Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Chato: Serikali kujenga Uwanja wa kisasa wa Michezo

Mkuu yakubidi uwe muelewa wa vitu...imesemwa huu uwanja unajengwa kwa ajili ya watu kwenda kushangaa tu kisha unaushika na kulamba ukuta wake na roho yako itapona, Amina.
Huu ni uhujumu uchumi uliopitiliza, ila ndo hivyo kuna muda sheria huegemea upande mmoja ..
 
Anashindwa kujenga uwanja wa kisasa Mwanza, Mbeya au Arusha, wenda siku moja tukaanda hata kombe la mataifa la Africa.Hamna tofauti Leo kama mkapa angekuwa alijenga ule uwanja Mtwara
huyu jamaa anamatatizo makubwa sana
 
Kuna nini CHATO lakini ? Mbona awamu hii ya 5 CHATO imekuwa jina maarufu sana ?

Mimi nilikuwa najua CHATO ni kijiji tu alikotoka Rais JPM lakini mbona naona kama vile rasilimali zimeanza kugunduliwa huko sijui zinagunduliwa ama zinapelekwa.

Maana naona hadi waziri wa china alifikia huko kwani kuna siri gani ebu tuambieni maana Kipindi cha Nyerere BUTIAMA hakukuwa na siri,Kipindi cha Mwinyi kwao zanzibar sijui, Kipindi cha Mkapa LUPASO hata ilikuwa hatuijui tumekuja kuijua juzi alipokuwa anaenda kuzikwa, Kipindi cha Kikwete MSOGA pale bagamoyo hakukuwa na siri lakini hiki Kipindi cha JPM huko CHATO kuna nini ?
 
Kalemani, does he know anaongea nn huyo?
Sahv ata hao viongozi wake hawana sauti yakumpinga ata kama wanajua ukwel kitu hakina manufaa watashangilia ili kulinda nafasi zao
Ni unafiki ndio umejaa
 
Huo uwanja ukiwepo utasaidia kutumika hata shughuli zingine maana utatumika kimukoa, alafu mambo ya kujengewa vitu Kama watumiaji hawataenda kutumia ni wao wana makosa kikubwa hela ikipatikana ya kuendeleza sehemu yoyote iendelezwe bila kuchelewa hasa wilayani na vijijini kuliko jificha ujinga mwingi na uchawi,

Mimi napenda maendeleo vijijini yaani vijijini vyote vikiwa vinapata maendeleo kwa njia yoyote sijali kikubwa maendeleo hata kwa kuomba misaada ya kuendeleza vijijini ifanyike Ili tuondoe ujinga ujinga, mambo ya mtu kusubiri afike mjini akiwa hajui hata kuvuka barabara na matumizi ya vitu inatakiwa iondolewe kwa maendeleo Kila mtu apambane kufurahia maendeleo ya vijijini Ili watu waishi kisasa hata kufuga na kulima watafuga kisasa kwanini hatupendi watu wawe na exposure ya vitu?

Wasipona vitu vizuri na kujua kutumia inamaana waje mjini kuja kujifunza Sasa tutahudumia watu wangapi mjini? Nasisitiza nimependa JPM alivyoamua kuonyesha mfano kuwapelekea watu wa wilayani maendeleo ya vitu waelimike tuwe sawa na mjini na uchumi utainuka.
 
Maajabu ya Dunia!
Yaani Beberu atoke ubeberuni aje Chato kushangaa uwanja wa mpira?

Nisawa na Beberu aje kushangaa magholofa ya kariakoo.

Ni akili za kitoto na kipumbavu kuamini kwamba uwanja wa mpira ni kivutio cha utalii
 
CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI‬

‪Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania

---------
Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
Mkuu,

Ni bora uwanja huo ujngwe Katoro/Buseresele ambapo ni katikati ya Geita na Chato vinginevyo labda wanataka kuifanya Vatican City!!
 
Maandalizi yanaelekea kukamilika kufanikisha hilo!Yaani siku za mbeleni mechi za Taifa stars zitakuwa zikipelekwa Chato ili basi watu wa kanda ya ziwa iwe rahisi kuiona timu yao ya Taifa!

Chato kumenoga!
 
Huo uwanja ukiwepo utasaidia kutumika hata shughuli zingine maana utatumika kimukoa, alafu mambo ya kujengewa vitu Kama watumiaji hawataenda kutumia ni wao wana makosa kikubwa hela ikipatikana ya kuendeleza sehemu yoyote iendelezwe bila kuchelewa hasa wilayani na vijijini kuliko jificha ujinga mwingi na uchawi,

Mimi napenda maendeleo vijijini yaani vijijini vyote vikiwa vinapata maendeleo kwa njia yoyote sijali kikubwa maendeleo hata kwa kuomba misaada ya kuendeleza vijijini ifanyike Ili tuondoe ujinga ujinga, mambo ya mtu kusubiri afike mjini akiwa hajui hata kuvuka barabara na matumizi ya vitu inatakiwa iondolewe kwa maendeleo Kila mtu apambane kufurahia maendeleo ya vijijini Ili watu waishi kisasa hata kufuga na kulima watafuga kisasa kwanini hatupendi watu wawe na exposure ya vitu?

Wasipona vitu vizuri na kujua kutumia inamaana waje mjini kuja kujifunza Sasa tutahudumia watu wangapi mjini? Nasisitiza nimependa JPM alivyoamua kuonyesha mfano kuwapelekea watu wa wilayani maendeleo ya vitu waelimike tuwe sawa na mjini na uchumi utainuka.
Rais ajaye naye aelekeze miradi lukuki kijijini kwao,na huo ndio uwe utamaduni wetu!
 
Sisi wadau wa maendeleo tunakushangaa tangu kuteuliwe hadi sasa hujapeleka mchanganuo wa gharama za ujenzi wa Chato Stadium

Kandarasi hii ilipaswa itangawze mapema sana na ujenzi uwe umeanza fedha tunazo unasubiri nini?

Unataka hadi Rais aje akutumbue huu ujenzi utalisaidia taifa kupata fedha za kigeni Chato sasa hivi mandege makubwa yanatua kuna mbuga ya wanyama na vivutio vingi vya utalii.

Hakikisha unatangaza kandarasi hii kabla ya mwisho wa January ikiwezekana February mkandarasi aanze kazi.

Na tunataka Rais Museven aje kuweka jiwe la msingi ili ujenzi wake uende haraka hatutaki sijui phase one ohh mara phase three huu uwanja tunataka ukamilike kabla ya 2022.

Maendeleo hayana chama.

Hapa kazi tu.
 
Hivi ule uwanja wa mpira wa Dodoma (ule wa mfalme wa Morocco) umeishia wapi?

Maendeleo hayana mahali na chama.
 
Hivi uwanja wa mpira unahamasishaje watalii?

Yaani watalii waache huko kwao kwenda kushangaa Wembley Stadium waje washangae Chato Stadium?

Haya bana.
Hahahhaahhaaahahahhaaha yn Tanzania inamajaabu mengi kuliko maajabu ya dunia
 
Back
Top Bottom