Chato: Msanii wa nyimbo za asili aliyemtumkana Rais Samia ahukumiwa miaka 6 jela

Chato: Msanii wa nyimbo za asili aliyemtumkana Rais Samia ahukumiwa miaka 6 jela

Mkuu Lissu kupigwa risasi ni tofauti na kufungwa jela. Mbona Sugu alifungwa kwa kumtukana JPM pia Mbowe na Matiko walifungwa miezi 7 kwa uchochezi!! Ila sio RISASI. Yaani kumuua mtu kisa kakutukana ni kuvuka mipaka, ila Lissu angefungwa tungeona kawaida maana tulizoea kila siku wanamfungulia kesi mahakamani.
Et ungeona kawaida basi hata huko kupigana risasi mngekuja kuzoea pia na kuona kawaida, nchi hii mnazoea vitu vya ajabu sana ndio maana nasema hata aina ya uchaguzi wa 2020 ambao watu huulalamikia wangekuja kuuzoea tu kama wanavyokiri kuzoea wizi wa kura wa ccm uliyopo miaka yote.
 
Pole Mkuu ilo lipo juu ya upeo wako.
Upeo unaosema ambao ndugu unao ndiyo huo huo wa kukaririshwa na makaratasi. Kwakutumia utaalaam na utashi wa akili lazma ilo swala lingekua na matokeo tofauti. Mfano,mtu akiuuliza je,msanii katika mambo yote aliosema msanii je,kuna uongo tu?
 
Hakika inanpa furaha sana Watanganyika wa kisukuma wakinyooshwa kwa ushamba wao
 
Et ungeona kawaida basi hata huko kupigana risasi mngekuja kuzoea pia na kuona kawaida, nchi hii mnazoea vitu vya ajabu sana ndio maana nasema hata aina ya uchaguzi wa 2020 ambao watu huulalamikia wangekuja kuuzoea tu kama wanavyokiri kuzoea wizi wa kura wa ccm uliyopo miaka yote.
Kufungwa kwa kesi za kubambikiza ni prevalent Tanzania lakini kumiminiana risasi kisa siasa hatukuwahi kuyaona. Huwezi linganisha hayo mawili kabisa. Una justify kuuwana kisa kumkosoa Rais? Are you serious
 
Kufungwa kwa kesi za kubambikiza ni prevalent Tanzania lakini kumiminiana risasi kisa siasa hatukuwahi kuyaona. Huwezi linganisha hayo mawili kabisa. Una justify kuuwana kisa kumkosoa Rais? Are you serious
Ndio nakwambia kwamba huko kufungana kwa kesi za kubambikiana sio jambo la kawaida kisa mmelizowea, wengine wanaweza kuwashangaa et watanzania wamezoea kufungana kwa kesi za kubambikiana kwamba kwao ni kawaida. Sasa hayo ya kupigana risasi kisa siasa nayo mngeyazoea tu maana hakuna hoja yeyote ya msingi ya kuzoea hayo mliyoyazoea hivi sasa.
 
Intelligence Justice;
Hii ndiyo defamation to destroy other people's reputation na sheria ile uliyoitupia inamhusu huyu..

Na kwa kweli huyu anastahili Kwa sababu si tu amedhalilisha Imani na utu wa mtu mwingine Kwa maneno yake na kuusambaza katika media bali anasema mwenyewe kwenye maneno yake hayohayo kuwa haogopi kukamatwa Kwa kumtukana mtu mwingine...

Lakini wale waandishi wa kitabu cha "I AM THE STATE" kumhusu aliyekuwa Rais wa Tanzania (2015 - 2021) hayati John P. Magufuli hiyo si defamation na ukienda mahakamani utapata taabu sana kuthibitisha unless otherwise angekuwepo John P. Magufuli mwenyewe na zile mahakama zake na mahakimu wake wa kimkakati..

Hao wameandika kitabu kuhusu matendo ya uongozi wa aliyekuwa Rais wao. Ni mambo ya kweli, hakuna uongo na hayo kamwe hayawezi kuwa matusi..

Tatizo ni kuwa, wapenzi wa John P. Magufuli wamechukia kwa sababu upande wasioutaka (negative side) wa mtu wao umekuwa exposed na kwa tafsiri yao isiyoweza kusimama mbele ya sheria na haki, eti hayo ni matusi yanadhalilisha na kuvunja heshima na utu wa mtu wao na mkakimbilia kujificha kwenye sheria inayovuja isiyoweza kuwakinga mnapoloa na mvua ya mawe...!!.

Sikiliza ndugu @Intelligence Justice, mtu yeyote (ukiwemo wewe na hata mimi) aweza kujivunjia heshima na kuharibu utu wake mwenyewe kwa maneno na matendo yake. Na hayo matendo na maneno yake ndiyo huambatana nayo kokote aendako hata kama ni kaburini kama huyo aliyekuwa Rais wenu..!!

Poleni sana wana Chato.
Nyie watu wamchongo mna muda mfupi sana wa kutema uozo uliowajaa lakini kuna siku mtaukana hadharani.
 
Huyu ameyataka mwenyewe.

Kumwita Rais ni 'ovyo', eti Rais ni 'msimbe', eti Rais ana 'mapunye kichwani', eti "hata mwaka haujaisha Rais ameiba ndege", eti Rais "alikuwa hajawahi kupanda ndege"hivi kulikuwa na ulazima wa kuyasema hayo ya upuuzi, kejeli, matusi, na uwong ili kuufikisha ujumbe wake?

Huyu kijana amejosa akili, amekosa staha, amekosa heshima, amekosa ustaarabu. Hivi kwa umri wa Mama Samia, hata asingekuwa Rais, unaweza kumtolea maneno kama hayo?

Kwanza huyu kawatusi akina mama wote wanaovaa ushungi. Kwake yeye kila anayevaa ushungi ana mapunye kichwani. Hivi kuna ndege iliyoibuwa na Rais? Hivi kweli Rais Samia kabla ya kuwa makamu wa Rais, alikuwa hajawahi kupanda ndege? Kumwita Rais ni ovyo, lazima uwe na uthibitisho, ni ovyo katika nini. Huko ambako wafanyakazi wanashi dwa hata kuwalipa mishahara wafanyakazi wa umma, hatujasikia watu wakisema Rais ni ovyo.
Jela kaitaka mwenyewe

Ova
 
Wakisema wamchangie wanachato pekee anatoka tena asubuhi tu
 
Back
Top Bottom