Chawa wa Mama wamemgeuka Salim Kikeke; wamempora nafasi yake wamempa Mobhare Matinyi

Chawa wa Mama wamemgeuka Salim Kikeke; wamempora nafasi yake wamempa Mobhare Matinyi

Wa Tz mnapenda sana kugeuza stori za vijiweni kuwa habari kamili, kila mtu anamipango yake jamaa alivyosema tu anaondoka BBC nyie mkaanzisha stori za hisia kuwa inawezekana anakuja kupata nafasi serekalini, sahiv matarijio yenu yamekua tofaut mnasema kadhulumiwa nafasi yake.

Siyo kila mtu anamipango sawa na hisia zako, kikeke angekua anataka nafasi serekalin asingempiga maswali magumu Samia kwenye ile interview had samia akapanic angeanza kumsifia kulekule ajitengenezee mazingira
 
Sio rahisi BBC kumuachisha kazi mfanyakazi hapo London labda kama huzijui vema employment laws za Uingereza. Ni rahisi tu ndani ya miaka 2 ya mwanzo wa ajira lakini hata hiyo ina discrimination disclaimer, baada ya hapo sio rahisi- ni mchakato mrefu sana. Kumbuka pia kwamba wazungu wa UK hawajali sana elimu ya darasani, wanajali sana uzoefu kazini na ndio maana wanakazania sana apprentships, work expirences etc kwa watoto wao. na kuna makamuni hutoa degree kwa uzoefu wa kazi pekee. Nakuomba tu acha kutoa sweeping statements bila ushahidi maana defamation itakuhusu.
Unaona sasa ulivyo muongo eti wazungu wa UK hawajali elimu sana! Jidanganye labda kwa kazi ya kubeba boksi. Haujui lolote nakuhakikishia SK kimemtoa BBC elimu na kashindwa na Mkenya ndio yeye na wenzake wakatoa wengine wakakimbilia Idhaa ya Kiswahili ya Uturuki. BBC bila elimu na kumbuka dunia inapika kwenye bahari ya mabadiliko makubwa sio hizi Local media sina akina Swebe,Baba Levo,Kitenge, Kumwembe na akina Jose Mara zilivyojaza upuuzi na ujinga mtupu. Tena ukome kusema UK hawajali elimu vile vyuo vyao unajua wanavyozilinda kupokea watu wajinga kama wewe.
 
Hakuna salamu hapa, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kama ilivyokuwa kwa Tido Mhando aliyetolewa BBC na kuletwa kusimamia TBC, ndivyo ilivyokuwa kwa Salim Kikeke. Taarifa za kiintelejensia zinapenya kuwa ndugu Kikeke aliombwa kung’atuka BBC ili arudi nchini kuandaliwa kuwa msemaji wa serikali. Baada ya kufika nchini alisubiri kwa muda mama aachie nafasi ya uteuzi bila mafanikio. Ndipo akaamua kwenda kujishikiza pale EFM ili mama akipangua nafasi za uteuzi yeye ateuliwe kuwa msemaji wa serikali. Inavyoonekana ni kama vetting bado ilikuwa haijakamilika.

Baadaye upekuzi ulipofanyika kwa kina zaidi, ikaonekana nafasi ya usemaji wa serikali haitamfaa. Nafasi ile inamfaa mtu muongeaji na mwenye uwezo wa kuelekezwa kusema uongo akatoka hadharani kuusema na kuutetea kwa macho makavu. Kikeke ni mtu wa msimamo na asiyefundishwa nini cha kuongea. Ni mtu mwenye kusimamia maadili ya habari na anamuogopa Mungu. Ni vigumu sana kumwambia aende hadharani kusema uongo kwa lengo tu la kutetea jambo au madudu ya serikali.

Hiki ndiko kilichomponza kijana wa watu licha ya kushawishiwa kurudi nyumbani apewe kazi na serikali lakini kazi aliyoahidiwa amekuja kupewa mtu mwingine. Wafanyakazi wa BBC huwa wanafundishwa maadili ktk taaluma ya habari yanawafanya waive sawasawa na kutokubali kuyumbishwa.

