Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

Uchaguzi 2020 Chato: Msafara wa Tundu Lissu washambuliwa kwa mawe

ilifika mahala kila mwanaccm akipata chochote hata kwa kushinda shambani hukimbilia kumshukuru kumsifu magufuli hata mvua ikinyesha wanamshuru magufuli
Acha hiyo tuu, unaweza kuta Katibu CCM wilaya mkewe kajifunga anasema " tumefanikiwa kupata mtoto wa kike Leo mchana, tunashukuru Mungu na Rais Magufuli kwa mke wangu kujifungua salama hospitalini"
 
Too sad ,tushindane kwa hoja sio mawe aisee ,uhuni wa aina hii ni wa kukemewa kwa nguvu zote maana hautusaidii .
 
Ndio ulichoelewa! 😆
Kwa hiyo alipopigiwa jiwwr ni Naeiasit?noma Chadema nasikia hawana hata pesa za kuweka mabango ya wagombea, hizo pesaw za kukodi watu wemepata wapi?
 
Mheshimiwa Tundu Lissu aamuru Barabara ya Chato Kufungwa baada ya wafuasi wa CCM kushambulia kwa mawe msafara wake na kuharibiwa gari la vifaa vya muziki (PA).

View attachment 1599022
View attachment 1599076
Ukiona umesongwa sana na natatizo yameibuka ujuwe basi kunakaribia kucha. Wanasema mti wenye maembe yalowiva ndio inatupiwa mawe kwa wingi.

Msikate tamaa kwani kunakucha muda si mrefu Mungu ndiye anaweka giza na kuleta Mwanga. Kitaeleweka.
 
Wamekodisha vibarya toka chato na Bariadi. Huyo jamaa makazi yake yako bariadi
Magufuli mwenyewe kwao siyo chato bali kalazimisha kuwepo kwa nguvu za Polisiccm, mara baada ya uchaguzi atarejea kwao Burundi
 
ni ujinga kujitoa muhanga kwa ajili ya siasa!
jali maisha yako na familia yako....siasa ni mapito tu....
unatoka katoro mbali kote unaacha kazi zako na familia yako kisa siasa?!!
Tukiwa na Taifa la watu kama wewe ni hatari sana.

Watawala ndio wanaotaka iwe hivyo lakini wao hawafanyi hivyo mana wanajua kuwa siasa ni sehemu ya maisha yao.
CCM wengi wanajali familia zao na maisha yao ndio kama unavyosema na ndio maana haya maovu yote yanatokea.

Ni wanyama tu ndio wanaojali maisha yao na watoto wao tu. Lakini Binadam anapaswa kujali maisha ya kila mmoja yawe ya haki. Ndio maana kuna wanajeshi wanaotoa maisha yao kwa ajili ya wengine waishi kwa amani na raha mustarehe. Mara nyingi hawa ni wale wanaotoka katika familia duni na wamekosa Fursa. Huwezi ukamkuta mtoto wa Waziri anakua Polisi au Mwalimu wa shule ya msingi au Sekondari ya Kata. Huwezi ukamuona mtoto wa Rais anakua Mgambo akalinde Geti la soko au la ushuru wa mazao.

Binafsi nawaheshimu sana watu wanaosimama upande wa maskini na upande Dhaifu. Hao ndio wanaopanda mbegu ya haki na mabadiliko tangu enzi za manabii.

Hivi unadhani Gwajima anaweza kugombea ubunge kupitia Chama cha upinzani wakati ni bilionea na ameshazoea maisha ya Raha.
Mara nyingi hua namtafakari JPM kuwa kama ni kweli ana uchungu na nchi hii mpaka anaona kuwa urais ni mzigo mkubwa je, ni kwa nini alishiriki katika maamuzi yote mabaya yaliyoliletea taifa hili hasara kubwa na kuibiwa tangu awamu ya Tatu?

Kwa nini hakuwahi kuipinga serikali na kuikosoa wazi wazi badala yake amekua akiitumia serikali kuwaumiza wananchi wakati akijua wazi kabisa kuwa Makosa yote yalisababishwa na serikali zilizopita. Mfano kuacha watu wajenge hovyo halafu anakuja anatumia dola kuwavunjia bila fidia .

Alipaswa akatae na kusema hawa ni watu wanyonge na maskini siwezi kuwavunjia bila kuwalipa fidia mana serikali ndiyo ilizembea watu wakawekeza fedha zao hapo. Hajawahi kusema wala kuumizwa na uonevu wa watu zaidi ya kuwaumiza . Nyumba za serikali ziliuzwa zote kwa makada wa CCM kwa bei ya kupeana huku wakijua wazi kuwa Tanzania ni nchi ya KIJAMAA lakini hakuwahi kupinga huo uporaji wa Mali za umma uliofanywa na wanaCCM kwa uroho wa kumiliki Mali zote za nchi hii.

Hakawahi kufanya kama alivyofanya Mrema alipoipinga serikali kwenye Kashafa ya Chavda na nyingine ,akaamua kuipinga serikali na akafukuzwa uwaziri kwa kusimamia Haki. Mrema alipata umaarufu wa kweli pamoja na kukosa Urais kutokana na kizingiti cha Mabilionea wanaomiliki Mali zote za nchi hii na vyeo vyote na familia zao. Mrema alikua ni mzalendo wa kweli mtetezi wa wanyonge mana alijitoa mhanga kupoteza madaraka ili asimamie haki.

Hawa wengine ni wazalendo wa kupigania maisha yao kama unavyoshauri ili wapate maisha mazuri.

