imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Je ni tusi?Kuna lugha zingine katumia za dharau
Sijui mvaa ushungi nk
Hiyo siyo sawa
Hata roma aimbagi hivyo
Ova
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Je ni tusi?Kuna lugha zingine katumia za dharau
Sijui mvaa ushungi nk
Hiyo siyo sawa
Hata roma aimbagi hivyo
Ova
Roma anaingiaje hapo? Roma natukana? Anamtweza yeyote?Hapo roma anapewa onyo
Which gang?... from Charo? Kumbe the Gang is real?
Sukuma.Which gang?
sio kweli mbona we unamatusi sana vp huwa unamtukanaga na mama ako.hasa ukilewa we jamaa unakuwa wa hovyo sana juz nimekukuta unatoka kulewa upo chakar mkonon upo na chupa ya chibuku nakuuliza vp pale juu wamefunga, ukajibu ooh we mseengeee,. Kwakwel iliniuma sana leo nakujibu mseeengeee mwenyewe acha matusi au na mm nikufunge miak50Umeisha sema Kule ufaransa, siyo lazima tufanane, huku bongo wengempa hata mvua 30 ashike adabu. Mtu wahivyo anaweza hatamtukana mama yake.
hiyo adhabu ni ndogo, hivi alimlea huyo kijana anajisikaje kuwa na kiazi km hicho. Dogo ana chuki iliyopitiliza.Msanii wa Nyimbo za asili ya Kisukuma, Dawa Juma mkazi wa Kijiji cha Makurugusi wilayani Chato mkoani Geita, amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya Tsh. Milioni 10 baada ya kupatikana na hatia ya kumtukana rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa mahakama ya wilaya Chato, Amalia Mushi, baada ya mshitakiwa kukiri kosa mbele ya mahakama hiyo.
Awali mwendesha mashitaka wakili mwandamizi wa serikali, Robert Magige, ameiambia mahakama hiyo kuwa mshitakiwa alitunga wimbo wenye lengo la kumtukana matusi rais Samia Suluhu Hassan, licha ya kujua wazi kuwa kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Amesema akiwa na nia ovu alirekodi wimbo huo na kuusambaza kwenye mitandao ya kijamii ili kupeleka ujumbe wake kwa umma huku akijinadi kuwa haogopi kukamatwa.
Mwendesha mashitaka huyo, amesema kitendo cha kuchapisha taarifa za uongo na matusi kisha kuyasambaza kwenye mitandao ya kijamii (You tube) ni kinyume na kifungu cha 16 cha sheria ya makosa ya mtandao,sheria namba 14 ya mwaka 2015.
Hata hivyo mshitakiwa baada ya kusomewa mashitaka yanayo mkabili amekiri kutenda kosa hilo, licha ya kudai kuwa hakuwa na nia mbaya kwa kuwa alikusudia kuonyesha hali ilivyo mbaya kwa jamii baada ya bidhaa kupanda bei.
Aidha baada ya mshitakiwa kukiri kosa, wakiri wa serikali Magige ameiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine wenye lengo la kumtukana rais kutokana na sababu zao binafsi.
Akitoa hukumu, Hakimu wa mahakama hiyo, amedai kuwa kwa kuzingatia kuwa mshitakiwa hakuisumbua mahakama hiyo, kwa kukiri kosa kwa kinywa chake mwenyewe mahakama inamhukumu kifungo cha miaka sita jela au kulipa faini ya shilingi milioni 10.
Hata hivyo mshitakiwa amepelekwa gerezani kuanza kutumikia kifungo chake baada ya kushindwa kulipa faini iliyoelekezwa na mahakama hiyo
Chanzo: Dima Online
=======
Wimbo huo kwa tafsiri ya Kiswahili;
Dawa Dawa
Ubeti wa 1
Leo naongea na Rais mwenye ushungi, Kwanini huvui ushungi?
Au Kichwa chako kina mapunye? Tuambie
Bei ya mafuta ya Kula imepanda, sabuni za kufulia nazo zimepanda bei
Niuze Mkaa nikamatwe, Rais gani huyu Watanzania? Au kwa kuwa hatukumchagua?
Urais kaupata kwa kurithi, punguza bei ya sabuni
Bora Magufuli, alikuwa anatutetea Wanyonge
Tunaomba Rais upunguze bei ya mafuta tuanze hata kununua ya Tsh 100/= na sabuni irudi kwenye bei yake ya Tsh. 300/=
Mimi naitwa Dawa, siogopi kumsema Rais
We Rais wetu ni Mshamba, mwaka kesho hatukuchagui
Umedharauliwa hadi na wanawake kwa sababu umepandisha bei ya bidhaa
Nimeona pia kwa vijana, tusikae tu vijiweni, tukubali kushinda mashambani, tusiombe ombe misaada
Urithi wa mashamba utaendelea kutumaliza
Ubeti wa 2
Muhudumu tupe pombe, pombe pombe bia tamu, wanawake ni watamu, yaani tamu tamu tamuuu
Mke wangu tukilala, yaani nipe ile tamu
Sasa narudi kwenu wasanii, mnaojiita wasanii wakubwa
Mnatuona sisi kama wadogo kama sio wasanii vile
Eleweni sasa kwamba na sisi ni watu, ipo siku tutajulikana pia
Mnajidai sana kwa kuwa ninyi ni wasanii wakubwa, tutambueni na sisi
Bei ya mafuta ya kula imepanda, sabuni za kufulia nazo zimepanda bei
Niuze mkaa nikamatwe, Rais gani huyu Watanzania? Au kwa kuwa hatukumchagua?
