Chatu mkubwa katika pori jirani na 'Chuo Nyeti' Mbweni Malindi adhibitiwe upesi kabla hajaleta madhara

Chatu mkubwa katika pori jirani na 'Chuo Nyeti' Mbweni Malindi adhibitiwe upesi kabla hajaleta madhara

Aisee napitaga sana huko kufanya mazoezi ila kutembea inakuwaga mwisho saa moja na nusu ...ila lile pori lazima TU chatu wawepo
 
Ila wavulana wa Dar mnachekesha. Unaogopa chatu kweli? Asante mama kwa bandari, vijana wako hawana ujasiri wa kukabiliana na chatu, hawataweza mikiki mikiki ya bandari hawa.
Mpaka mtu amezwe ndio mtaacha mizaha kwenye mambo serious..
 
Aisee umenikumbusha zamani sana, tulivokuwa high school shule flani kongwe sana iliyopo karibu na msituni Minaki tulikuwaga na chatu wengi sana na nyoka wengi sana, aisee namshukuru mungu nilimaliza salama na sikuwahi kuumwa na nyoka, kipindi cha mvua walikuwa wanatoka msituni wanapanda huku juu madarasani kutafuta joto, kuna siku wakati rafiki yangu anatoa vitabu kwa ajili ya kuvipanga, vitabu alivokuwa amevieka chini kweny kona ya ukutani, bhana si kulikuwa kuna nyoka kajificha kweny gape kali ya vile vitabu na ukuta, aliruka ghafla baada ya kusikia vitabu vinahamishwa, mm nilikuwa nipo busy nasoma zangu, jamaa yangu akapiga kelele "Wazee nyoka" aisee mm ni jasiri wa vitu vingi lakini nyoka hapana, baada ya kusikia hio sauti ya mshkaji nilijikuta nipo nje ya darasa sijui nilifikaje, haraka nilianza kuokota mawe na kumrushia, wengine wakawa wanahangaika kule ndani hawaamini kilichotokea, kwa bahati nzuri kuna washkaji walikuwa nje ya darasa wakajumuika na mm kumrushia mawe yule nyoka, bahati nzuri akafa hakumdhuru mtu yeyote, alikuwa ni nyoka wa kijani, unene na urefu wa yule nyoka ulikuwa very significant kabisa.
kuna mambo nikifikiria nabaki tuu namshukuru mungu, siku zingine unapishana na nyoka, one day nilimkanyaga nyoka mweusi bahati nzuri kwa hofu yangu ya nyoka likizo nilivorudi home mzee wangu alininunulia mabuti kwaio hakuweza kunidhuru lakini huo mshtuko na hizo mbio zilizofuata baada ya hapo aisee adrenaline ni kitu chengine. Ilikuwa ni kawaida sana kipindi cha mvua kwa wiki wanafunzi wawili au watatu kupelekwa hospitali ya kisarawe cause of snake bites.
Siku nyingine tuliua chatu mkubwa, yule alikuwa anauwezo wa kumeza mtu mzima bila shida, hio siku siwez sahau, wanaume tulipambana hadi akafa mm kawaida yangu nikiwa mbali nikirusha mawe yangu fresh kabisa.
Nakumbuka mwalimu mkuu alitupa kila mmoja aliyehusika kumuua kreti la soda, nilikuwa nasubiria siku za wali ndo nashushia wali na soda na washkaji zangu(sio mpenzi wa soda tokea kitambo, nilikunywa moja tuu zingine niliwaachia).
Baada ya kumuua yule chatu nakumbuka kuna mlinzi akatuambia hamwez kuwamaliza chatu wanaishi kweny huu msitu, nilichoka aisee.
Hadi namaliza minaki tulifanikiwa kuua chatu wawili.