Tumshukuru Mungu kwa kuwaleta duniani watu wasioangalia maisha yao binafsi. Ingekua wote wana roho za ubinafsi utumwa na ukoloni mpaka Leo ungekuwa upo Duniani . Afrika kusini imepata Uhuru kwa sababu ya vijana waliokua wamejitolea kupigania Haki.

CCM inaongozwa na mabilionea waliotumia Fursa ya Kujiita wajamaa na kupora Mali zote za umma kupitia madaraka.
Nyumba zote za Osterbay. Masaki, Upanga , Na maeno yote muhimu kwenye miji yote iliporwa na Makada wa CCM wakiopo na waliopita . Walishirikiana kujilimbikizia mali kupitia madaraka.

Watu kama hao ambao kwao uongozi ni biashara inayowatajirisha sana huku wakiwa wanaweza kufanya wanachotaka kwa MTU yeyote bila kuulizwa na MTU yeyote usipokua MTU mmoja tu ambaye ni Rais ,kwa maana kwamba akikaa kimya ndio basi; kamwe huwezi kushindana nao bila kuwa na watu wanaoweza kujitolea na kukabilana nao .

WanaCCM wengi wanaogonbea mpaka Udiwani ni wale wenye utajiri mkubwa , wanachofanya ni kumwaga pesa na kuandaa vijana ili wafanye vurugu hata kuua watu na wakija polisi kuchunguza wanawahonga mapesa ili taarifa zibadilishwe ionekane kuwa hakuna jambo baya lililofanywa na WanaCCM hao hivyo panakua hakuna Kesi.

Uroho wa Makada wa CCM umezalisha taifa la watu waovu wasiojali uhai wa MTU mwingine asiye na faida ya kimadaraka kweo.
Ditopile marehemu alipiga MTU risasi hadharani lakini kutokana na ukada wake wa CCM kesi ilibadilika na kuwa ndogo kabisa na kuachiwa. Mungu ndiye aliyeamua mwenyewe kama atakavyoendekea kuamua dhidi ya madhalimu..

Haki itasimama hata kama Viongozi wa dini wote watanunuliwa na kusema kuwa wao ndio wanaoamua ipi ni haki na ipi ni dhuluma. Yani kwa sasa viongozi wa dini hawajui kutofautisha kati ya haki na wajibu wa serikali kujenga miundo mbinu kwa kodi za watu. Kwao miundo mbinu ni kazi ya MTU anayejitolea na sio Kuwa na Bunge linalopanga kuwa Pale pajengwe daraja na likajengwa na Bajeti ikatilewa bila kutesa na kuuana kwa ushabiki.

Yaani kwa sasa mpaka viongozi wa dini wanaongea kwa kuuma meno utafikiri kuna mtu amechukua sadaka yao akainunulia sigara. Mchungaji anaongea kwa hasira kabisa na kwa chuki utafikiri Naye ni mgombea kama Gwajima . Eti tumchgue Huyu ni mchaMungu na yule ni msaliti . Wamesahau kuwa Yesu alikataa kupewa Fahari za dunia kwa kupinga kumsujudia Shetani. Viongozi wa dini wameonyeshwa fahari ya dunia na kumsuhudia CCM mkuu.
 
Tukiwa na Taifa la watu kama wewe ni hatari sana.

Watawala ndio wanaotaka iwe hivyo lakini wao hawafanyi hivyo mana wanajua kuwa siasa ni sehemu ya maisha yao. CCM wengi wanajali familia zao na maisha yao ndio kama unavyosema na ndio maana haya maovu yote yanatokea...
Hujajibu lolote, mtu katoka katoro kapigwa jiwe chato akimshabikia chizi aliemtukana Mama magufuli.
Dawa itawaingia tu. Huwezi dharirisha wana chato then wakuache tu, mikutano yote kwanzia mbogwe amezõmewa. Haya akaseme kwa Robert.

Sent from my SM-M205F using JamiiForums mobile app
 
Huyu Lissu hana nia njema anataka kutoa watu sadaka ili mambo yake yaende .
 
aCHENI UJINGA WENU YOU MEAN MAGUFULI AKIFIKA SINGIDA APIGWE MAWE I HAD NEVER SEEN A STUPID OF THAT GRADE VIONGOZI WAKO KWNYE KAMPENI WANA ZUNGUKA NCHI NZIMA KUTANGAZA SERA ZAO WHAT WRONG WITH IT
Amewadharilisha sana watu wa Chato, ngoja afunzwe naye adabu toto tundu
 
aCHENI UJINGA WENU YOU MEAN MAGUFULI AKIFIKA SINGIDA APIGWE MAWE I HAD NEVER SEEN A STUPID OF THAT GRADE VIONGOZI WAKO KWNYE KAMPENI WANA ZUNGUKA NCHI NZIMA KUTANGAZA SERA ZAO WHAT WRONG WITH IT
Amewadharilisha sana watu wa Chato, ngoja afunzwe naye adabu toto tundu
Unga mkono uchawi kwa kuwa wewe ni mshirikina
unajua amejiona yeye ni yeye na vimaneno vyake vya ICC, ni bora wamemshusha na bado. Hapa JF mlikuwa mnashabikia kuwa JPM japendwi kwao ma ndo maana kaenda. Ilikuwa ni kuwadhihaki watu wa Chato. Wametenda kweli na wapongezwe kwa hilo
 
Tatizo wameyaponda sana maendeleo yaliyowekwa chato. Hii imeamsha hasira kwawakazi wa huko. Ulitarajia Lissu atapokelewa vizuri chato? Big NO!

Meza wembe...
 
Antipas ndio aina ya wapinzani nchi hii iliwahitaji kwa muda mrefu, Mwenyezi Mungu amjalie maisha awanyooshe hawa bata
 
Back
Top Bottom