LGE2024 CHAUMMA yapata ushindi wa kiti 1 kati ya viti 181 Mbeya na kuwa chama pekee cha upinzani kilichopata ushindi mkoani humo

LGE2024 CHAUMMA yapata ushindi wa kiti 1 kati ya viti 181 Mbeya na kuwa chama pekee cha upinzani kilichopata ushindi mkoani humo

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

CHADEMA, ACT hola? Wagombea walienguliwa wote au nini kimetokea?

CHAUMA upinzani anashinda anamshukuru Rais Samia kwa kushinda? CCM safari hii mmetisher!:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

=====

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimefanikiwa kupata ushindi katika nafasi ya Mwenyekiti Serikali ya mtaa kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 ikiwa ndio Chama pekee cha upinzani kilichopata ushindi jijini Mbeya.

Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Akizungumza baada ya kuapishwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko - Mwanjelwa Brian Mwakalukwa wa chama hicho amesema atahakikisha anashirikiana ipasavyo na wenyeviti 180 waliopita kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwani maendeleo hayana Chama.

"Uchaguzi ulikuwa wa huru na haki, tunamshukuru mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan kwa kunirejeshea jina langu kama nimeshinda, nilikuwa na Furaha sana,"alisema Mwakalukwa

PIA SOMA
- LGE2024 - CHAUMA: Chagua viongozi wa CHAUMA na Sera ya Ubwabwa, huwezi kufanya maendeleo bila kushiba!
 
Safi sana.

Chadema itarudi kivingine. Lkn tusije kulaumiana.
 
Safi sana. Mvua ikinyesha ndipo utaona panapovuja kwenye nyumba.
 
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimefanikiwa kupata ushindi katika nafasi ya Mwenyekiti Serikali ya mtaa kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 ikiwa ndio Chama pekee cha upinzani kilichopata ushindi jijini Mbeya.
Ubwabwa si upo kwa wingi Mbarali na Kyela?
 
Mzee wa ubwawa wa Chauma Kwa mara ya kwanza amenyakua ushindi wa mgombea wake kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Mtaa Jijini Mbeya.

Ikumbuke Mbeya Kwa kina Sugu ndiko Chadema wanajifanyaga ni ngome Yao lakini Wameambulia Sifuri yaani zero huku nafasi zote zikienda Kwa Tulia-CCM na Chauma 😁😁😁😁.👇👇

My Take:
Ukiweka Wagombea wenye staha na maadili Wananchi wanakuchagua maana Viongozi wa Mitaa tunaishi wote huku huku tunatambuana sio sawa na Wabunge au Madiwani Hadi tuhadithiwe.

======

WENYEVITI WA MITAA MBEYA WABEBESHWA JUKUMU LA WATOTO WA MITAAN.

Wenyeviti wa Mitaa 181 ya Jiji la Mbeya kutoka vyama vya CCM na CHAUMA pamoja na wajumbe 905 wanaounda uongozi wa serikali za Mitaa, wameapishwa baada ya zoezi la uchaguzi kukamilika na kutangazwa kuwa washindi kwenye nafasi hizo.

Wenyeviti hao 181, kati yao 180 wanatokana na chama cha mapinduzi CCM huku mmoja kati yao akitokana na chama cha Ukombozi wa Umma CHAUMA, wamehimizwa kuzitumia nafasi hizo vyema ikiwa ni pamoja na Kupambana na ongezeko la watoto wa mitaani.

Mohamed Aziz ni Katibu tawala wa Wilaya ya Mbeya, anasema Kama viongozi wa serikali za Mitaa wakishindwa kusimamia usalama kwenye Mitaa yao hakutakua na utulivu hivyo ni jukumu lao kuyasimamia hayo, huku msimamizi msaidizi wa uchaguzi Ally Nnunduma akiwataka kuchangia mawazo yao katika maendeleo ya Jiji la Mbeya.

Nae mwenyekiti pekee anayetokana na chama cha ukombozi wa Umma, (CHAUMA) Brayan Mwakalukwa kutoka mtaa wa Soko kata ya Ruanda amesema anayofuraha kubwa kushinda nafasi ya mwenyekiti kupitia Chama hicho na anaahidi kutoa ushirikiano kwa wenyeviti wenzake, Diwani wa kata Ruanda na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt Tulia Ackson.

View: https://www.instagram.com/reel/DDADK0HIyvb/?igsh=ajJtc3Q0aGowZ29k
 
Kuna wakati nilikuwa nasikia kelele mitandaoni eti Tulia amekalia kuti kavu kwenye jimbo Sugu anasubiri kuapishwa.

Mitandao inawadanganya sana Chadema.
Ni Upuuzi wa Machadema na wewe,yaani Tulia aliyeibadilisha Mbeya Kwa miaka 5 apigwe chini uchague Mzee Sugu aliyekaa miaka 10 na hakuna alichofanya.?

Zama za ushabiki wa kijinga hazipo Kwa Sasa na bahati mbaya Machadema wamekalia hayo hayo.

Ngoja mwakani washikishwe adabu sawa sawa.
 
Wakuu,

CHADEMA, ACT hola? Wagombea walienguliwa wote au nini kimetokea?

CHAUMA upinzani anashinda anamshukuru Rais Samia kwa kushinda? CCM safari hii mmetisher!:KEKLaugh::BearLaugh::BearLaugh:

=====

Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimefanikiwa kupata ushindi katika nafasi ya Mwenyekiti Serikali ya mtaa kwenye Uchaguzi wa Serikali za mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024 ikiwa ndio Chama pekee cha upinzani kilichopata ushindi jijini Mbeya.

Akizungumza baada ya kuapishwa Mwenyekiti wa Mtaa wa Soko - Mwanjelwa Brian Mwakalukwa wa chama hicho amesema atahakikisha anashirikiana ipasavyo na wenyeviti 180 waliopita kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi kwani maendeleo hayana Chama .

"Uchaguzi ulikuwa wa huru na haki, tunamshukuru mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan kwa kunirejeshea jina langu kama nimeshinda ,nilikuwa na Furaha sana,"alisema Mwakalukwa

PIA SOMA

- LGE2024 - CHAUMA: Chagua viongozi wa CHAUMA na Sera ya Ubwabwa, huwezi kufanya maendeleo bila kushiba!
Chadomo chaliii 😁😁😁
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Chadema lichama lilishajifia, eti mdude na sativa ndo mashujaa wao.
Mbowe kapuyanga tuu. Mama kawagalagaza.
Hivi watu wapuuzi kama hao wasio na staha unaweza wasimamisha Kwa watu wastaarabu wakawachagua?

Sasa huo ni mfano mmja tuu,watu wa hivyo wasio na maadili Wala Heshima ndio walisimamishwa kushindana na CCM ambayo Ina wazee wenye Heshima zao wengine wamedumu kwa miaka 30.

Bahati mbaya sana uchaguzi wa Serikali za Mitaa tunatambuana
 
Kuna wakati nilikuwa nasikia kelele mitandaoni eti Tulia amekalia kuti kavu kwenye jimbo Sugu anasubiri kuapishwa.

Mitandao inawadanganya sana Chadema.
Sana tena sana shida ya Chadema hizi vurugu sio jambo wa Tanzania wanapenda watu hawataki fujo wa Tanzania watu wakupenda raha nadhani muda muafaka wakirudi kwenye reli wakafanya siasa badala ya uanaharakati watafanikiwa kipindi pekee walifanya siasa baada ya kumchukua CCM Lowasa vs CCM walifanya siasa na walifanikiwa. Siasa za kufanya kama unagombania uhuru zimepitwa na wakati.
 
Back
Top Bottom