Charles Kitwanga: Sioni umuhimu wa Nchi kufanya Sensa kila baada ya miaka 10

Je utaratibu ndio kama huu wenu wa kuuliza kama mna smartphone na kupiga tiki milango ?
Kuna shida gani? Sensa ya mwaka huu ilikuwa transformative; kiasi cha data kilichokusanywa ni kikubwa na cha maana sana; ingawa hakiwezi kuwa perfect lakini hata ikiwa 70-80 correct, kitakuwa na maana sana.
 
Ni mtazamo mzuri ila lazima tuelewane kua bado hatujafika huko. Ila tutafika kama tutakua na viongozi wenye maono.

Kwa sasa hivi tuna Watanzania wengi hawazaliwi kwenye vituo vya afya. Sizani kama hili lipo USA mnako kuzungumzia. Sasa Usipo fanya sensa hawa utajuaje taarifa zao.

Pia kuna vifo vinatokea na haviripotiwi vituo vya afya tafsiri yake havirekodiwi.Hili nalo ni kizuizi cha kutofanya SENSA.

Bado hakuna mifumo mizuri ya kushare data kutoka Taasisi moja kwenda nyingine hivyo ni ngumu kupata takwimu za uhakika bila kufanya SENSA.

Hata ukitumia wenye viti kufanya SENSA gharama bado iko pale pale. Kwa sababu lazima waende training na walipwe kwa kazi walio ifanya. Huwez mzungusha mwenyekiti kwa siku 11 asilipwe posho, nahakika hawezi kukubali na akikubali atafanya bora liende

Hata hivyo nakubaliana na mtazamo waje huenda miaka 50 tutaweza acha huu utaratibu.Ni swala la muda tyu kama tunavo endelea kupunguza matumizi ya kuni na mkaa.

Sent from my CPH1819 using JamiiForums mobile app
 
Kitwanga aache uongo.nakaa uingereza na nimefanya sensa mara mbili .sema hawatumii nguvu kama hiyo ya kwetu. Volume ya document inatumwa kila address na household wanazijaza mostly online bila mbwembwe za training wala nini. Kwa kuwa level ya civilization nadhani tunazidiana serikali ina confidence na self assessment sawasawa na upigaji wa kura .so labda kitwanga alimaanisha nchi zingine ila hapa uk sensa ni miaka 10 sawa na bongo
Nikiwa hapa moja ilikuwa March 2011 na mwaka jana march 2021. Huyu dingi akishakaa karibu na bia inabidi mic zizimwe la sivyo atazidi kuharibu.
 
Sawa, jana Makongoro Nyerere amemwambia kamisaa wa Sensa Anne Makinda kuwa mkoa wa Manyara wamehesabiwa watu takribani laki 3. Sasa kwa muundo huo watz si tutatangazwa kuwa tupo milioni 30 hivi kutoka milioni 50 ya 2012. Sensa 2022 ni zoezi lililofeli
 
Wizara Gani husika,,
SWALI gani hili unauliza?

Wizara husika means km NI takwimu za makazi wizara ya ardhi..sijui takwimu za walemavu iko wizara yake sijui mambo ya nishati iko wizara yake
 
Sababu deal CIA na pesa wanatoa wao basi sawa
 
Una Sasa unataka mkoa wa manyara wawe wangapi? Hata hivyo mkuu wa mkoa amejuaje takwimu za Wana manyara ilihali wenye dhamana ya kutangaza idadi ya watu waliohesabiwa wakati wa sensa ni NBS na ofisi ya mtakwimu mkuu ZANZIBAR. Na Rais ndiyo mhusika mkuu wa kutangaza idadi ya watu wote nchini.
 
Mkuu wapi nimesema 'ninataka' idadi ya watu mkoa wa Manyara iwe kadhaa? Mimi nimeeleeza kuwa kwa mujibu wa sensa hii huenda watanzania tukawa wachache sana maana takwimu zinazotajwa zina namba ndogo sana ukifananisha na takwimu zilizopatikana kwa sensa ya 2012. Itakuwa kinyume na tunavyoaminishwa kuwa tumezaliana sana
 
Inawezekana kweli ulichosema.
 
hii kauli usikute kaitoa baada ya kupiga KVant.
 
Jmn na huyo aliwahi kuwa Waziri nchi hii?? Sensa haichukui only taarifa za idadi ya watu.
Taarifa hizo zinaweza patikana kirahisi kama kila balozi au kata kutakuwa na uandikishaji wa watu pindi wanapohamia hiyo kata. Utasema unapokaa na tin number yako
 
Kwani Mkuu Serikali haijui imewafikia Wananchi wake kwa kiasi katika upande wa miundo mbinu na huduma za Kijamii kama vile Shule na Hospitali? Kwa mfano Serikali ina uwezo wa kujua idadi ya shule zinazomilikiwa na Serikali na watu binafsi nchi pamoja na vituo vyote vya huduma za afya kwa yenyewe kupitia idara zake ndiyo wanaidhinisha hayo mambo.
Nafikiri Kitwanga ana hoja ya Msingi katika kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ambapo fedha hizo zingetumika katika kuboresha maeneo mengine yenye uhitaji.
Binafsi naamini Serikali ina uwezo wa kupata takwimu sahihi za watu wake kwa kuzitumia vyema taasisi zake zilizotawanyika maeneo mbalimbali nchini.


Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Kunahitajika mfumo makini wa kusajili vizazi vyote na vifo vyote. Huenda tutakuwa na mfumo kama huo miaka 20 ijayo!
Ni rahisi kujua idadi ya waliozaliwa lakini ni ngumu sana kwenye kujua idadi ya vifo kwa sababu ni idadi ndogo sana ya watu wanaoripoti vifo hivyo kwenye taasisi husika.
 
Jmn na huyo aliwahi kuwa Waziri nchi hii?? Sensa haichukui only taarifa za idadi ya watu.
Jaribu kutafakari yupo sahihi kabisa labda kama ulikua mnufaika wa sensa
 
Sensa unajibu majibu mengi kuliko unavyidhani.
 
Angeongea wakati wa marehemu ningemuelewa hii naona kama anafurukuta tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…