CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

1587449370724.png

Kielelezo hiki kinaonyesha baadhi ya hatua za kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona
()
nimekisoma na kubaini kuwa serikali yetu imetupitisha kwenye njia hii lakini bado watu wanaona haikufanya sawa. Tatizo liko wapi? Je in sayansi ipi inatumika kuikosoa serikali?
 
Moja kwa moja twende kwenye mada husika. Naona raia wengi wakitoa ushauri kwa serikali tena shauri nyingi zikiwa ni kuzuia watu wasitoke ndani sababu ya ugonjwa huu wa Corona.

Hivi kati ya Corona na Njaa kipi ni hatari zaidi.? Hilo ni swali fikirisha sana, binafsi naona njaa ndio hatari tena hatari zaidi ya moto. Hakuna kitu kinaua kwa asilimia kubwa hapa duniani kama njaa, njaa ndio huua mamilioni ya watu kila mwaka. Hakuna ugonjwa wowote unaweza fikia kitu inaitwa njaa. Hii Corona sidhani kama imeua ata watu 500k mpaka sasa. Sikatai na wala sipingi madhara ni makubwa kiujumla katika maisha yetu. Ila huwezi sema Corona ni hatari kuliko njaa.

Nyie mnao sema watu wafungiwe wasitoke ndani kisa Corona mnataka watu wafie ndani kwa njaa kisa Corona.? Mtambue kuwa kuna baadhi ya watu mpaka watoke ndio wapate kula. Tuseme Tanzania ina watu zaidi ya millioni 50 kama wanavyo tuambia wao, let say katika hao millioni 50 nusu yake ndio matajiri wanaojiweza sasa mnataka mzuie watu millioni 25 wasitoke ndani kutafuta liziki wakae ndani tu kisha wafe.! Faida yake ni nn hapo.?

Cha msingi watu wawe makini sana na huu ugonjwa, watu tufuate ushauri unaotolewa na wizara ya afya. Cha kuongezea katika familia watoke watu wanao enda kutafuta tu sio unatoka toka tu bila sababu za msingi usichukulie poa huu ugonjwa ni hatari lakini si hatari kama njaa. Watu tuepuke misongamano, watu tuvae barakoa hii usichukulie poa vaa barakoa huku ukipambana katika shughuli zako, watu tunawe mikono mara kwa mara maana tunashika sehemu mbalimbali kila mara ikibidi watu waoge mara kwa mara.
 
Waingereza husema huwezi kuila keki yako na ikabakia (You can't eat your cake and have it). Haiwezekani mtu aliyekufa kwa CORONA akasikia njaa!!
 
Sasa mtaji wa maskini ni Afya sasa mtu akipata corona atafanyaje Nazi , ebu tusubiri tuende kama Uganda watapata majibu chanya ...hili tuige .
 
Lockdown ni ujinga,utakuwa umefanya nini sasa kuwafungia watu ili hali unajua hali zao,ishi yao,muuza kahawa umfungie atakula nini,mchuuzi Wa ndizi,konda,wapika hotel, waziba Pancha,waikota machupa,acha tupambane na adui corona tukiwa nje siyo kujificha tukitoka tunamkuta,kila MTU achukue hatua, kujilinda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Lockdown ni ujinga,utakuwa umefanya nini sasa kuwafungia watu ili hali unajua hali zao,ishi yao,muuza kahawa umfungie atakula nini,mchuuzi Wa ndizi,konda,wapika hotel, waziba Pancha,waikota machupa,acha tupambane na adui corona tukiwa nje siyo kujificha tukitoka tunamkuta,kila MTU achukue hatua, kujilinda

Sent using Jamii Forums mobile app

Sawa kabisa
Ili tujaze hospital ambazo ziko za kutosha
Ili tupewe oxygen ambayo ipo ya kutosha kwenye kila hospital

Wazo zuri sana
 
Unakuta mama kajifunga barakoa halafu kabeba mtoto mgongoni na hana barakoa na anapanda nae daladala, hiki ni kituko!
Napendekeza iwekwe katazo la akina mama kutoka nje ya nyumba na watoto, badala yake watafute ndugu wa kuwaachia kabla ya kwenda kujitafutia riziki.

Nyie mnaonaje?
 
Wamama ndiyo baba ndiyo mama... unataka wapigwe marufuku familia zife njaa
 
Back
Top Bottom