Chato: Kituo cha Polisi Muganza chachomwa moto na wananchi kupinga mauaji ya mtuhumiwa anayedaiwa kusababibishiwa kifo na Polisi

Chato: Kituo cha Polisi Muganza chachomwa moto na wananchi kupinga mauaji ya mtuhumiwa anayedaiwa kusababibishiwa kifo na Polisi

Bodaboda Amepigwa Na Polisi Na Kumsababishia Kifo Ndipo Wananchi Wameandamana Na Kuvunja Kituo Cha Polisi Watu Wawili Wamesha Poteza Maisha Kutokana Na Ufyatuaji Wa Risasi Na Mabomu Ya Machozi

Npo Kwenye Tukio Nitaendelea Kuwapa Taarifa
Hee imekuwaje Tena nyumbani kwa hayati?polen,tatizo nn lakin?
 
Kila kona ni mauaji ya raia yakifanywa na Polisi
 

Attachments

  • VID-20230330-WA0000(1).mp4
    5.4 MB
Bodaboda Amepigwa Na Polisi Na Kumsababishia Kifo Ndipo Wananchi Wameandamana Na Kuvunja Kituo Cha Polisi inadaiwa Watu Wawili Wamesha Poteza Maisha Kutokana Na Ufyatuaji Wa Risasi Na Mabomu Ya Machozi

Npo Kwenye Tukio Nitaendelea Kuwapa Taarifa

--
View attachment 2571126
Watu wa Chato ikataeni CCM inamdharau Magufuli? Unganisheni hapo hapo maandamano ya kudai katiba mpya huo ndio mwanzo wa mabadiliko.
 
ningekuwepo ningehakikisha naondoka na roho ya Polisi wajinga sana hawa watu sijui walilaaniwa na nani mbwa hawa
 
Haiwezekani bodaboda auawe na polisi harafu wananachi wakichukua maamuzi munaonq waonni wabaya..Haiwezekani..Mie nawaunga mkono hao wananachi WA Mganza Kwa hatua walizozichukua
 
Geita. Jeshi la Polisi wilayani Chato mkoani Geita limelazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waombolezaji na wananchi wa Kata ya Mganza, kufuatia vurugu zilizotokea wakati wa maziko ya kijana Enos Misalaba (32) anayedaiwa kukamatwa na polisi kisha kupigwa na kusababisha kifo chake.
Mkuu wa Wilaya ya Chato, Deusdedith Katwale amethibitisha kutokea tukio hilo na kusema yupo njiani kuelekea eneo la tukio na taarifa zaidi atazitoa baada ya kufika Mganza.
Kaka wa marehemu, Samweli Misalaba akizungumza na Mwananchi kwa njia ya simu, amesema wakiwa kwenye eneo la maziko kwa taratibu za mazishi, wananchi walikataa kuendelea na maziko baada ya msomaji risala ya marehemu kusema amekufa kwa ugonjwa wa kifua na siYo kupigwa kama jamii inavyoamini.
“Tulikubali kuzika, tumeshachimba kaburi wakati wa historia ya marehemu msomaji alisoma kuwa amekufa kwa kuugua kifua ndio wananchi wakakataa na kubeba jeneza na kuurudisha mwili kituoni wakitaka waelezwe kifo cha marehemu kimetokana na nini. Wakarudisha mwili kituoni polisi, wakaanza kupiga mabomu ya machozi na wananchi wakaendelea kuandamana,” amesema ndugu wa marehemu.
Enos Misalaba anadaiwa kukamatwa siku ya Jumatatu Machi 27 akituhumiwa kuiba betri ya gari na alikamatwa na polisi wa Kituo cha Mganza. Inadaiwa alipigwa na kuzidiwa kisha kupelekwa kwenye Kituo cha Afya Mganza na Jumanne asubuhi alipoteza maisha akipatiwa matibabu.

MWANANCHI.
 
Back
Top Bottom