halafu wanadamu huwa wanamchukulia chatu poa sana. vile vile unavyomwona, anachohitaji yeye ni kukurukia akukamate tu, akishafanikiwa, kujiviringisha mwilini mwako ni dakika sifuri, na ukishaona amejiviringisha, hata uige greda lije livute ajiviringue haliwezi, ana nguvu za ajabu kuvunja mbavu na kuhakikisha haupumui na muda mchache tu unapoteza maisha. wapo watu walioshuhudia wenzao wakifa mbele yao na hawana uwezo kumwokoa mtu ambaye tayari ashakamatwa na chatu, sio rahisi. zamani kijijini kwetu tulikuwa tunaambiwa ukimchoma na sindano au kitu chenye ncha kali anaweza kuachia, ila sasa ngozi yake ni nguvu ajabu, unaweza kukata na panga likadunda. nakumbuka hiyo ndio ngozi kijijini kwetu tulikuwa tunatengenezea ngoma, zinalia vizuri kweli. nashauri maliasili waende wakamwue haraka huyo au la wanakijiji wajitolee wakammalize tu.