CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Niambie chato kaendalini.likizo yake ilishakwisha aliludi kwenye majukumu yake,kuludi tu ndio sekeseke likaanza la corona akapiga ndefu dar to dom.dom kalaa juu ya mawe palee kaona wanafki wengi watamletea corona akapiga ndefu mpaka chato,sasa katulia anasoma mchezo.
kwahiyo kama mchezaji basi yeye iniesta ananyumbulika tu
 
Kwa sasa bado hatujafikia that state of emergency kwa hiyo hakuna ulazima wa kufanya hivyo...

Ila tunapofikia huko, hatutakua na budi kufanya total lockdown...



Cc: mahondaw
 
Nasikia kasema "Chapeni kazi" Na yeye tunamtaka arudi Dar ili afanye mambo muhimu ya kitaifa!
Arudi Dar? Bado unamawazo ya zama zile, mambo yote kwa sasa ni Dom!
 
Bams,
Mbona tumekwisha amua!? Hatupiti mtoni wala nchi kavu, tunapita angani😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂!
 
Sawasawa na mkifa sijui nchi gani itawategemea...inategemewa na nini maana nyinyi wenyewe tegemezi.
Chuki hata baada ya kufa na kufufuka Yesu, bado umeikumbatia! Ukombozi upi sasa utakuokoa? wa Mbowe!?
 
Mkuu fujo itasababishwa na Nini?
wewe ni ufipa Chadema nyie wote ni pro lockdown sikujibu sababu unaitwa sijijui na hujijui kweli, au ngoja nikujibu,

kati yetu wabongo kuna wengi wetu mamilioni ‘of the poorest among the poor’ na ni vibarua lazima tutoke tukauze kahawa mtaani ndo familia ipate msosi sasa ukitufungia ndani siku mbili tu tutakufa njaa sababu nchi yetu maskini hatuna uhakika kama serikali itatulisha six months at least na kama isipotulisha na njaa ikizidi tutatoka nje kibishi kama huko Zimbabwe maana njaa ni kali kuliko Corona na tukitoka nje kibabe manjagu na wajeda wataanza kutushughulikia kwa kuvunja sheria ya lockdown nasi tutajaribu kuwaelewesha!!

hapo watu wasio na kitu hawana cha kupoteza kukiwa na vurugu watavunja maduka ya watu matajiri waibe na wapinga muungano wataanzisha fujo ili kuwatoa jela mesheikh wa uamsho! nanyi Ufipa mtapata ajenda ya uchaguzi kuwa sirikali inaonea wanyonge kwa kukurupuka kuweka watu maskini ndani na kuwanyima msosi na kupiga wavunja lockdown! uzoefu wa Rwanda na Kenya kuna taarifa kuna watu wameshaaga dunia katika ndondi za wavunja lockdown na askari wababe!

vurugu hamna iwapo nchi yetu ina pesa ya kulisha 50m people tukienda lockdown na lockdown huwezi kupanga iishe lini inaweza kuchukua six months hata huko ulaya kila siku wanaongeza siku tu sababu haijulikani lini maambukizi yataisha!!!

ufipa hamna agenda ya uchaguzi hadi sasa!
 
Huo
Makanisa, Miskiti yote ingefungwa. Ningepiga marufuku abilia kuingia na kutoka Dar, Mipaka yote ingefungwa isipokuwa wanaoleta chakula, dawa na bidhaa muhimu, Kumbi zote za starehe zingefungwa kila mlevi anunue pombe dukani akanywe kwake.

Mishahara yote ya umma ambayo ni kuanzia milion 3 ingekatwa 50% ili kununua chakula kwa watu masikini.
Huo nao ni udikteta!
Huwezi nikata mshahara wangu bila ridhaa yangu kwa sababu yoyote ile isipokuwa kama nadaiwa!
Kama ww ndio ungekuwa Magu naomba tungekuwa na hali mbaya sana!
 
Marry Ngowi,
Umejitahidi kumuelewesha, ila sina uhakika kama kakuelewa! Tunamshukuru Mungu kwa kutupa rais anayecheza kama Pele, Ronardo, Gaucho, na Mess kwa pamoja! Mungu hakika anaipenda Tz na watu wake! Hakika maharamia wasio na agenda wala sera mwaka huu watatapatapa saaana bila mafanikio! Hakutakua na kufungiana Tz, na tutatoboa salama, Mungu yupo!
 
Marry Ngowi,
Nakuelewa mkuu,Ila kitu pekee ambacho hujui pamoja wewe kuwa mwanaccm na mzalendo wa ukweli kwa mujubu wa definition ya uzalendo wa awamu hii ya Magufuli ni kuwa serikali yetu ina pesa za kuendesha nchi kwa miezi sita kwa mujibu wa magufuli.kumbuka kuendesha nchi ni gharama kubwa kuliko kuwasustain watu wachache watakaoshindwa kujisustain wakati wa lockdown.

Lakini pia tukiacha Mambo yaendelea Kama yalivyo ni kwamba tutakaa na ugonjwa huu muda mrefu sana,uchumi utashuka sana na wakati huo wabangaizaji ndo watakufa zaidi kwa kuwa kila mtu atakuwa amechoka kimwili na kifedha so no kusaidia na hasara kwa serikali utakuwa kubwa mno kuliko ingeamua kusaidia wajiojiweza sasa.

mbaya zaidi tutakuwa na wagonjwa wengi na while huduma zikiwa kiduchu.hivyo hayo yote unayoyaongea ni kwa sababu ya uanaccm wako unaokuzuia kuona mbali
 
Mratibu
Tafadhali zuia utumiaji matusi. Sisitiza lugha ya kiistaarabu na utumiaji wa hoja na mantiki. Pia zuia itikadi za chama katika suala la Korona - Dont Politisize Pandemic Please !!!
 
Upendo huu wa kijinga hata kwenye maandiko matakatifu haupo, " Mpende jirani yako kama unavyojipenda mwenyewe" sio mpende jirani yako kuliko unavyojipenda mwenywe.

Yani unahofia matako ya jirani yako yaliyofunikwa kuliko matako yako yaliyowazi!! Jirani ameshajifungia (lockdown) sisi hakuna lockdown tutawatetea waliojifungia? Kwani nchi waliojifungia na kufunga mipaka yao hawana nchi jirani?

Mmeshupaa na kunawa mikono kwani hawa waliokufa hapa kwetu na Wazungu huko Italy, Spain na USA hawana maji ya kunawa yanayotiriri au Sanitizer!!! Duh ila matanzania majinga!
 
Acha tujipe muda,, ila hili janga linahitaji akili kubwa sana kwenda nalo sawa,, tofauti na hivyo ni majanga tunayatafuta..
 
Chibudee, Ameeleweka vema
Huwezi mlazimisha mtu ajifungie ndani kwa kuogopa corona ilhali kula yake inategemea shughuli zake za kila siku.

Mi nafikiri lile wazo la kuwekea lockdown Dar peke yake ni jema.
Pia serikali itoe utaratibu wa kupunguza idadi ya mahudhurio ya wafanya kazi kwa siku,

kwa mfano;-
tuchukue halmashauri ina wafanyakazi 50,, 25 wanaweza pangwa kufanya kazi wiki hii ,,,wakati wenzao 25 wamejifungia majumbani ,,, kisha wiki ijayo waliokuwa nyumbani wanakuja kazini na wenzao wakienda kujifungia,,, hii ikifanyika nchi nzima itapunguza sana msongamano mijini na hivyo kupunguza chances za maambukizi mapya.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom