Charles Kitwanga: Sioni umuhimu wa Nchi kufanya Sensa kila baada ya miaka 10

Ndo maana waafrika tunazidi kuwa Masikini kwa mambo kama haya Sensa
 
Jmn na huyo aliwahi kuwa Waziri nchi hii?? Sensa haichukui only taarifa za idadi ya watu.
Taarifa zote za sensa zinaweza kuwa tracked kidigitally. Unless uwezo wako wa kufikiri ni mdogo ndo maana huoni kama ni possible kupata taarifa zote bila kuhitajika kufanya sensa
 
Hata wangetumia wajumbe wa nyumba kumi wangepata data nzuri kwa gharama nafuu maana anawajua wakazi wa kila nyumba kwenye maeneo yao
Kuna watu Wana fungu lao Kama iyo lami ya dar to Moro so mtu anajiandaa kuwanyonya masikini yaani kwa wajinga Ni kupiga hela tu
 
Binafsi naamini hii ndo sensa ya mwisho.
 
NIDA ilitakiwa hata mtoto anapozaliwa basi apate kitambulisho amabacho RITA wanakuwa na kopy ya hicho hicho kitambulisho. Sasa hivi hata wageni wanaoishi hapa nchini wanapatiwa nida card.

Ilitakiwa hata bank wakihitaji taarifa za mteja za awali kama majina,umri, adress, kazi anayofanya, credit reference history vyote nida iwapa taarifa. Polisi wawe na access na nida, serikali ya mtaa,mahakamani, pension funds, mashuleni. Yaani nida ilitakiwa iwe kama social security ID no. Na hili linawezekana kwa uweke,aji uliofanywa nida lakini wanaogopa kuna watu wa kati watakosa ugali ikiwa nida itabeba kila kitu na hii ndio ingekuwa inaleta idadi kamili ya watu na makundi yao kama mgeni, mtoto, mlemavu, mgonjwa, anapaswa kulipa kodi anamiliki nini na ana shughuli gani.
 
Usemi wa jipu jipu! Jipu la kwanza kabisa nakumbuka alikuwa ni huyo Kitwanga
 
Hivi mkiwa na utaratibu mzuri wa kurekodi wageni na watoto wanaozaliwa kuna haja ya sensa ya kila baada ya miaka 10 ?
Useme kabisa huo utaratibu ufanyikaje,sio kukosoa bila kutoa njia
 
Taarifa zote zinazochukuliwa wakati wa sensa zinaweza kuchukuliwa wakati wote. Mfano idadi na aina ya nyumba...kila ujenzi usajiliwe kwa Mtendaji.
Yaani nikasajili nyumba yangu kwa mtendaji ?

Kwani wewe kuweza ?
 
😳 seriously! Tumeliwa
Huyu naye eti slikuwa anatutawala
Hivi ccm akili mliweka wapi?
Mnawaza matamanio yenu tuuuu kwa pesa za mvuja jasho
Masihi shuka dah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…