Ushauri wangu, kama unaona hatari ipo karibu bora uifanyie timing, don't procrastinate kwa sababu ukifanyiwa timing ww ni kifo, kama sisi tulikuwa ni wanafunzi na tulitumia jembe, sululu na mawe kumuua na nyie tafuteni namna afe hata kama ni Mali ya mtu au ni mtu kajibadilisha kuwa chatu, naamini mna resources kuliko hata tulizokuwa nazo sisi.
 
Mwanaume unaogopa chatu kweli? Dah.....katika maisha yangu sijawahi ogopa chatu napambana nae vizuri tu....
 
Kama huyu
IMG_20230527_203035.jpg
 
Mida yake ya kuvuka barabara hiyo ya lami ni kati ya saa 2 hadi Saa 3 usiku na ni mkubwa sana.

Nina uhakika wale wote wanaopita hiyo njia wakiwa ama katika Bajaji au Pikipiki za Bodaboda au DalaDala za Mbweni - Makumbusho au hata gari binafsi ama mmeshawahi kukutana nae au nanyi hivi karibuni tu mtakutana nae.

Ushauri wangu kama GENTAMYCINE kwa taasisi zote kuu mbili nyeti nchini Tanzania ni kwamba kwakuwa mji unakuwa na watu wanahamia maemeo yaliyokuwa ni maalum kwa mafunzo yao (Maporini/Misituni) basi ikiwapendeza wawe wanahamishia hayo mapori mafunzo yao maeneo ya mbali zaidi ili viumbe hatari kama huyu chatu (joka kubwa) wasiwe hatarishi kwa wananchi / wakazi.
Chatu ni mboga tamu sana hasa ukimchoma na upate mihogo ya kukaanga au ndizi choma
images-12.jpg
images-11.jpg
 
Mida yake ya kuvuka barabara hiyo ya lami ni kati ya saa 2 hadi Saa 3 usiku na ni mkubwa sana.

Nina uhakika wale wote wanaopita hiyo njia wakiwa ama katika Bajaji au Pikipiki za Bodaboda au DalaDala za Mbweni - Makumbusho au hata gari binafsi ama mmeshawahi kukutana nae au nanyi hivi karibuni tu mtakutana nae.

Ushauri wangu kama GENTAMYCINE kwa taasisi zote kuu mbili nyeti nchini Tanzania ni kwamba kwakuwa mji unakuwa na watu wanahamia maemeo yaliyokuwa ni maalum kwa mafunzo yao (Maporini/Misituni) basi ikiwapendeza wawe wanahamishia hayo mapori mafunzo yao maeneo ya mbali zaidi ili viumbe hatari kama huyu chatu (joka kubwa) wasiwe hatarishi kwa wananchi / wakazi.
Hivi huyo nyoka bado hajauawa? Niliwahi kusikia malalamiko siku za nyuma kuwa kuna chatu mkubwa maeneo hayo.
 
Mida yake ya kuvuka barabara hiyo ya lami ni kati ya saa 2 hadi Saa 3 usiku na ni mkubwa sana.

Nina uhakika wale wote wanaopita hiyo njia wakiwa ama katika Bajaji au Pikipiki za Bodaboda au DalaDala za Mbweni - Makumbusho au hata gari binafsi ama mmeshawahi kukutana nae au nanyi hivi karibuni tu mtakutana nae.

Ushauri wangu kama GENTAMYCINE kwa taasisi zote kuu mbili nyeti nchini Tanzania ni kwamba kwakuwa mji unakuwa na watu wanahamia maemeo yaliyokuwa ni maalum kwa mafunzo yao (Maporini/Misituni) basi ikiwapendeza wawe wanahamishia hayo mapori mafunzo yao maeneo ya mbali zaidi ili viumbe hatari kama huyu chatu (joka kubwa) wasiwe hatarishi kwa wananchi / wakazi.
Mura leo umeniangusha sana tatah, chatu kitu kidogo sana.
 
Wanaume wa dar bwana yani hadi Chatu mnaomba msaada mwa serikali??mnashindwa ungana hapo mumuje?
 
Back
Top Bottom