CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Wahenga walisema; 'mtoto wa moto ni majivu'. mwenye akili ajilinde, anaetaka kukutana na kifo awasikilize wanasiasa.
 
Bams,
Magu Hana nianjema Kwa raia wa nchi hii. Anataka watu wapate tabu Kwa Sera take ya "Expect No Mercy"
 
Azarel, Mkuu hilo wala halina ubishi. Mzee anapambania mapato ya serikali kuliko afya ya wananchi wake. Kwanini vyuo na shule vilifungwa? Jibu ni rahisi tu "kwakuwa kule hakuna uzalishaji bali matumizi pekee hasa kwenye shule za serikali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chibudee,

Hongera rais JPM kwa uamuzi wa busara, wale waliokimbilia kuweka lock down sasa wanahaha wanataka kufungua lock down maana hali ya uchumi ni mbaya. Sasa wengi hawana chakula na matatizo yanaendelea.

Ushauri wa kuosha mikono pasipo kushika pua macho na mdomo wakati mikono yako sio safi ndio canzo kikubwa kueneza haka kaugonjwa. Jihadhari na jikinge pasipo kuwaambukiza watu wengine. Tuige mfano wa Sweden, Big up Amiri Jeshi mkuu.

JPM hapa Kazi tu!

 
Ndio jukumu mojawapo la serikali kama imejipanga.
Hivi kuna serikali itaweza kuwapa tu hela wananchi wake bila yenyewe kuzalisha kitu?.
unadhani serikali hela wanaokota au wanazichimba?..
 
Mkuu kwani majirani wakifunga mipaka na sisi Tanzania hatujafunga mipaka ni faida gani tutapata?
Tunazidi kupata hasara kwa kwa kujiweka katika risk kubwa ya maambukizi toka ndani na nje ya nchi kitu ambacho kitapelekea kupoteza maisha ya watu wenge zaidi.

Pia kwa kuwa wenzetu wamechukuwa hatua mapema, wakati wao wanapokuwa hawana maambukizi sisi huenda tukawa na hali mbaya zaidi; watafungua mipaka yao na kufanya biashara baina yao, sisi tutaachwa kisiwa maana hakuna taifa litakalokubali kuhatarisha afya za RAIA wake.
 
Hivi kuna serikali itaweza kuwapa tu hela wananchi wake bila yenyewe kuzalisha kitu?.
unadhani serikali hela wanaokota au wanazichimba?..
Ndio maana nimesema kama imejipanga vinginevyo haitaweza.
 
Naomba kuuliza Je nchi zote zinazotuzunguuka zimeshafunga mipaka?
Je zote zimetangaza complete lockdown?
Je kwa nchi za jumuia ya Africa Mashariki hali ikoje?
Je zote zimefunga mipaka?
Je zote zimetangaziwa complete lockdown?


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahaaa..naona mzee anataka kutumia fursa ya wengine kufunga mipaka ili awapiku! Tuombe Mungu yasitukute km ya huko ulaya na marekani maana tutalia na kusaga meno..tutatamani tungefunga mipaka hata mwaka mmoja ila haitawezekana tena!!
 
Zote zina lockdown mkuu.Jamaa yetu anasema tupige kazi ili wakimaliza kucoronwa tuwapige pesa.TBC wameanza kupiga kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…