Chatu mkubwa katika pori jirani na 'Chuo Nyeti' Mbweni Malindi adhibitiwe upesi kabla hajaleta madhara

Wafanye mpango kama vipi wale jamaa wa Maliasili waje wamchukue na wamuhamishe maeneo hayo maana kuna shughuli nyingi za kiraia maeneo hayo tangu kuwepo na bandari bubu maeneo yale.
Na bila shaka atakuwa anatokea kwenye ule msitu wa wavunja matofali unaopakana na hicho chuo
Ndiyo yuko nao Jirani.
 
Ila wavulana wa Dar mnachekesha. Unaogopa chatu kweli? Asante mama kwa bandari, vijana wako hawana ujasiri wa kukabiliana na chatu, hawataweza mikiki mikiki ya bandari hawa.
😂😂😂😂😂😂 muulize yeye alienda kufanya nini malindi kama sio umbea tu ameshindwa kutulia zake 365
 
Mpumbavu kama huyo na Wenzake baadhi unaowaona hapa ( Waliochangia ) waelewe nini Mkuu?

Wewe ndiyo uliyeuelewa vyema huu Uzi na Kuchangia Kiumakini na kwa tahadhari Kubwa ya huyo Chatu ambayo GENTAMYCINE nimeitoa / nimeileta hapa JamiiForums kwa nia njema tu ili nisaidie na niokoe Wengine wasije Kudhurika nae.
Ndomana wakati mwingine tunaambiwa usiwaamshe wale waliyolala,unawaacha na ubish wao

Ova
 
Mida yake ya kuvuka barabara hiyo ya lami ni kati ya saa 2 hadi Saa 3 usiku na ni mkubwa sana.

Nina uhakika wale wote wanaopita hiyo njia wakiwa ama katika Bajaji au Pikipiki za Bodaboda au DalaDala za Mbweni - Makumbusho au hata gari binafsi ama mmeshawahi kukutana nae au nanyi hivi karibuni tu mtakutana nae.

Ushauri wangu kama GENTAMYCINE kwa taasisi zote kuu mbili nyeti nchini Tanzania ni kwamba kwakuwa mji unakuwa na watu wanahamia maemeo yaliyokuwa ni maalum kwa mafunzo yao (Maporini/Misituni) basi ikiwapendeza wawe wanahamishia hayo mapori mafunzo yao maeneo ya mbali zaidi ili viumbe hatari kama huyu chatu (joka kubwa) wasiwe hatarishi kwa wananchi / wakazi.
halafu wanadamu huwa wanamchukulia chatu poa sana. vile vile unavyomwona, anachohitaji yeye ni kukurukia akukamate tu, akishafanikiwa, kujiviringisha mwilini mwako ni dakika sifuri, na ukishaona amejiviringisha, hata uige greda lije livute ajiviringue haliwezi, ana nguvu za ajabu kuvunja mbavu na kuhakikisha haupumui na muda mchache tu unapoteza maisha. wapo watu walioshuhudia wenzao wakifa mbele yao na hawana uwezo kumwokoa mtu ambaye tayari ashakamatwa na chatu, sio rahisi. zamani kijijini kwetu tulikuwa tunaambiwa ukimchoma na sindano au kitu chenye ncha kali anaweza kuachia, ila sasa ngozi yake ni nguvu ajabu, unaweza kukata na panga likadunda. nakumbuka hiyo ndio ngozi kijijini kwetu tulikuwa tunatengenezea ngoma, zinalia vizuri kweli. nashauri maliasili waende wakamwue haraka huyo au la wanakijiji wajitolee wakammalize tu.
 
Kijijini walikuwepo wenye uwezo wa kumeza mpaka ndama na tuliwaua sana, huyo GENTAMYCINE aka Popoma ilibidi apambane naye amuue sio kutupigia kelele hapa.
Chatu anatakiwa kuhamishwa, siyo kuuawa. Ukizingatia pale alipo inawezekane kwa ni ni ndiyo natural habitat yake, hajavamia isiookuwa watu ndiyo wamevamia natural habitat yake.
Hivyo alichokifanya GENTAMYCINE ni sahihi kutoa wito kwa mamlaka husika kuchukua hatua.
Uanaume ni kujua mahitaji ya kimsingi na kiasili ya viumbe wengine.
 
Mida yake ya kuvuka barabara hiyo ya lami ni kati ya saa 2 hadi Saa 3 usiku na ni mkubwa sana.

Nina uhakika wale wote wanaopita hiyo njia wakiwa ama katika Bajaji au Pikipiki za Bodaboda au DalaDala za Mbweni - Makumbusho au hata gari binafsi ama mmeshawahi kukutana nae au nanyi hivi karibuni tu mtakutana nae.

Ushauri wangu kama GENTAMYCINE kwa taasisi zote kuu mbili nyeti nchini Tanzania ni kwamba kwakuwa mji unakuwa na watu wanahamia maemeo yaliyokuwa ni maalum kwa mafunzo yao (Maporini/Misituni) basi ikiwapendeza wawe wanahamishia hayo mapori mafunzo yao maeneo ya mbali zaidi ili viumbe hatari kama huyu chatu (joka kubwa) wasiwe hatarishi kwa wananchi / wakazi.
Kwakua ni eneo la mafunzo ni sahihi awepo hapo kwani ni sehemu ya watakavyo kumbana navyo maporini.
 
halafu wanadamu huwa wanamchukulia chatu poa sana. vile vile unavyomwona, anachohitaji yeye ni kukurukia akukamate tu, akishafanikiwa, kujiviringisha mwilini mwako ni dakika sifuri, na ukishaona amejiviringisha, hata uige greda lije livute ajiviringue haliwezi, ana nguvu za ajabu kuvunja mbavu na kuhakikisha haupumui na muda mchache tu unapoteza maisha. wapo watu walioshuhudia wenzao wakifa mbele yao na hawana uwezo kumwokoa mtu ambaye tayari ashakamatwa na chatu, sio rahisi. zamani kijijini kwetu tulikuwa tunaambiwa ukimchoma na sindano au kitu chenye ncha kali anaweza kuachia, ila sasa ngozi yake ni nguvu ajabu, unaweza kukata na panga likadunda. nakumbuka hiyo ndio ngozi kijijini kwetu tulikuwa tunatengenezea ngoma, zinalia vizuri kweli. nashauri maliasili waende wakamwue haraka huyo au la wanakijiji wajitolee wakammalize tu.
Unachoma kitu chenye ncha Kali chili tumboni ambako ni laini,siyo juu,juu hata shoka linadunda
 
Kwa hio kila siku mida hio chatu ndio anatoka mishe zake anarudi chimbo [emoji23][emoji23]
 
Chatu akiwa na njaa hupita mpaka dirishani. Chuo hicho wajiangalie. Kama huo msitu Una wanyama wengi wadogo basi Hakuna shida.

Muhimu maliasili wamhamishe.
 
Back
Top Bottom