CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Hivi unajua Italy inaongoza kwa ushoga duniania ikifuatiwa na USA?
 
Akili za kuambiwa changanya na zako! Jilinde wewe na familia yako. Jifungie kama unaweza. Usitoke au kushiriki nikuasnyiko kama sio lazima (niongeze hapa.....salini majumbani mwenu, Mungu yupo popote!) Usisubiri wanasiasa wakwambie jifungie. Wanasiasa muda wote wanawaza kura (votes) tu. Trust no body.
 
Ufunge usifunge wao wamefunga mipaka yao sasa sijui utapenyaje!
 
Tanzania haitokaa ipate rais mzuri kama Dr.Magufuli nakumbuka mara ya mwisho Tanzania kupata kiongozi mzuri na bora kabisa ilikuwa 5 November 1985 yaani takribani kama miaka 40 iliyopita.

Binafsi naamini siku CCM ikiondoka madarakani itakuwa ndio mwisho wa dunia,maana sidhani kama dunia ina zaidi ya miaka 40 tena.

Mr President wetu amekuwa na huruma sana na wananchi wa chini na wanyonge wenye kuunga unga maisha ,ndio maana kaona bora kusiwe na lockdown maana wengine tungekuwa tunagombea uji kwenye mbavu za mbwa zetu huku Tandale wakati wenzetu wa Masaki wangekuwa wanafanya stay home challenge huku waki ji selfisha na makuku ya KFC pale .
 
wewe na mwezio Kawe Alumni. ni mfano bora kwanini kuna baadhi ya nchi mtu akitoa maoni yake anauwawa
 
Mkuu naelewa,Ila ccm huwa inakawaida ya kuwanyanganya watu akili zao.Ashukuriwe Mungu wa Mbinguni Kama wamekurudishia mkuu
Hakuna mwenye uwezo wa kumnyanganya mtu akili.

Maana kama ni hivyo kaka Mbowe amewanyanganya wengi sana, huu mwaka wa 16 yupo na cheo chake pale ufipa.
 
Hakuna mwenye uwezo wa kumnyanganya mtu akili.

Maana kama ni hivyo kaka Mbowe amewanyanganya wengi sana, huu mwaka wa 16 yupo na cheo chake pale ufipa.
Unajua kikundi chake wamekubalina Nini? Magufuli yupo madarakani kwa kura 8 m watanzania tupo 60m.Je alichaguliwa kweli na watanzania?
 
Anzisha uzi mimi nitauchangia.
Vipi mbona unakwepa tena,wewe si ndo umeleta Mambo ya kina Mbowe? Au Mbowe na ccm Nani kaka madarakani muda mrefu? Na still wadanganyika bado ni wabangaizaji kushinda hata warundi na wanyarwanda waliokuwa kwenye Vita miaka yote
 
CCM kwa miaka 16 aliyokaa Mbowe madarakani wamekuwepp wenyeviti wawili.

Hakuna nchi ambayo kila raia maisha yake yanakuwa mazuri eti kwa sababu ya chama kimoja cha sasa, ni juhudi yako binafsi ya kusoma bila kuchoka na kuwa mbunifu.

Tabora peke yake ni kubwa kuliko Rwanda, Morogoro ni kubwa kuliko Burundi. Kushinda humu jukwaani kulalamika sio sawa na kupambana na changamoto za kuibadili Tanzania kiuchumi.
 
Kwa hiyo kazi ya ccm na serikali yake ni nini sasa? Kufanya ufisadi na kugawana madaraka?
 
Phillipo Bukililo,
Vipi hakuna nchi kubwa duniani kuliko Tanzania na maisha yao yako vizuri,Kama issue ni ukubwa? Lakini pia sisi tupo vizuri kuliko Malawi ingawa Malawi ni sawa na Morogoro ,jr hapo unasemaje?
 
Viva JPM kwa mawazo yako mazuri na ya kutia nia. Neno kubwa kuliko yote; Tumuombe Mungu. Ametuleta duniani, anajua kutulinda. Ila tumwombe ulinzi naye atatupa ulinzi mathubuti. Hakika, tukivuka hapa, Tz itakuwa nchi bora duniani
 
Vipi hakuna nchi kubwa duniani kuliko Tanzania na maisha yao yako vizuri,Kama issue ni ukubwa? Lakini pia sisi tupo vizuri kuliko Malawi ingawa Malawi ni sawa na Morogoro ,jr hapo unasemaje?

Sisi tupo vizuri mkuu, kama akili yako umeiandaa kuona mabaya tu hakuna wa kukulazimisha kubadili mtazamo wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…