Charles Kitwanga: Sikutaka kujikomba, nililogwa nikapona kimiujiza, nilikuwa na vita na Serikali

Charles Kitwanga: Sikutaka kujikomba, nililogwa nikapona kimiujiza, nilikuwa na vita na Serikali

Tuna deal na mzazi, mwacheni mtoto!
Mkuu mi namjua huyo mtoto wake....najaribu kuvuta picha kutoka kwa mtoto kwenda kwa baba

Remember mtoto ana 50% ya DNA ya baba,alichonacho mtoto baba anaweza kua nacho mara mbili zaidi

Mtoto alikua na nyodo mzee acha kabisa....na nikicheck huyu jamaa anavyoongea kwenye hii interview,anavyongea kwa mafumbo katika kumdharau Magufuli,directly atakua na nyodo,tena yeye anaweza kua hata worse than mtoto wake.

Another comparison ni akili...huyo binti alikua na akili kama sikosei alikua top student walipokua first year,nadhani UDSM engineering hapakumfaa tena,ghafla next year haonekani,uvumi ukapita alienda mbele South Africa....

Sasa kama mtoto alikua na akili nyingi hivyo,my estimation ni kwamba baba atakua mara mbili ya huyo binti....

Na my estimation ni nearly correct sababu kwenye hii interview jamaa mwenyewe anasema alisoma computing UDSM ambapo ni course ya top students plus kaenda Essex UK,which means huyu jamaa alikua na akili kwenye top 1% percentile!With this interview my theories are just clear and proven!

Sijasema namtwika mtoto vitendo vya baba yake,maana ni watu wawili tofauti...

Najaribu kufanya comparison mzazi na mtoto wake
 
Nimemsikiliza jamaa na ni wazi anaamini sana mambo ya ushirikina. Hata ya India anaamini ilisababishwa na mkono wa mtu. Ni aibu sana.

Amandla...
Kwanini iwe aibu kwani wewe huamini kama kuna uchawi duniani?!
 
Mwanasiasa ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga amezungumza mambo mengi katika mahojiano maalum na Dar24 na kufunguka mambo mengi ikiwemo sakata lake la kuvuliwa Uwaziri kwa kile kilichoelezwa aliingia Bungeni akiwa amelewa.

KITWAGA: NILILOGWA, NITATENGENEZEWA ZENGWE NIKAPONA KIMIUJIZA
Mwanasiasa Charles Kitwanga amesema huwa anacheka akikumbuka stori ya kuvuliwa nafasi ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani mwaka 2016 kwa madai alilewa kwa kuwa siku ya tukio alikuwa anaumwa na alikunywa dawa.

Amesema hayo ni mambo hutokea katika Siasa ambapo pia unaweza kutengenezewa zengwe, skendo, kulongwa au kutafutwa ili umalizwe, ambapo yeye yote yalimkuta.

Kuhusu kurogwa anasema “Nilipata kiharusi, nikalazwa Muhimbili nikaenda kupona India, nadhani nilipona kimiujiza kwa kuwa namuamini Mungu.”

Kuhusu kuvuliwa Uwaziri amesema “Huwa inaniumiza nikikumbuka, kwani nilijua, ninajua na wenyewe wanajua walichofanya.”

KITWANGA: NILIWEKEWA ULINZI NA KUFUATILIWA KILA HATUA
Charles Kitwanga amedai wakati akiwania Ubunge 2020 alikuwa akifuatiliwa na anaoamini ni walinzi, karibu na nyumbani kwake ambapo walimfuatilia kila anakokwenda.

Amesema “Kulikuwa na magari matatu kwa siku 10, ndani ya magari hayo kulikuwa na vijana wa PCCB, Usalama wa Taifa na Askari, ni kama ilikuwa mashindano ya Kitwanga na Serikali.”

Kuhusu ukaribu wake na hayari John Magufuli anasema “Alikuwa rafiki yangu lakini tangu alipokuwa Rais hatukuwahi kukutana wawili zaidi ya kukutana katika shughuli za kikazi, sikuwahi kufika nyumbani wala ofisini kwake, huwa sijikombi na sitafanya hivyo.”

Ili ufanye Kazi na Jiwe unatakiwa kuhamishia akili matakoni ndio maana unaona prof mzima anasema alitolewa jalalani mara mwingine aseme baada ya Mungu anayefuata nai Rais Kwa muktadha ule ni Jiwe nk nk..

Jiwe kiukweli hapana tulipigwa na kuonja radha ya stori za madikteta kama Idd Amini n.k..
 
Sawa mkuu. Nakumbuka miaka ya nyuma ile kampuni yako ya INFOSYS ilitoa ajira kwa vijana wengi sana, pia ulipiga tenda kubwa kubwa kwenye taasisi nyeti za serikali ikiwemo BOT.
Stupid company sustaining itself from government and politicians mercy....

Inayofanya kazi za uchuuzi wa vifaa vya IT,kwanza sio vifaa vya IT,mostly wanaichuuzia serikali computer za desktop na laptop na antivirus,thats it,nothing else!

Thats stupidity,a business a class 7 lever can do with easy...

It is now a defunct company,sababu it was made on by politicians ili tu wajigawie hizo kazi za serikalini wao wenyewe politicians....

Government connections zimekufa na kampuni ni kama imekufa wote wana njaa plus Kitwanga mwenyewe anaongea unaona kabisa kachacha...

We thought they can make a self sustanable company ,self operating,sustained by superior and creative solutions offerings to the market as a market independent from any government influence and not huruma ya government officials sababu unajuana na "mawaziri" fulani serikalini

These are not real businessmen,these are workers and politicians who happen to open a company like Infosys kufanya kazi za serikali sababu tu anataka kuzifanya hizo yeye kama yeye apate ugali,thats why the company has scrumbled down when Magufuli blocked them out

These are pretenders,ndio maana wamejikita kwenye kazi generic kama kuuza laptop and blah blah which anyone can do,thats why mtikisiko kidogo tu they are on their butts now

Ndio maana makampuni yote wanayofungua wanasiasa ni ya kijinga,anapokosa uwaziri na yenyewe yanakufa,just like this.....They are not businessmen...

Makampuni yanayotegemea huruma ya Putin,ambae akikata bomba la gesi yanafia hapo hapo...these are not real companies...these companies are extensions of vyeo vya hawa politicians kama Kitwanga,akifukuzwa na zenyewe zinafia hapo hapo
 
Allies wa yule nduli wanaanza kujitokeza sasa kusema maovu yote mpaka waliokuwa katika kikosi kazi cha ku excute watu watajitokeza pia kutoa confesion zao
 
Nadhani hakuna sehemu rahisi kuwa kiongozi kama Tanzania....haikuhitaji kuumiza kichwa kwa mikakati na sera endelevu bali unatakiwa tu kuwa na uwezo mkubwa wa kusoma alama za nyakati na kufuata uelekeo wa upepo.......

Uwe na uwezo wa kuyapangilia maneno yatayoendana na mihemko ya wananchi kwa wakati huo au kumponda yule ambaye anaonekana kuwa anachukiwa na wengi......ukiviweza hivyo wewe utakuwa mtawala mpaka vijukuu vyako.....

Tanzania weledi ni kitu Cha mwisho kwa watawala....mtu yeyote anaweza kuongea lolote linalowafurahisha na watu wakalipokea na kuliamini kama lilivyo......

Wanasiasa wetu wamewahi kujitambua hili mapema na ndio maana wanaishi maisha ya peponi ilihali bado wapo duniani....ukijifanya kudadavua na kuleta weledi wanakucheka na kukuonjesha asali......

Ndio maana tuna wanasiasa au chama kipo madarakani kwa karibia miaka 50 kwa kuhubiri kutatua kero zile zile na bado watu wanawashangilia.......

Ndio maana Leo mtawala anatembelea VX la milioni 90 kwenda kuzindua mradi wa maji ya kisima Cha Cha Milioni mbili huku ameshika chupa ya maji safi MKONONI.........
 
Ila jiwe licha ya mazuri yake,yule jamaa haiwezekani kumpaka rangi, kama hadi kitwanga Rafiki yake amesema hivi basi baadhi ya mambo hasingiziwi
nilidhani ungempa jiwe credit kwa kumng'oa cheo swahiba wake.... kitu cha nadra sana Afrika

of course Kitwanga has an axe to grind kwa kunyolewa uwaziri, lazima amzodoe JPM, lakini dhamira yake inamsuta, anashindwa hata kumtaja JPM...

na anakiri kwamba ni kweli he was under the influence.... hakuwa na akili timamu jioni ile bungeni....

