Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

Kwanza ni kutoe hofu, mimi sifungamani na vyama vya kisiasa wala kidini.

Pili, Wakati vitu vinarundikwa Daslam hamkujua kuna wahitaji? Je ulikuwa ni upendeleo?

Chato ipo katikati ya Wilaya takribani sita. Ndio maana nimesema Musoma na viunga vyake, Kahama, Shinyanga na Simuyu wafike Mwanza.

Ujiji, Kigoma, Bukoba, Biharamulo, Geita wafike Chato. Maana walifika Daslam kwa takribani miaka 60.
 
Kama mzaha kwenye Soap Opera walianza na Traffic Light pasipo na gari, mara paa mwanafunzi wa kwanza kitaifa hii ndani ya episode ya pili..
 
Ile ya Bugando imeshindwa kuwahudumia au? Au hayo yanafanyika hili hiyo huduma iwe karibu na nyumbani. Kama ni kufa mtu atakufa tu hata kama anahishi hospitalini.
 
Tumwulize Umi Tanga hamna watu wa kustahili hospitali ya rufaa ya kanda. Umbali wa Chato hadi Bugando na umbali wa Tanga hadi KCMC ama Mhimbili upi mkubwa? Kanda ya kusini je wana hospitali ya rufaa?
 
... kwa hiyo kuyarundika Chato ndio itakuwa tiba? Kama unadhani kurundika Dar sio tiba kwanini udhani kufanya hivyo Chato ndio itakuwa tiba?
Kuna vitu ni vyepesi sana kuvichanganua na moja ni Chato kuzungukwa kila pande yaani lazima tu watu wa maeneo hayo wakanyage pale. Ilhali mtu Kigoma anavuka takribani mikoa mitano hadi Daslam, Haiwezekani!
 
Dodoma hii hii nayoijua ama kuna nyingine boss?
 
Hakuna cha ubaba! Taifa umaskini chanzo ni yeye. Magufuli ndiyo ananyoosha hii sasa.
Wewe huijui Tanzania na wala haumjui Nyerere hata chembe, anayofanya Mh. Magufuli sasa hajafikia na hatafikia robo ya mambo ya maendeleo aliyofanya Nyerere.

Ushabiki usivuke mipaka ukawafanya watu wavimbe vichwa.
Sasa toka humu JF nenda kaanze kuhesabu barabara, madaraja, reli, ndege, shule, vyuo, hospital, viwanda, mabwawa ya kuzalisha umeme, na huduma zilizokuwa zinatolewa na serikali wakati wa Nyerere kwenye hivyo vitu nilivyo kutajia.

Huyu muheshimiwa Magufuli alikuwa anakunywa chai ya maziwa na mkate shuleni na vyuoni, hakukuwa na mkopo elimu ya juu, wote ilikuwa bure. Huenda hata enzi zake alipata madaftari shuleni huko primary school.

Watu walilipiwa na serikali usafiri wa kutoka kijijini huko inakojengwa hospital kwenda chuo, wanachuo walipanda hadi ndege kwenda UDSM.

Wewe nahisi ni kijana wa majuzi, mwache Nyerere aitwe baba wa Taifa. Kuna watu kibao kawapeleka nje kusoma elimu ya juu fani mbali mbali.
Huyu wa sasa unataka kumkuza kuliko Nyerere tuambie wangapi amepeleka nje tofauti na wale, nasema wale nikiamini unawajua.

Ukweli Mh. Magufuli ni rahisi ninae mkubali na kumtetea sana popote pale, ni wa mfano baada ya Nyerere anafuata yeye kwa mtazamo wangu hadi sasa.
Sijui hapo baadae ataendeleza ubora au ataharibu! Hilo swali muda utatupatia majibu sahihi. Hatuwezi kuagua na kupiga ramli kama waganga.
 
Kuna vitu ni vyepesi sana kuvichanganua na moja ni Chato kuzungukwa kila pande yaani lazima tu watu wa maeneo hayo wakanyage pale. Ilhali mtu Kigoma anavuka takribani mikoa mitano hadi Daslam, Haiwezekani!
... tuanzie na mkoa wenyewe wa Geita; hivi kwa akili ya kawaida sana katikati ni wapi? Naona Chato iko CENTRAL kwelikweli!
 
Hayo yote unayotanabaisha hapa mbona ameyapokea baada ya kuwafukuza British? tokea hapo mbona hamna yaliyoongezeka?!.

Hivi vitu vya ubaba na umama ni siasa tu! Nina documents za Germany East Africa (Deutschland) na British Territory ambazo hata Jamhuri haina na haitokuwa nazo.

Narudia nina documents za Germany na British zenye ukweli wa yote ambazo hata Jamhuri haina.

Ukitaka kupiga maendeleo Tanzania hii kwanza ukatae ubaba na hivyo ndivyo Magufuli alipofanikisha na watu wanastaajabu.

"Kama walikuwa wanafanya, mbona hayaonekani?!." - John Pombe Magufuli
 
Dada shikamoo siyo kwa point hii!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…