Urais kaupata kwa kurithi, punguza bei ya sabuni
Bora Magufuli, alikuwa anatutetea Wanyonge
Ubeti wa 3
Mimi nimeanza kuja kitofauti, wala msiulize huyu anaimbaje
Wengine wanahoji, hivi huyu dawa ana akili kweli?
Mi nawajibu sina akili, nina nyimbo tu
Chuchumaa chuchumaa
Halafu wasanii wengine wanashinda siku nzima pasipo hata kusikilizwa wimbo mmoja, lakini kazi yao kubwa kujisifu
Wasanii imbeni nyimbo za kuelimisha
Msiwe kama Msanii Madaso wa Chato anayenuka, kila alikoenda kuimba alikuwa anaiba wake za watu,
Inakuwaje watu wanakushabikia lakini wewe unaiba wake zao?
Ndio maana hata usanii wake umekufa, mimi namueleza ukweli
Sasa tambueni dawa kali nimeanza kuimba japo sikuwa msanii mwanzo
Mashabiki wangu endeeleni kunisikiliza mimi msanii wenu dawa
Nipo tayari kuwatetea ndugu zangu maana mnahangaika mno
Ubeti wa 4
Leo nimekuja kuzungumza na Rais Samia, huyo mwenye ushungi
Jamani ndugu zangu tunateswa mno, watu wanaokata mkaa wanakamatwa ovyo mno
Ukiwaza hao askari wanaowakatama wanaupeleka wapi huo mkaa, ni uonevu tu
Nimechunguza nikabaini na wao huwa wanaenda kuuza huo mkaa
Sasa huo sio uonevu?
Wewe Rais mwenye mashavu yako wewe
Niite dawa kali mimi huwa situkani mtu asiye na hatia
Naongea mambo ya kweli
Simuogopi Rais, kama mnaweza njooni mnikamate lakini tayari nimeshazungumza ukweli
Dawa kali mwenyewe mimi ni jeshi, tembea
Ubeti wa 5
Maisha yamekuwa magumu mno, sisi tusio na kazi tulidhani kaja mwanamke atatutetea
Kumbe ni ovyo tu, msimbe huyu
Magufuli alipokufa haikupita hata wiki, ndege 3 zilipotea
Ndege hizo ilitambulika kazipoteza Mkuu wa Majeshi
Ulitaka uzipeleke wapi, wewe mvaa ushungi nakuuliza, nijibu
Yaani tangu uingie madarakani hata mwaka haujamaliza unaiba ndege?
Ulikuwa unazipeleka wapi? Au hakuwahi kupanda ndege kabla?
Nipo radhi kutetea raia wanaoteseka, kuliko kumtetea Rais mwenye ushungi anayetutesa vibaya
Hela zimekuwa ngumu mpaka dada zetu wanajiuza
Wanajiuza sababu ya ugumu wa Maisha, kwani kama hela zinamwagika nani atajiuza?
Huu ndo wimbo umempeleka Jela
hiyo katiba mtungie mamako we nguruwe. Katiba mpya huna hata haya? Kwa hiyo katiba itakuwa ya kumtukana Rais? Hiyo itakuwa ya kumtukana mamako itungeni hapo kwenu.Kule ufaransa jamaa alimtandika macron kofi la aina ya UTANITAMBUA na akafungwa miaka 3
nyie tusi hilo miaka 6
KUNA HAJA YA KATIBA MPYA KUONDOA SHERIA KANDAMIZI, RAISI WA TANZANIA NI MUNGU WA PILI KWA KATIBA HII
nawaza kama Jamaa angemtandika kofi samia si angeuuawa
Kwahiyo Makamanda ndo wakusapoti matusi ya kiuwendawazim?Kutukana kosa lake ni FAINI
Ukishindwa FAINI ndiyo unaenda jela.
Huyo faini ni Milion 10,akipata siku yyt anatoka.
Makamanda mchangieni mtu wenu atoke.
Kule ufaransa jamaa alimtandika macron kofi la aina ya UTANITAMBUA na akafungwa miaka 3
nyie tusi hilo miaka 6
KUNA HAJA YA KATIBA MPYA KUONDOA SHERIA KANDAMIZI, RAISI WA TANZANIA NI MUNGU WA PILI KWA KATIBA HII
nawaza kama Jamaa angemtandika kofi samia si angeuuawa
Hukumu ipo sawa tu mbona ata Musiba alihukumiwa kumlipa Membe fidia ya Shilingi Bilioni 9 wakati katika ukoo wao wote hawajawahi kumiliki pesa kama iyo.Kule ufaransa jamaa alimtandika macron kofi la aina ya UTANITAMBUA na akafungwa miaka 3
nyie tusi hilo miaka 6
KUNA HAJA YA KATIBA MPYA KUONDOA SHERIA KANDAMIZI, RAISI WA TANZANIA NI MUNGU WA PILI KWA KATIBA HII
nawaza kama Jamaa angemtandika kofi samia si angeuuawa
Alichokiri👆🏾Wengine wanahoji, hivi huyu dawa ana akili kweli?
Mi nawajibu sina akili
Lakini kweli hakuogopa maana amekiri kufanya kosa hilo. Hongera zake kwa kuwa mkweli.