Kwamba ni pombe ya ulanzi, au madawa ya hospitali, au madawa ya kulevya, sisi hatungeweza kubaini. For all we cared, Waziri alisimama bungeni akiwa mentally impaired, President was livid, sacked his arse out of cabinet, didn't give a hoot about their lifelong friendship, a first in the history of Africa... Thumbs up to Pombe Magufuli
 
This is typical Sukuma man!. Hatujikombi!.
Big up sana kwa Charles Kitwanga.
P
Basi wewe si Msukuma... Wewe ulianza kujikomba kwa Magufuli akaku ignore sasa umekazana sana kwa Samia. Nadhani naona bado hajaamua.... Wewe ni Mzaramo, Mmatumbi,Mndengereko au Mtu wa Msoga.

Watu wa Nyanda ya juu Kusini,Kanda ya Ziwa ni watu ambao husimamia wanachoamini most of them.
 
nilidhani ungempa jiwe credit kwa kumng'oa cheo swahiba wake.... kitu cha nadra sana Afrika

of course Kitwanga has an axe to grind kwa kunyolewa uwaziri, lazima amzodoe JPM, lakini dhamira yake inamsuta, anashindwa hata kumtaja JPM...

na anakiri kwamba ni kweli he was under the influence.... hakuwa na akili timamu jioni ile bungeni....

Kwamba ni pombe ya ulanzi, au madawa ya hospitali, au madawa ya kulevya, sisi hatungeweza kubaini. For all we cared, Waziri alisimama bungeni akiwa mentally impaired, President was livid, sacked his arse out of cabinet, didn't give a hoot about their lifelong friendship, a first in the history of Africa... Thumbs up to Pombe Magufuli

watu hutumia akili kufikiri wengine matako.

mtu mlevi anayelewa mpaka bungeni mpuuzi anataka abebwe!!!!!
 
Mwanasiasa ambaye amewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, Charles Kitwanga amezungumza mambo mengi katika mahojiano maalum na Dar24 na kufunguka mambo mengi ikiwemo sakata lake la kuvuliwa Uwaziri kwa kile kilichoelezwa aliingia Bungeni akiwa amelewa.

KITWAGA: NILILOGWA, NITATENGENEZEWA ZENGWE NIKAPONA KIMIUJIZA
Mwanasiasa Charles Kitwanga amesema huwa anacheka akikumbuka stori ya kuvuliwa nafasi ya Uwaziri wa Mambo ya Ndani mwaka 2016 kwa madai alilewa kwa kuwa siku ya tukio alikuwa anaumwa na alikunywa dawa.

Amesema hayo ni mambo hutokea katika Siasa ambapo pia unaweza kutengenezewa zengwe, skendo, kulongwa au kutafutwa ili umalizwe, ambapo yeye yote yalimkuta.

Kuhusu kurogwa anasema “Nilipata kiharusi, nikalazwa Muhimbili nikaenda kupona India, nadhani nilipona kimiujiza kwa kuwa namuamini Mungu.”

Kuhusu kuvuliwa Uwaziri amesema “Huwa inaniumiza nikikumbuka, kwani nilijua, ninajua na wenyewe wanajua walichofanya.”

KITWANGA: NILIWEKEWA ULINZI NA KUFUATILIWA KILA HATUA
Charles Kitwanga amedai wakati akiwania Ubunge 2020 alikuwa akifuatiliwa na anaoamini ni walinzi, karibu na nyumbani kwake ambapo walimfuatilia kila anakokwenda.

Amesema “Kulikuwa na magari matatu kwa siku 10, ndani ya magari hayo kulikuwa na vijana wa PCCB, Usalama wa Taifa na Askari, ni kama ilikuwa mashindano ya Kitwanga na Serikali.”

Kuhusu ukaribu wake na hayari John Magufuli anasema “Alikuwa rafiki yangu lakini tangu alipokuwa Rais hatukuwahi kukutana wawili zaidi ya kukutana katika shughuli za kikazi, sikuwahi kufika nyumbani wala ofisini kwake, huwa sijikombi na sitafanya hivyo.”

huyu naye anatuchosha tu na swaga zake kwa nn hakusema wakati JPM yuko hai kama si unafiki.wakati mwingine tumwogope Mungu.
 
Hujui Mnyet. Ni mtoto wa dada ake marehemu?Ni mmoja Kati ya waliokua hawagusiki na waliokula Maisha kipindi Cha Mjomba wake akiwa madarakani.
Dah, kweli nasikia Mnyeti alikua bilionea kipindi cha Magufuli kutoka kuwa mwalimu hadi DC kisha RC kisha mbunge bilionea
 
Back
Top Bottom