NIDA ilitakiwa hata mtoto anapozaliwa basi apate kitambulisho amabacho RITA wanakuwa na kopy ya hicho hicho kitambulisho. Sasa hivi hata wageni wanaoishi hapa nchini wanapatiwa nida card.
Ilitakiwa hata bank wakihitaji taarifa za mteja za awali kama majina,umri, adress, kazi anayofanya, credit reference history vyote nida iwapa taarifa. Polisi wawe na access na nida, serikali ya mtaa,mahakamani, pension funds, mashuleni. Yaani nida ilitakiwa iwe kama social security ID no. Na hili linawezekana kwa uweke,aji uliofanywa nida lakini wanaogopa kuna watu wa kati watakosa ugali ikiwa nida itabeba kila kitu na hii ndio ingekuwa inaleta idadi kamili ya watu na makundi yao kama mgeni, mtoto, mlemavu, mgonjwa, anapaswa kulipa kodi anamiliki nini na ana shughuli gani.