CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Takwimu mpya zinaonyesha kwamba kwa mara ya kwanza tangu janga hili la korona lianze duniani, Marekani imeripoti vifo zaidi ya 2,000 kwa siku moja tu (ndani ya saa 24 wamekufa watu zaidi ya 2,000 kwa korona)!

Nimeona nikazie jibu lako kwa huyo member wa JF ambae hadi sasa hivi hajui sababu ya kwanini Nchi kama Marekani, Italia na Uispania watu wanakufa kwa wingi pamoja na kuwepo hizo lockdowns. Ni aibu sana kwa mtu mzima kuuliza swali la namna hiyo humu JF.
mkuu habari ya miaka
 
Mmmmmmmmmmmmmmm! Ila tutataka awe mfano wa kuigwa aje DSM na aendelee kwenye mikusanyiko huku akipiga kazi.

Ila tukumbuke maneno ya Rais mstaafu "Changanya na zako"
 
Yuko sahihi! Tena sahihi sana!

Mbona kila siku mnaambukizana ukimwi lakini hamjataka mipaka ifungwe?

Kufanya ufuska hamuogopi, lakini haka ka corona mnajifanya mnataka kufungiwa kwenye hayo mageto yenu machafu!

Kwa siku watu wangapi wanakufa kwa kansa, malaria, kisukari, homa ya ini, ukimwi na magonjwa ya ngono? Mbona mipaka haijafungwa?

Watu wachape kazi! Kama kufa basi tutakufa tukiwa tunafanya kazi! Hatuwezi kuwa watumwa wa corona!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika Hali ya Kawaida Tujihadhari wenyewe..ukifa utakufa wewe mwenyewe wala hakuna Rais atakuzuia kufa nae ni mtu kama wewe tu.

Chukua tahadhari kubwa wewe mwenyewe..jilinde na watu wako acha kukimbia kushoto kulia halafu unasema ooh hatujaambiwa lockdown.

Lockdown nyie mnaijua..Funga kila kitu hapa mtakufa kama njiwa jike baadae tena mtageuka kusema ooh Hii serikali mbaya inaua watu ndani.
Jilinde Mwenyewe usiende kwenye Ma bar jihadhari na mikusanyiko.
 
Tatizo uchaguzi

Sifa nyingine hazifai , mwanzo aliaanza vizuri ila sasa naona anaporeza network.

Ummy amebaki pekee yake maskini hajui nini afanye, anajitahidi kuelekeza kuwa kuna maambukizi ya ndani lakini mtoto wa chato hana habari analazikisha watu waende makanisani.

Kwa taarifa yake makapuni binafsi karibia yote yamefunga ofisi, wananchi hawatoki kwa sababu ijaonekana mzee anasililiza bbc tuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tabutupu,
Tunasubiri week mbili tukishaanza Kufa ndio tutajua kuwa tutafunga au hatutafunga. Raha sana
 

Attachments

  • IMG-20200411-WA0010.jpg
    IMG-20200411-WA0010.jpg
    50.3 KB · Views: 1
Is there any production which is done by students? Acha watoto wakae watulie majumbani, acha kumpa Rais sifa za kijinga, by the way vita dhidi ya corona hailengi kuwakomoa Chadema na kuwanufaisha CCM,

Ugonjwa uko na unajua, kuruhusu watoto kurudi shule ni sawa na kuruka mkojo na kujanyaga mavi, mkuu tafakari ikiwa serikali ilifunga shule na vyuo tukiwa na mgonjwa mmoja, vipi Leo ambapo tuna wagonjwa 30+ itakuwa ni akili kweli?

Tatu kuna maeneo yana maambukizi mengi sana mfano Dar, hebu niambie watoto waanze kurudi shuleni wengine watoke Dar waende mkoani na wamikoani waende Dar si itakuwa balaa sana

Huu ugonjwa umewafanya watu kuwa wajuaji, by the way nimegundua kuwa wanaong'ang'ana shule zifunguliwe ni wale wasio na watoto au wale wako private schools, si kwamba wana waonea huruma watoto kukosoa elimu la hasha wana masilahi binafsi tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Makanisa, Miskiti yote ingefungwa. Ningepiga marufuku abilia kuingia na kutoka Dar, Mipaka yote ingefungwa isipokuwa wanaoleta chakula, dawa na bidhaa muhimu, Kumbi zote za starehe zingefungwa kila mlevi anunue pombe dukani akanywe kwake.

Mishahara yote ya umma ambayo ni kuanzia milion 3 ingekatwa 50% ili kununua chakula kwa watu masikini.
mkuu.. nini maana ya kufunga mipaka? hata hao wanaoleta dawa na chakula pia wasingeweza kuingia kama mipaka ingefungwa...!
 
Huyu ni wa kumpuuza tu hana hata chembe ya sympathy !what a disgrace kind of a president!

Hebu elezea wewe ndo ungekua rais ungekabiliana vipi na maambukizi na effects za huu ugonjwa. Usikae kumtukana tu, weka points zako tuzi challange labda utaweza kuona ujinga wako upo wapi na ujirekebishe kama akili unayo au tusaidie kuuona ujinga wa rais


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Muda bado wa kuruhusu vyuo na shule kufunnguliwa tusubiri kwanza tuone halihii ya maambukizi ya sisi kwa sisi ikoje?na viongozi waendelee kutoa somo la kuepuka misongamano hasa katika misiba angalao watu wawe wasiozidi 20 na wasikae kwa zaidi ya siku 2 baada ya maziko

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamani naomba wachambuzi na wajuvi wa mambo mnisaidie. Tatizo la Corona ni kubwa na kiukweli kama unaakili timamu, linatisha. Sasa, kwanini unapofika wakati wa kuchukua hatua hasa za kuzuiya mikusanyiko, Mzee wa kaya anaruka wakati alisema kwa nyakati tofautitofauti kwamba tuko vizuri sana kiuchumi?

Hii Coronio si masihara, huko kwa Wenzetu inachukua hadi WAKUBWA wa nchi, kuna Maeneo Mengine imeondoka na Maraisi wastaafu, sasa kwanini hapa kwetu Mzee lockdown anaiogopa kama anavyoogopa KATIBA Mpya?.
 
Someni andiko lote la mleta mada kisha tafakari nia ya mleta mada. Hapo utagundua kwamba mleta mada anatoa ujumbe tofauti. Lakini ukisoma tu kichwa cha habari hautoelewa nia ya muandishi.
 
Back
Top Bottom