JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mwanasiasa ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga amezungumza mambo mengi katika mahojiano maalum na Dar24 na kufunguka mambo mengi ikiwemo sakata lake la kuvuliwa Uwaziri kwa kile kilichoelezwa aliingia Bungeni akiwa amelewa.
KITWAGA: NILILOGWA, NITATENGENEZEWA ZENGWE NIKAPONA KIMIUJIZA
Mwanasiasa Charles Kitwanga amesema huwa anacheka akikumbuka stori ya kuvuliwa nafasi ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani mwaka 2016 kwa madai alilewa kwa kuwa siku ya tukio alikuwa anaumwa na alikunywa dawa.
Amesema hayo ni mambo hutokea katika Siasa ambapo pia unaweza kutengenezewa zengwe, skendo, kulongwa au kutafutwa ili umalizwe, ambapo yeye yote yalimkuta.
Kuhusu kurogwa anasema “Nilipata kiharusi, nikalazwa Muhimbili nikaenda kupona India, nadhani nilipona kimiujiza kwa kuwa namuamini Mungu.”
Kuhusu kuvuliwa Uwaziri amesema “Huwa inaniumiza nikikumbuka, kwani nilijua, ninajua na wenyewe wanajua walichofanya.”
KITWANGA: NILIWEKEWA ULINZI NA KUFUATILIWA KILA HATUA
Charles Kitwanga amedai wakati akiwania Ubunge 2020 alikuwa akifuatiliwa na anaoamini ni walinzi, karibu na nyumbani kwake ambapo walimfuatilia kila anakokwenda.
Amesema “Kulikuwa na magari matatu kwa siku 10, ndani ya magari hayo kulikuwa na vijana wa PCCB, Usalama wa Taifa na Askari, ni kama ilikuwa mashindano ya Kitwanga na Serikali.”
Kuhusu ukaribu wake na hayari John Magufuli anasema “Alikuwa rafiki yangu lakini tangu alipokuwa Rais hatukuwahi kukutana wawili zaidi ya kukutana katika shughuli za kikazi, sikuwahi kufika nyumbani wala ofisini kwake, huwa sijikombi na sitafanya hivyo.”