Huu ni uhujumu uchumi uliopitiliza, ila ndo hivyo kuna muda sheria huegemea upande mmoja ..Mkuu yakubidi uwe muelewa wa vitu...imesemwa huu uwanja unajengwa kwa ajili ya watu kwenda kushangaa tu kisha unaushika na kulamba ukuta wake na roho yako itapona, Amina.
Wanatumwa,Kujipendekeza Hadi aibu. Wanakera Sana Hawa waramba viatu.
Sahv ata hao viongozi wake hawana sauti yakumpinga ata kama wanajua ukwel kitu hakina manufaa watashangilia ili kulinda nafasi zaoKalemani, does he know anaongea nn huyo?
Maajabu ya Dunia!
Yaani Beberu atoke ubeberuni aje Chato kushangaa uwanja wa mpira?
Nisawa na Beberu aje kushangaa magholofa ya kariakoo.
Mkuu,CHATO STADIUM KUJENGWA HIVI KARIBUNI
Waziri Medard Kalemani amesema Serikali ipo mbioni kujenga Uwanja wa mpira wa Chato Stadium ambao amedai utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya Tanzania
---------
Serikali imetangaza kujenga uwanja mkubwa wa mpira wilayani Chato, mkoani Geita ili kukuza sekta ya michezo nchini na kuvutia watalii na wawekezaji. Uwanja huo unatarajiwa kuwa wa pili kwa ukubwa baada ya wa Benjamin Mkapa ulipo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nishati Medard Kalemani amesema hayo wakati akihutubia sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya taifa ya Burigi-Chato na kueleza kwamba uwanja huo utaitwa Chato Stadium na ujenzi wake unatarajiwa kuanza hivi karibuni.
"Hivi karibuni tunajenga Uwanja wa mipra Chato Stadium ambao utatumika sana katika kuhamasisha Wawekezaji na hasa Watalii wanaotoka nje ya nchi yetu" amesema Waziri Medard Kalemani.
Rais ajaye naye aelekeze miradi lukuki kijijini kwao,na huo ndio uwe utamaduni wetu!Huo uwanja ukiwepo utasaidia kutumika hata shughuli zingine maana utatumika kimukoa, alafu mambo ya kujengewa vitu Kama watumiaji hawataenda kutumia ni wao wana makosa kikubwa hela ikipatikana ya kuendeleza sehemu yoyote iendelezwe bila kuchelewa hasa wilayani na vijijini kuliko jificha ujinga mwingi na uchawi,
Mimi napenda maendeleo vijijini yaani vijijini vyote vikiwa vinapata maendeleo kwa njia yoyote sijali kikubwa maendeleo hata kwa kuomba misaada ya kuendeleza vijijini ifanyike Ili tuondoe ujinga ujinga, mambo ya mtu kusubiri afike mjini akiwa hajui hata kuvuka barabara na matumizi ya vitu inatakiwa iondolewe kwa maendeleo Kila mtu apambane kufurahia maendeleo ya vijijini Ili watu waishi kisasa hata kufuga na kulima watafuga kisasa kwanini hatupendi watu wawe na exposure ya vitu?
Wasipona vitu vizuri na kujua kutumia inamaana waje mjini kuja kujifunza Sasa tutahudumia watu wangapi mjini? Nasisitiza nimependa JPM alivyoamua kuonyesha mfano kuwapelekea watu wa wilayani maendeleo ya vitu waelimike tuwe sawa na mjini na uchumi utainuka.
Hahahhaahhaaahahahhaaha yn Tanzania inamajaabu mengi kuliko maajabu ya duniaHivi uwanja wa mpira unahamasishaje watalii?
Yaani watalii waache huko kwao kwenda kushangaa Wembley Stadium waje washangae Chato Stadium?
Haya bana.