo Zanzibar ni wengi tu hasa wa madhehebu ya Katoliki, Anglican na haya ya kiroho
Ww jamaa ni Muongo na wala hujui chochote kuhusu Charles Hillary nyie ndo wale mnatusumbua vijiweni kila kitu mnajifanya mnajua kumbe fiksi
 
Huyo nasikia ni mzaliwa wa Jang'ombe sema huu ukafir kautoa wapi au ndio aliweka jina la bosheni lakini ni mandevu?
Charles Hilary ni Mzanzibari mzawa, ambapo kwenye ukoo wao kuna mchanganyiko wa Waislam na Wakristo.
Hii pia naomba waelewe wale wote wanaohisi labda Zanzibar hakuna Wakristo wazawa, wapo tena wala huwezi kuwajua na pia ni wazanzibari safi na wanajichanganya na waislam waliopo Zanzibar na wala hawana mambo ya kijinga kama wengine wanaohamia.
 
Ww jamaa ni Muongo na wala hujui chochote kuhusu Charles Hillary nyie ndo wale mnatusumbua vijiweni kila kitu mnajifanya mnajua kumbe fiksi
Sasa unamkatalia nini mwenzako kuelezea mawazo yake? Unajua historia ya Kanisa la Mkunazini na lile jingine la Mbweni? Zenji kuna makanisa ni ya Zamani sana kushinda mengi yaliyopo bara.
 
Back
Top Bottom