Chato: Msanii wa nyimbo za asili aliyemtumkana Rais Samia ahukumiwa miaka 6 jela

Chato: Msanii wa nyimbo za asili aliyemtumkana Rais Samia ahukumiwa miaka 6 jela

Msanii wa Nyimbo za asili ya Kisukuma, Dawa Juma mkazi wa Kijiji cha Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita, amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya Tsh. Milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.

Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa mahakama ya wilaya Chato, Amalia Mushi, baada ya mshitakiwa kukiri kosa mbele ya mahakama hiyo.
This is a typical case ya this scenario Ukosekanaji wa Haki kwenye Mhimili wa Mahakama, kunaweza kuwa kunachangiwa na Majaji/Mahakimu wenye uwezo mdogo kubaini haki?

Any right thinking member of the society, akiyasoma tuu hayo mashairi, atagundua this man is insane!, huyu sio mtu wa kupelekwa jela, ni mtu wa kupimwa akili na kuanza matibabu!.

P
 
Mimi angekula 12..viboko sita wakati anaingia na sita wakati anatoka akamuoneshe mke wake..Mjinga kabisa huyu..Unasema huogopi kukamatwa wewe ni Nani..haya Sasa wakusaidie hao waliokutuma..
Rais ni mtu mkubwa sana kwenye nchi yetu..wa enzi zile walikufuru wakata kumfananisha na Mungu..wewe ni Nani umdhihaki rais wetu..Hakimu Mushi fanya marejeo ya hukumu..huyu Mjinga aongezewe adhabu ili iwe fundisho kwa vibaraka wengine.
Baadhi ya lugha alizotumia hazina staha kwa viongozi wa kitaifa!

Hata kama angekua na ujumbe wake angeufikisha kistaarabu na ukaeleweka!

Unapofanya ukosoaji kosoa mfumo usim-attack Samia Moja Kwa moja kosoa mfumo kama anachofanya ROMA
 
Wimbo mzuri shida maneno na jina sijui kwa nini hajatumia mafumbo wwimbo wote. Ameniboa huyu fala
 
wimbo umezungumzia mambo muhimu sana mfano kupanda kwa gharama za maisha ila hakukuwa na ulazima wa kutumia maneno kama msimbe sijui mvaa ushungi mara mapunye kwa kweli katukana na alistahili kuadhibiwa
Unajuaje kama kaimba mvaa ushungi wakati nyimbo ni ya kisukuma full.? Uhuru wa maoni uko wapi sasa hapo?

Halafu mmekaa kibwege mnasema Lissu alionewa kupigwa njugu! Alichofanya huyo raia kina tofauti gani na cha Lissu?
 
Haya ndio mambo ambayo vijana wengi hasa wanaojiita wasanaii wanafail, hivi huwezi kumkosoa kiongozi bila kutumia lugha kali kali?
 
Kuna namna bora ya kufikisha mawazo mbona Roma kaimba vizuri hakuna anayehangaika nae

Rais yoyote ni taasis na kiongozi wa nchi hapaswi kuogopwa lakini anapaswa kuheshimiwa huyu adhabu aliopewa ingepunguzwa sawa lakini hakuna sheria kandamizi hapo
Aliyeita raisi dikteta uchwara yeye alikuwa sahihi, yani hii nchi tupigwe nyuklia tu tuanze upya
 
Back
Top Bottom