CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

CHATO: Rais Magufuli asema Serikali haitafunga mipaka wala kuwazuia watu kutoka ndani ili kujikinga na maambukizi ya virusi vya Corona

Mwanza tumetangaziwa kwanzia leo sehemu kama Mwanza Hotel,Goden,Bunda Sriga,Malaika Beach na sehemu zote za starehe kufungwa ili kuepusha mikusanyiko isiyo ya lazima
Ndio lockdown yenyewe hiyo.....
lock from inside
 
Haya mambo siyo rahisi sana. Kiutalaamu ilibidi tuwe na hatua kali zaidi na ziwe enforced. Mikusanyiko hatarishi izuiwe, watu wakae nyumbani ukiacha wale ambao kazi zao ni za lazima. Hakikisha supplies salama ya vyakula etc.

Haya ni majukumu yanayo hitaji pesa nyingi ili yaende vizuri. Wenzetu wana economic stimulation packages ku compensate kwa negative effect ya hizo prevention and control strategies pamoja na kuwapatia watu chakula.

Serikali yangu ama haina hizo hela au inaona vigumu kusimamisha miradi yake pendwa ili pesa zihamishiwe kwenye hili janga. Sijui lipi ni lipi lakini hapa ndio kwenye kizungu mkuti. Matokeo yake tuna ambiwa corona ni hatari tujikinge nayo na hapo hapo tuna ambiwa hapa kazi tu.

Pia sio lazima hatua zichukuliwazo zihusu nchi nzima tunaweza kuwa na selective strategies kwa maeneo fulani tu kama Dar, Arusha an sehemu nyingine wakawa na hatua tofauti kutegemea na behavior ya hili gonjwa sehemu tofauti.
 
Marekani, Italy wote hao wanalia njaa sasa hivi. Itali kawafungia zaidi ya mwezi sasa Hali zao ni taabani tuache siasa za chadema na CCM.

Lock down INATESA..
Hivi unadhani magufuli anashindwa kusema wote tukae ndani.?.
Haya akisema wote tukae ndani unadhani yeye ataathirika na nini?.
Kula atakula,kulala atalala.
JE sisi raia tutaishi vipi.
Magenge yafungwe,maduka yafungwe kila mtu ndani..
Hapo ndo mwanzo wa bidhaa kuuza kwa magendo.
Kilo moja ya unga tutauziwa 10,000.

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Hata Hao MATAIFA makubwa yameanza kufeli.
Utapata wapi hela ya kuwahudumia wananchi wako mwezi mmoja na kuendelea wakati hakuna KAZI WANAZO FANYA? Masiya,

"baba unahonga hawara elfu kumi,
watoto wanakufa na njaa nyumbani"
 
Haya ma miradi ya kununua ndege cash, sgr, stiglaz na pesa zinazotumika kufanya siasa uchwara za kununua wapinzani zingetufaa sana kipindi hiki kigumu.
 
Hii signature yako Mpwa! Dah
Nimeuliza kwanini anaogopa wakati hii ni Donna Counrty? Na amesema kuna pesa ya kulisha watanzania wote kwa Miezi 6. Unataka kuniambia kwamba tukifungiwa ndani hiyo miezi 6 Corona itakua haijaisha kwetu? Jibu swali bwana acha kujifanya mwalimu
 
mjingamimi,
Nimeuliza kwanini anaogopa wakati hii ni Donna Counrty? Na amesema kuna pesa ya kulisha watanzania wote kwa Miezi 6. Unataka kuniambia kwamba tukifungiwa ndani hiyo miezi 6 Corona itakua haijaisha kwetu? Jibu swali bwana acha kujifanya mwalimu
 
Usalama upo lakini lazima waache nafasi kuepuka maambukizi
Mbona kama yuko peke yake? Usalama wa viongozi wa kitaifa ni usalama wa taifa, ndio maana makamu wa rais na rais kipindi hiki lazima wana usalama wahakikishe wako salama kiafya ili taifa liwe salama, hawaonekani mara kwa mara wakiwa wamejichanganya katika jamii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haya ma miradi ya kununua ndege cash, sgr, stiglaz na pesa zinazotumika kufanya siasa uchwara za kununua wapinzani zingetufaa sana kipindi hiki kigumu.

Sasa na wewe hapo unaona umekwisha changia mada JF.
 
Kwa hiyo mnataka rais atangaze lockdown nchi nzima?

Je, wengi wetu tunauwezo wa kula na kunywa walau wiki tatu bila kutoka nje kutafuta riziki?

Acheni ushabiki!

Sent using Jamii Forums mobile app

Si alisema iko pesa ya kutilisha miezi 6? Au kwakua wewe ni Mfia chama hii point akiitoa uligeukia upande wa pili ujifanye hujaisikia?
 
Back
Top Bottom