Chato, Geita: Rais Magufuli afungua jengo la Mahakama ya Wilaya na kuweka jiwe la msingi jengo la Zimamoto

Chato, Geita: Rais Magufuli afungua jengo la Mahakama ya Wilaya na kuweka jiwe la msingi jengo la Zimamoto

Aliyoyasema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.

#Ujenzi wa Mahakama hii utasaidia kupunguza ucheleweshwaji wa uendeshaji wa mashauri hivyo naipongeza Mahakama kwa kuamua kujenga Mahakama hii wilayani Chato mkoani Geita.

#Pia naipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kujenga gereza katika wilaya hii.

#Mahakama sio majengo pekee, tangu mwaka 2015 tumeteua Majaji wa Mahakama ya Rufaa 11, Majaji wa Mahakama Kuu 39 na tumeajiri Mahakimu 396, Serikali itaendelea kuajiri Watumishi wa Mahakama kadri itakavyowezekana.

#Natoa rai kwa vyombo vyote vinavyohusika na kutoa haki kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha haki za Watanzania zinapatikana kwa wakati.

#Nawapongeza Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa jitihada zenu za kuokoa maisha ya watu na mali zao, pia nawapongeza katika ukusanyaji wa mapato kwani kuanzia mwaka 2015 mmekusanya zaidi ya shilingi Bil. 73.

#Jeshi la Zimamoto na Uokoaji endeleeni kuchapa kazi kwa bidii ili yale malalamiko yanayotolewa na wananchi yapungue ikiwezekana yaishe kabisa.

Aliyoyasema Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma.

#Kuanzia mwaka wa Fedha 2017-2019 tumekamilisha ujenzi wa Mahakama Kuu mbili za Mikoa ya Kigoma na Musoma, nyumba tatu za kufikia Majaji mkoani Mtwara, Mahakama za Hakimu Mkazi tatu pamoja na za Wilaya 13.

#Tunaendelea na maandalizi ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya Mahakama jijini Dodoma ambapo mpaka sasa tumeshapata kiwanja, tunaendelea na hatua za kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.

#Katika jitihada za kuhakikisha wananchi wanapata huduma kwa wakati, hivi karibuni tunategemea kuanza ujenzi wa majengo ya Mahakama Kuu ambayo ni majengo jumuishi yatayojumuisha huduma zote katika jengo moja.

Aliyoyasema Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.

#Tunamshukuru Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutenga jumla ya shilingi Milioni 713 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Chato mkoani Geita.

#Endapo jengo hili lingejengwa kwa utaratibu wa kawaida wa kutumia Wazabuni lingetumia jumla ya sh. Bil.1.6 hivyo tumeokoa fedha nyingi.

#Ujenzi wa ofisi na kituo cha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Wilaya ya Chato ulianza Octoba, 2019 na unatarajiwa kukamilika Februari, 2020.
1576662571262.png
 
Kila kitu kwake jamani. hakika vitabomolewa ili usijenge precedence ya rais kupendelea kwake. Vitabomolewa kama majengo yote ya ccm iliyorithi toka chama kimoja enzi za Nyerere yatataifishwa kuwa majengo ya serikali
Yatataifishwa na serikali ya CCM?
 
Kila kitu kwake jamani. hakika vitabomolewa ili usijenge precedence ya rais kupendelea kwake. Vitabomolewa kama majengo yote ya ccm iliyorithi toka chama kimoja enzi za Nyerere yatataifishwa kuwa majengo ya serikali

..hapana.

..busara ni kuhamia Chato kufuata fursa na maendeleo.

..kama wananchi walihama kanda ya kusini kuja Dsm kufuata maendeleo, kwanini washindwe kuhama toka maeneo mengine kwenda Chato kufuata maendeleo?
 
Hivi jengo la mahakama ya Wilaya ni lazima lifunguliwe na Rais wa Nchi ?
 
Tuko bize kufuatilia chama kuu LA upinzani na chama tawala2020 wakifanya uchaguzi,

Hiyo ya kufungua mahakama hata hakimu mfawidhi anaweza fungua
 
Yeeeeeeea kwenye vyeo tu ndo pamenikosha 💕💕
 
Kwa wale waliofika hata darasa la tatu jiografia yao itawabana na kuwaelekeza kuwa katika ramani ya taifa letu ukiigawa katika pande NNE kuu za dunia kaskazini utaikuta mikoa ya mwanza ,shinyanga,Geita, arusha,Mara na manyara

Ukiongeza pande nane za dunia kaskazini magaribi utaukuta mkoa wa kagera na kaskazini mashariki utakuta mikoa ya Kilimanjaro na tanga .hivyo kuifanyanya chato iwe katika mikoa iliyo kaskazini haswaa ya nchi yetu na kama utaongeza pande kumi na sita bado greed references nazo zitakuongozwa kuwa chapo ipo wapi
(Pitia ramani kule chini na greed references)

Licha ya kuwa chato inatoa rais wa sasa mkoa mwingine jirani tu mkoa wa geita chato inapopatikana kuna mkoa wa Maranao umetoa rais wa kwanza wa taifa hili hivyo kufanya mikoa ya kaskazini kuwa na marais wawili licha ya mikoa hii (KUBANDIKWA JINA LA KANDA YA ZIWA KWA SABABU TU INAPAKANA NA MAZIWA MAKUBWA KATIKA TAIFA HILI HII IPO KIUTAWALA ZAIDI ) jiografia haitabadilika na chato itabaki kaskazini

Licha ya chato kuwa kaskazini kama nilivyoainisha hapo juu na kwa msaada wa Google map na mistari ya longitudes na latitudes bado chato inahitaji maendeleo kama eneo la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Tuwaambie wote wanaobeza maendele miradi inayowekwa chato kuwa ipo miradi mingi nchini sio chato tu

Tuwaambie wote wanaosema kaskazini imetengwa huku wakisema chato inaendelezwa kuwa na chato ipo kaskazini tena ndio kaskazini haswaa

Tuwaelimishe walisiojua kuwa maendeleo hupangwa kulingana na uhitaji tuwaeleze

Tuwaeleze kuwa kila eneo katika taifa hili linamaana na hukaliwa na watanzania wenzetu


USSR
Screenshot_20191220-030216.jpeg
IMG-20191220-WA0001.jpeg
Screenshot_20191220-031153.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom