ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

Kwani huo unabii umetabiri ndege, redio ama chatGpt?

Akili zako finyu ndio zimekutuma chatgpt, ndege n.k ndio kuongezeka kwa maarifa.

Daniel hakutabiri hayo maarifa unayoyawaza wewe.
Yataje wewe maarifa unayofikiri ndiyo yaliyotabiriwa na Danieli
 
Biblia haisemi hivyo ulivyoandika. Biblia yangu inasema:
Mathayo 24:14 (NEN)
"Injili hii ya ufalme itahubiriwa ulimwenguni kote kuwa ushuhuda kwa mataifa yote. Ndipo mwisho utakapokuja."
Kwa kasi hii ya kuongezeka kwa maarifa unafikiri itachukua miaka 100 Injili kuwafikia watu wote duniani. Sherehe tu za kuapishwa kwa Rais Trump ("Rais wa Dunia") zimefuatiliwa na mamilioni ya watu duniani. Katika sherehe hizo Rais Trump aliombewa na Wachungaji wazi wazi kwa Jina la Yesu. Huo tayari ni ushuhuda kwa watu wa Russia, Afghanistan, China na kote kwingine. Hao Wahadzabe unaowasema tayari wameishafikishiwa Injili na "wamisionari."
Kaa tayari mpendwa, "Kwa kuwa bado kitambo kidogo tu, yeye ajaye atakuja wala hatakawia.”(Waebrania 10:37 NEN)
Ndugu tuliza mizuka. Hii dunia sio ya wakristo peke yao.
 
Miaka takriban 2500 iliyopita, Mungu alimwambia Nabii Danieli awaambie watu kuwa wakati wa mwisho maarifa yataongezeka. Tunasoma hivyo katika kitabu cha Danieli 12:4: "Lakini wewe, Ee Danieli, yafunge maneno haya, ukakitie mhuri kitabu, hata wakati wa mwisho; wengi wataenda mbio huku na huko, na maarifa yataongezeka."

Leo, tunaona wazi kutimia kwa unabii huo kupitia maendeleo makubwa ya teknolojia, hasa katika Akili Mnemba. Zamani, maarifa yalihifadhiwa katika vitabu na kupatikana polepole, lakini sasa, kwa sekunde chache tu, mtu anaweza kupata maarifa na taarifa nyingi kwa njia ya mitandao, AI, na mifumo ya kisasa ya kompyuta. Akili Mnemba si tu kwamba inachakata taarifa haraka, bali pia inajifunza, inafikiri, na hata kusaidia kufanya maamuzi magumu. Ni dhahiri, maarifa yameongezeka kama ilivyotabiriwa.

Kuongezeka kwa maarifa ni moja ya dalili za siku za mwisho. Katika Mathayo 24:3-14, Yesu alieleza ishara na dalili nyingine zitakazotokea kabla ya kuja kwake na kabla ya mwisho wa dunia. Dalili na ishara hizo karibu zote zimeishatimia. Huu ni uthibitisho wa wazi kuwa Biblia ni kitabu cha kuaminika. Kwa wanaoamini kitabu hiki, kuongezeka huku kwa maarifa ni maonyo kwamba nyakati tulizo nazo si za kawaida. Huu ni wakati wa kuwa macho, ni wakati wa kujiandaa kiroho, na kusimama imara kwa Mungu, kwa kuwa siku ya kurudi kwa Yesu imekaribia!

Ibilisi anajua wakati uliobaki ni mchache(Ufunuo 12:12), kwa sababu hiyo anafanya kila jitihada kuwashawishi watu wasiamini kuwa Mungu yupo. Anatumia mbinu nyingi kuwashawishi watu wazame katika matendo ya dhambi kama ushoga, uzinzi, ulevi, wizi, uongo nk, ili siku hiyo ikifika waachwe, maana Yesu akirudi atawachukua na kuwapeleka mbinguni wale tu waliotubu dhambi zao na kumwamini Yesu. Watakaoachwa watabaki katika dhiki kuu ambayo haijawahi kuwepo tangu kuumbwa kwa ulimwengu(Mathayo 24:21); na hatimaye siku ya mwisho wote wasioamini watatupwa pamoja na Ibilisi katika moto wa milele(Mathayo 25:41).

Wimbo huu na picha hizi zimetengenezwa kwa msaada wa chatGPT/AI
View attachment 3235549 View attachment 3235550View attachment 3235551View attachment 3235552View attachment 3235553
Haya Yote Nimeyapenda ila Mimi Kitu kimoja tu..

Naomba Uniambie Na Unitonye Kwa siri Umetumia AI ipi au Link ipi Kutengeneza Hiyo Nyimbo Imetulia Sana
 
Wee Leo hii unaishangaa AI,

Wenzio kina BushMen waliishangaa chupa ya coca-cola iliyoshuka toka angani ikazua kuzaa zaa Kijiji kizima

Wale WA stoneAge waliishangaa Sana kilivovumbuliwa chuma na maisha yakaendelea

Kuna wenzio waliishangaa umeme enzi zile za mafuta ya Taa na mishumaa.

Binadamu anazidi kufunguka, na atafunguka na kuvumbua ata wee ukishakufa.

Nnachoamini Mimi,
Hakuna tatizo lisilokua na solution,
Hakuna Cha siku ya mwisho Wala ufufuo
Ukifa Wewe waliobaki wanaendeleza cycle
 
Wee Leo hii unaishangaa AI,

Wenzio kina BushMen waliishangaa chupa ya coca-cola iliyoshuka toka angani ikazua kuzaa zaa Kijiji kizima

Wale WA stoneAge waliishangaa Sana kilivovumbuliwa chuma na maisha yakaendelea

Kuna wenzio waliishangaa umeme enzi zile za mafuta ya Taa na mishumaa.

Binadamu anazidi kufunguka, na atafunguka na kuvumbua ata wee ukishakufa.

Nnachoamini Mimi,
Hakuna tatizo lisilokua na solution,
Hakuna Cha siku ya mwisho Wala ufufuo
Ukifa Wewe waliobaki wanaendeleza cycle
Pole. Subiri siku inakuja utajua ulikuwa hujui
 
Back
Top Bottom