1. Charles Kimei kama Mtanzania yeyote ana haki ya kikatiba ya kujiunga na chama chochote cha siasa, au kutojiunga,ana haki ya kuchagua kiongozi anayemtaka, au kuomba kuchaguliwa.
2. Charles Kimei kwangu mimi hakuwa na integrity yoyote ya maana. Alisema anamuogopa Magufuli sana na atafanya chochote Magufuli atakachosema.
Kauli hii kutoka kwa mtu mume inawekea shaka utu wake na uanaume wake. Kutoka kwa CEO wa Benki, inatilia shaka integrity ya benki hiyo.
Maana ni kama alisema kwamba Magufuli angetaka kuiba hela za CRDB aende kuzitumia kwenye uchaguzi, Kimei angekubali tu.
Hivyo sioni Kimei atapoteza integrity gani, wakati alikuwa hana integrity tangu mwanzo.