Chato yazidi kuneemeka; Serikali kujenga Hospitali ya Rufaa ya kanda ya Ziwa

... tuanzie na mkoa wenyewe wa Geita; hivi kwa akili ya kawaida sana katikati ni wapi? Naona Chato iko CENTRAL kwelikweli!
View attachment 1328475
Mada inaeleza ni Hospitali ya Kanda ya Ziwa na siyo Kanda ya Geita.

Hivyo basi kama ni Kanda ya Ziwa, Chato inakuwa baina ya Wilaya za Kigoma na Kagera pia hizo za Geita.

Huku Mwanza hizo hospitali mbili zinakuwa zimeshika Mara, Shinyanga na Simuyu.

Mbona hii haitaji Masters ya Mipango miji.
 
Hospital ishaisha na mambo yapombyeeee
Sent using Jamii Forums mobile app
 
umecheka kama wale wajumbe wa kamati kabisa!
 
... Chato kwenda Mwanza ni umbali gani? Very near! Kwani hospitali mbili za rufaa ziwe karibu wakati maeneo mengine ya nchi hayana? Tungetaka kuwa wakweli, hospitali hii ingejengwa either far west (Kigoma say) or far east (Musoma say) kanda hiyo hiyo ya Ziwa. Maana yake upande mmoja ungeenda Mwanza na upande mwingine Kigoma/Musoma lakini sio kama ilivyowasilishwa na Mh. Waziri Ummy!
 
Preferably labda Kigoma au Kagera maana Mara wamewekwa kati na Mwanza na Arusha too near!

Well labda ipelekwe Kigoma au Kagera basi. Without that Chato ni kati ya hao wote.
 
Duh! Seketule na bugando hazitoshi kwani..?
Unataka mijisindano yote hiyo imchome nani..? Wapelekewe na wengine huko
 
Baada ya Waziri Ummy kueleza hayo, baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CCM), Peter Serukamba walicheka.
Na mimi naungana nao kucheka 🀣🀣🀣...!!!
 
Utakuwa kichaaa kuliko huyo anayejenga
 
Wamejitokeza kutumia fursa baada ya kumsoma Magu,wanaona mamiradi yanaelekezwa huko,kwanini wasitumie fursa?Kigoma,Kagera,Rukwa hakuna hospitali yenye hadhi ya rufaa!Wagonjwa Wote hukimbilia Bugando Mwanza,hii ni wazi JPM ameamua kuwa Mobutu Seseko!
 
Waliocheka wasirudishwe kugombea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja ijengwe haraka sana. Tunaihitaji sana hospitali hiyo! Anaeona wananeemeka tunashauri naye ahamie huko.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duu! Huenda kukawa ni kulipa fadhila za kutotumbuliwa kwa miaka yote ya uwaziri! Binafsi nilizani Bugandle ingefanyiwa kwanza maboresho makubwa ili iweze kupanua huduma zake kama vile kupandikiza figo, kutoa huduma za matibabu ya moyo bila kufanya operation n.k! Quality is better than quantity!.....Pamoja na hayo ni vema tukaukemea huu utamaduni ulioanza kujengeka kwa mawaziri kushindana kujipendekeza kwa mkuu wa kaya, Leo huyu anapeleka uwanja wa ndege wa kimataifa, Kesho mwingine mwingine anajenga Soko la madini, Hapoapo mnasikia mwingine akitangaza kujenga uwanja wa mpira wa kimataifa wakati hakuna hata timu ya daraja la pili, Kesho kutwa m,nasikia mwingine akitangaza kujenga hospitali ya Rufaa ya kanda !!!!....Jamani hivi ni huko tu ndiko wanakoishi walipa kodi wa nchi hii????? Hebu tazameni na mikoa mingine, katika hiyo miradi yote kuna mikoa haina hata mmoja! Tujaribu kugawana keki ya taifa letu kwa haki, vinginevyo tutakuwa tunalipeleka taifa letu kusiko na njia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…