ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

Uongezefu wa maarifa uliozungumziwa hapo ni mkubwa kuliko ulivyorelate, akili mnemba ni very basic thing kwenye maarifa halisi ambayo yamemaanishwa.

Na si kwamba ukuaji wa maarifa haujawahi kutokea duniani, umetokea zaidi ya mara moja, rejea pale sodoma na gomola pamoja na pale kwenye mnara wa babel lakini pia hata ukisoma mwanzo wa uumbaji pale wana wa Mungu walipoanza kuona wana wa Adam na kile kizazi kilichozaliwa kutokana na muunganiko huo kulikua ni kizazi chenye balaa sana ambacho kilikua kinamchallenge Mungu hadi yeye mwenyewe alikiri kwamba mwanadamu ako na mawazo mabaya Kila siku.

Kwahiyo ongezeko la maarifa halihesabiwi kama ongezeko kama halileti challenge ya moja kwa moja kwa Mungu, na hii ndio uhesabiwa kama dhambi, kwa maana nyingine ni kwamba dhambi ni kile kitendo cha kuvuka mipaka na kuanza kufanya mambo beyond uwezo wa kawaida wa mwanadamu.

Kwahiyo Dunia iko inaendelea kujitahidi kutransform knowledge kuelekea pazuri ila level uliyoizungumzia wewe bado sana hasa kwa mtu mmoja mmoja.

Na ndio maana utaona hizi AI hazijaja bahati mbaya ila zimekuja kwa kusudi na ndio maana pia utaona hizi AI hazifanyi mambo beyond uwezo wa binadamu isipokua zinatunza kumbukumbu ambazo binadamu wanazo kwahiyo zinafanya Kila kitu ambacho kinafanywa na binadamu na kuishia hapo kwa maana hazifanyi kitu chochote beyond uwezo wa kibinadamu.

Kwahiyo ili tufike huko unakosema hadi pale ambapo watatokea watu wenye uwezo mkubwa na kuanza kuleta vitu venye kufanya mambo makubwa ambayo binadamu Hana uwezo wa kuyafanya na wala Hana uwezo wa kuyacontrol kama ambavyo anauwezo wa kucontrol gari au ndege na meli na hata robots.

Sasa sodoma na gomola kabla haijaangamizwa ilikua na watu wa namna hii, mtu anaweza akakaa zake maabara akatengeneza kiumbe cha ajabu na kikawa na uwezo wa kufanya mambo ya ajabu pasipo kuamuliwa hata na yule ambae amekitengeneza (kizazi chetu hiki cha social media, ukifunua ubongo unakutana na simba, yanga, man u, liver, arsenal, mara muziki na kadhalika, hata ukikipatia miaka mia mbele hakiwezi kufika kwenye hatua unayoisemea wewe).

So kama hiko ndio kigezo chako cha kudefine mwisho wa Dunia basi endelea kufurahia kwa maana bado sana mkuu.

Oops, nataka kusahau tena... Naomba nitajie kanisa unalohudumu ili nijumuike nawe this Sunday... Thanks in advance.
Umeandika Point mkuu 👍😊
 
Wenzio wako maabara wanaumiza kichwa kutafta solution mbalimbali maishani mwetu.

Afu wee unakesha makanisani kusubiri miujiza ili ukifa unyakuliwe😅
 
Kama ungesoma kwanza comments/replies zangu zote, usingeandika hayo. Niliishaeleza, chatGPT nimeitaja tu kwa sababu ndiyo habari ya mjini. Maarifa yameongezeka katika nyanja nyingi. Sio AI pekee
 
Miaka takriban 2500 iliyopita, Mungu alimwambia Nabii Danieli awaambie watu kuwa wakati wa mwisho maarifa yataongezeka. Tunasoma hivyo katika kitabu cha Danieli 12:4: "Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka."

Leo, tunaona wazi kutimia kwa unabii huo kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia, hasa katika Akili Mnemba. Zamani, maarifa yalihifadhiwa katika vitabu na kupatikana polepole, lakini sasa, kwa sekunde chache tu, mtu anaweza kupata maarifa na taarifa nyingi kwa njia ya mitandao, AI, na mifumo ya kisasa ya kompyuta. Akili Mnemba si tu kwamba inachakata taarifa haraka, bali pia inajifunza, inafikiri, na hata kusaidia kufanya maamuzi magumu. Ni dhahiri, maarifa yameongezeka kama ilivyotabiriwa.

