ChatGPT imetimiza unabii uliotolewa takriban miaka 2500 iliyopita!!

Hapa sasa unataka kubishana na biblia... Kasome tena, this time usisome kama gazeti mkuu😅😅😅
Mwanzo 18:20 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akasema, “Kuna malalamiko mengi dhidi ya watu wa Sodoma na Gomora, na dhambi yao ni kubwa mno.

Yuda 1:7 BHN
Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote.
 
Hapa sasa unataka kubishana na biblia... Kasome tena, this time usisome kama gazeti mkuu😅😅😅
Mwanzo 6:5,7SRUV
BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote...
BWANA akasema, Nitamfutilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi; mwanadamu na mnyama, na kitambaacho na ndege wa angani; kwa maana naghairi ya kwamba nimewaumba.

Nimekutajia mistari inayoonyesha kwanini Sodoma iliangamizwa kwa moto na kwanini wakati wa Nuhu watu waliangamizwa kwa gharika. Weka na wewe mistari yako inayosema walimchallenge Mungu ndio sababu wakaangamizwa.
 
Mkuu. Unafikiri sikumbuki maswali ninayojibu? NImeishakuambia hilo swali nimeishalijibu. Soma comments/replies zangu zote kuanzia mwanzo.
Miaka 2500 iliyopita, wakati unabii huu unatolewa, maarifa yalikuwa yanapungua au yanaongezeka?

Nimetafuta kwenye replies zako sijaona jibu la hili swali..
 
Pole, kumbe unachechemea. Mi napiga mbio niifikie mede ya thawabu
Ufikie tena. Kumbe hujaandikwa kwenye kitabu cha uzima basi. Tuko pamoja. Nakukumbusha tu huwez kuvishwa taji mwanzo wa mashindano mpaka mwisho so wewe ujidhaniae umesimama kuwa makini ucje ukaanguka kwa kibur cha kujiona uko perfect kama mafarisayo
 
Yohana 1:12
"Bali wote waliompokea, yaani wale walioliamini jina lake, aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu."
Ukiishampokea Yesu unafanyika mtoto wa Mungu; papo hapo jina lako linaandikwa katika kitabu cha uzima. Kupokea thawabu ndio mwishoni kwa sababu kila mtu atapata thawabu kulingana na kazi aliyofanya tangu alipompokea Yesu hadi siku alipoumaliza mwendo. Mwapotea kwakuwa hamyajui Maandiko.
 
Miaka 2500 iliyopita, wakati unabii huu unatolewa, maarifa yalikuwa yanapungua au yanaongezeka?

Nimetafuta kwenye replies zako sijaona jibu la hili swali..
Mkuu, huwezi kupima kupungua au kuongezeka kwa maarifa siku ya kutolewa kwa unabii. Unapima ongezeko la maarifa baada ya unabii kutolewa. Sasa pima maarifa yaliyokuwepo miaka 2500 iliyopita ulinganishe na maarifa yaliyopo sasa, utapata jibu, yamepungua au yameongezeka.
 
Sawa mkuu nimekupata vyema.
Mkuu, amekupotosha! Wakati wa Nuhu na wakati wa Sodoma watu waliangamizwa kwa sababu uovu wao ulikuwa umezidi sio kwa sababu ya kum-challenge Mungu.
Mwanzo 18:20 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akasema, “Kuna malalamiko mengi dhidi ya watu wa Sodoma na Gomora, na dhambi yao ni kubwa mno.

Yuda 1:7 BHN
Kumbukeni pia Sodoma na Gomora, na miji ya kandokando yake; wenyeji wake walifanya kama wale malaika; walifanya uzinzi na mambo yaliyo kinyume cha maumbile, wakapewa hukumu ya moto wa milele, iwe onyo kwa watu wote.
 
Walokole Acheni kuunga unga na kudandia vijimatukio,ata kutokea Kwa corona mlisema ndo siku ya mwisho iliyotabiriwa 😅
Corona ni moja ya ishara za kuja kwa Yesu kama ilivyotabiriwa katika Mathayo 24:7. "There will be pestilences...” Corona ni pestilence(ugonjwa mbaya)
 
Aisee,
Ngoja nipate muda nisome biblia vyema inawezekana nikaokota viwili vitatu.
 
Kipindi cha Kuanzia Miaka 2500 kabla ya kutolewa unabii hadi siku ya kutolewa unabii, maarifa yaliongezeka au yalipungua?
 
Wakati Redio inavumbuliwa ilionekana ni sayansi ya kipekee na ya mwisho kabisa,
 
Account yako imekuwa-hacked?
Nadhani akili yako imeanza kupiga short.. 😊, nitaiweka sawa tu.., jibu swali…

Kipindi cha Kuanzia Miaka 2500 kabla ya kutolewa unabii hadi siku ya kutolewa unabii, maarifa yaliongezeka au yalipungua?
 
Nadhani akili yako imeanza kupiga short.. 😊, nitaiweka sawa tu.., jibu swali…

Kipindi cha Kuanzia Miaka 2500 kabla ya kutolewa unabii hadi siku ya kutolewa unabii, maarifa yaliongezeka au yalipungua?
Nimeishakujibu
 
Nadhani akili yako imeanza kupiga short.. 😊, nitaiweka sawa tu.., jibu swali…

Kipindi cha Kuanzia Miaka 2500 kabla ya kutolewa unabii hadi siku ya kutolewa unabii, maarifa yaliongezeka au yalipungua?
Mstari mzima unasema "watu wataenda mbio huku na huko na maarifa yataongezeka." Leo hii watu wanaenda mbio sana kwa magari na kwa ndege, huwezi kamwe kulinganisha mbio za leo na za wakati ule. Hivyo ni dhahiri wakati unaozungumwa ni huu, sio kabla ya miaka 2500.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…