Tukumbuke pia Tido Mhando misimamo yake ni sawa na ya Kikeke. Tido aliombwa kurudi nchini akapewa TBC. Baada ya kunyesha msimamo usioyumba katika kusimamia ukweli kwenye habari, serikali ikamtupa nje na kisha kumfungulia kesi ya bandia ya uhujumu uchumi. Mpaka sasa nadhani hiyo kesi anateseka nayo mahakamani.

Kumbuka mtu kaacha kazi BBC anakolipwa mamilioni ya paundi za kingereza anashawishiwa kurudi nyumbani apewe kazi nzuri halafu hapewi! Hii sio sawa. Kama kazi hakuna au huna uhakika wa kumpa kazi, ni bora wangemuacha abaki BBC aendelee kuvuna paundi zake angerudi nyumbani afungue media awaajiri vijana wenzake.

Tazama mfano wa Abdalla Bulembo Majura aliyevuna paundi za kutosha akiwa BBC aliporudi nyumbani amefungua kituo cha redio ABM FM kule Dodoma amewaajiri vijana wa kitanzania wanapata ridhiki zao za kila siku bila tatizo. Kama Kikeke angeachwa aendelee kukaa BBC hadi astaafu angerudi nchini akiwa na paundi za kutosha akafungua kituo cha TV au redio akawaajiri vijana wenzake. Sio haki kumuahidi mtu kuacha kazi ya pesa nyingi halafu anarudi nyumbani kwa matumaini ya kupewa kazi, anatoswa mazima. Tabia hii sio nzuri na haitoi mfano mzuri kwa vijana wachapa kazi kama Kikeke.

USHAURI WANGU
Naishauri serikali impangie kazi nyingine ndugu Salim Kikeke kwa kuwa wameamua kugawa nafasi yake kwa mtu mwingine kinyume na makubaliano. Huu mchezo wa kutosana ukiendelea, itakuwa vigumu kuwashawishi vijana wezalendo kutoka ughaibuni kurudi nyumbani kuitumikia nchi yao. Nchi hii ni yetu sote, sio mali ya kikundi fulani cha watu.

Nawasilisha.
Kilichoelezwa Hapa na kumposa kikeke Ni kavideo chake Cha kudhiaki hoja ya bandari kwa kuchapisha maudhui ktk mtando wake wa Instagram na Kisha kushare na followers wake

Kivideo hiko kilimuonesha akiigiza Kama mtu anasain mkataba bila kusoma vzr Kisha anamuuliza umesign ....umesaini Kisha akasema sijasign ila nimesaini

Hicho ndicho kilichomponza kikeke na efm hakn maokoto
 
Kumbe wale waswahili wenzetu watangazaji wa idhaa ya kiswahili ya BBC wanalipwa mamilioni ya paundi ya Uingereza kila mwezi!
Hili ndo tatizo la wabongo... huwa hampendani!

Ulitaka wateseke wawe na maisha magumu kama nyie mliong'ang'ana kuishi hapa na hamkutaka kuvuka mipaka kutafuta fursa zingine za maisha?!
 
Ninakubaliana na Wewe 100%, kwani alimaliza form four mwaka 1988, Makumira sekondari akalamba Division 4.
Division 4 sio mwisho wa maisha... baadae alisoma kilimo na uandishi wa habari akaenda Ulaya na akasoma mpaka akafikia ngazi ya masters kwa taarifa yako. Na hivi sasa yeye ni bora kuliko waliopataga division 1
 
Ikulu kutamu, bro, kwenye mihangaiko yangu,niliwahi kufika BOT,kufanya interview, booy!tuliletewa chai nzito,korosho, vipaja vya kuku, baada ya kupiga, "nikamuuma" sikio mmoja wa wadada wa kazi pale ndani, akasema kwa wafanyakazi pale, hiyo breakfast ni kitu cha kawaida sana
 
Ninachojua, Kikeke na ma legend wenzake wa BBC Swahili waliamua kumaliza mikataba ya pale BBC baada ya studio kuhamishwa kutoka London kwenda nairobi.

Na ni watangazaji wengi tu waliamua kuacha kazi. Hizo Habari za kusema aliacha Kwa kutonywa Kuna mchongo Sio kweli.
 
Back
Top Bottom