Kuongezeka kwa maarifa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Katika Mathayo 24:3-14, Yesu alieleza ishara na dalili nyingine zitakazotokea kabla ya kuja kwake na kabla ya mwisho wa dunia. Dalili na ishara hizo karibu zote zimeishatimia. Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa Biblia ni kitabu cha kuaminika. Kwa wanaoamini kitabu hiki, kuongezeka huku kwa maarifa ni maonyo kwamba nyakati tulizo nazo si za kawaida. Huu ni wakati wa kuwa macho, ni wakati wa kujiandaa kiroho, na kusimama imara kwa Mungu, kwa kuwa siku ya kurudi kwa Yesu imekaribia!

Ibilisi anajua wakati uliobaki ni mchache(Ufunuo 12:12), kwa sababu hiyo anafanya kila jitihada kuwashawishi watu wasiamini kuwa Mungu yupo. Anatumia mbinu nyingi kuwashawishi watu wazame katika matendo ya dhambi kama ushoga, uzinzi, ulevi, wizi, uongo nk, ili siku hiyo ikifika waachwe, maana Yesu akirudi atawachukua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu(Mathayo 24:21); na hatimaye siku ya mwisho wote wasioamini watatupwa pamoja na Ibilisi katika moto wa milele(Mathayo 25:41).

Wimbo huu na picha hizi zimetengenezwa kwa msaada wa chatGPT/AI
View attachment 3235549 View attachment 3235550View attachment 3235551View attachment 3235552View attachment 3235553
Huwez kwenda mbinguni kama jina lako halijaandikwa kwenye kile kitabu cha uzima.
 
Hujasikiliza huo wimbo nilioutengeneza kwa msaada wa chatGPT? Hiyo ni solution tayari ya shida niliyokuwa naipata katika kutengeneza nyimbo.
 
Huwez kwenda mbinguni kama jina lako halijaandikwa kwenye kile kitabu cha uzima.
Jina langu liliishaandikwa zamani katika kitabu cha uzima, labda wewe ndo bado
 
Hata baada ya kugunduliwa kwa radio na simu watu waliona maarifa yameongezeka. Hapa baado kabisa tukifika 2050 kuzazi hicho kitakuwa kinatushangaa tuliishije, so relax Mkuu
 
Kuhan mwenye tabia ya kujikinai. Mi nachechemea nikifanya bidii ili niifikie viwango Mungu avitakavyo cjihesabii kuwa nimeshafika na kaza mwendo.
 
Miaka takriban 2500 iliyopita, Mungu alimwambia Nabii Danieli awaambie watu kuwa wakati wa mwisho maarifa yataongezeka. Tunasoma hivyo katika kitabu cha Danieli 12:4: "Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka."

Leo, tunaona wazi kutimia kwa unabii huo kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia, hasa katika Akili Mnemba. Zamani, maarifa yalihifadhiwa katika vitabu na kupatikana polepole, lakini sasa, kwa sekunde chache tu, mtu anaweza kupata maarifa na taarifa nyingi kwa njia ya mitandao, AI, na mifumo ya kisasa ya kompyuta. Akili Mnemba si tu kwamba inachakata taarifa haraka, bali pia inajifunza, inafikiri, na hata kusaidia kufanya maamuzi magumu. Ni dhahiri, maarifa yameongezeka kama ilivyotabiriwa.

Kuongezeka kwa maarifa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Katika Mathayo 24:3-14, Yesu alieleza ishara na dalili nyingine zitakazotokea kabla ya kuja kwake na kabla ya mwisho wa dunia. Dalili na ishara hizo karibu zote zimeishatimia. Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa Biblia ni kitabu cha kuaminika. Kwa wanaoamini kitabu hiki, kuongezeka huku kwa maarifa ni maonyo kwamba nyakati tulizo nazo si za kawaida. Huu ni wakati wa kuwa macho, ni wakati wa kujiandaa kiroho, na kusimama imara kwa Mungu, kwa kuwa siku ya kurudi kwa Yesu imekaribia!

Ibilisi anajua wakati uliobaki ni mchache(Ufunuo 12:12), kwa sababu hiyo anafanya kila jitihada kuwashawishi watu wasiamini kuwa Mungu yupo. Anatumia mbinu nyingi kuwashawishi watu wazame katika matendo ya dhambi kama ushoga, uzinzi, ulevi, wizi, uongo nk, ili siku hiyo ikifika waachwe, maana Yesu akirudi atawachukua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu(Mathayo 24:21); na hatimaye siku ya mwisho wote wasioamini watatupwa pamoja na Ibilisi katika moto wa milele(Mathayo 25:41).

Wimbo huu na picha hizi zimetengenezwa kwa msaada wa chatGPT/AI
View attachment 3235549 View attachment 3235550View attachment 3235551View attachment 3235552View attachment 3235553

Yoshua 8​

Mji wa Ai unatekwa
1Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usiwe na wasiwasi wowote; wachukue wanajeshi wako wote uelekee mji wa Ai, kwani mfalme wa Ai nimemtia mikononi mwako, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake. 2Mtautendea mji wa Ai pamoja na mfalme wake kama vile mlivyoutendea mji wa Yeriko pamoja na mfalme wake. Mali zake pamoja na mifugo yake mtakayoteka itakuwa ni mali yenu. Nendeni mwuvamie mji kutoka upande wa nyuma.”
3Basi, Yoshua akaondoka, pamoja na wanajeshi wake wote kwenda Ai. Akawachagua watu hodari 30,000 na kuwaambia watangulie wakati wa usiku.......

Mji wa Artificial intelligence, technology ilipozidi ikabidi uangamizwe, haya mambo yameanza kitambo..
Ai ya zamani ndio ilikuwa kiboko, hii Ai bado sana..
 
Kama ungesoma kwanza comments/replies zangu zote, usingeandika hayo. Niliishaeleza, chatGPT nimeitaja tu kwa sababu ndiyo habari ya mjini. Maarifa yameongezeka katika nyanja nyingi. Sio AI pekee
Ooh sorry nilicomment tu baada ya kusoma Uzi wenyewe ila pia nikwambie tu bado Dunia Haina maarifa yoyote mapya, na hakuna jambo lolote lililopo hapa kwa bahati mbaya yaani hakuna jambo la surprise yote ni yale yale tu.

Au kama lipo ila Mimi silijui nijuze tafadhali.
 
Hata baada ya kugunduliwa kwa radio na simu watu waliona maarifa yameongezeka. Hapa baado kabisa tukifika 2050 kuzazi hicho kitakuwa kinatushangaa tuliishije, so relax Mkuu
Sio lazima iwe hivyo. Tangu ulipoanza kula chumvi imepita miaka mingapi. Kuna chumvi mpya umeiona
 
Ooh sorry nilicomment tu baada ya kusoma Uzi wenyewe ila pia nikwambie tu bado Dunia Haina maarifa yoyote mapya, na hakuna jambo lolote lililopo hapa kwa bahati mbaya yaani hakuna jambo la surprise yote ni yale yale tu.

Au kama lipo ila Mimi silijui nijuze tafadhali.
Hili la chatGPT ni lilelile? Duh
 
Yoshua 8​

Mji wa Ai unatekwa
1Mwenyezi-Mungu akamwambia Yoshua, “Usiogope, wala usiwe na wasiwasi wowote; wachukue wanajeshi wako wote uelekee mji wa Ai, kwani mfalme wa Ai nimemtia mikononi mwako, pamoja na watu wake, mji wake na nchi yake. 2Mtautendea mji wa Ai pamoja na mfalme wake kama vile mlivyoutendea mji wa Yeriko pamoja na mfalme wake. Mali zake pamoja na mifugo yake mtakayoteka itakuwa ni mali yenu. Nendeni mwuvamie mji kutoka upande wa nyuma.”
3Basi, Yoshua akaondoka, pamoja na wanajeshi wake wote kwenda Ai. Akawachagua watu hodari 30,000 na kuwaambia watangulie wakati wa usiku.......

Mji wa Artificial intelligence, technology ilipozidi ikabidi uangamizwe, haya mambo yameanza kitambo..
Ai ya zamani ndio ilikuwa kiboko, hii Ai bado sana..
Hahaa, soma Biblia kwa utulivu
 
Back
Top Bottom