Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sio rahisi BBC kumuachisha kazi mfanyakazi hapo London labda kama huzijui vema employment laws za Uingereza. Ni rahisi tu ndani ya miaka 2 ya mwanzo wa ajira lakini hata hiyo ina discrimination disclaimer, baada ya hapo sio rahisi- ni mchakato mrefu sana. Kumbuka pia kwamba wazungu wa UK hawajali sana elimu ya darasani, wanajali sana uzoefu kazini na ndio maana wanakazania sana apprentships, work expirences etc kwa watoto wao. na kuna makamuni hutoa degree kwa uzoefu wa kazi pekee. Nakuomba tu acha kutoa sweeping statements bila ushahidi maana defamation itakuhusu.Kikeke hana shule yule ni mhuni mhuni tu. Kilichomtoa BBC ni shule sio kingine.
Pole sana. fanya kazi nyingine Salim si lazima uwe msemaji wa serikali. halafu nafasi haikuwa yako. ulikuja nayo ?au ulizaliwa nayo? mbona kazi zipo nyingi tu?Hakuna salamu hapa, naingia kwenye mada moja kwa moja. Kama ilivyokuwa kwa Tido Mhando aliyetolewa BBC na kuletwa kusimamia TBC, ndivyo ilivyokuwa kwa Salim Kikeke. Taarifa za kiintelejensia zinapenya kuwa ndugu Kikeke aliombwa kung’atuka BBC ili arudi nchini kuandaliwa kuwa msemaji wa serikali. Baada ya kufika nchini alisubiri kwa muda mama aachie nafasi ya uteuzi bila mafanikio. Ndipo akaamua kwenda kujishikiza pale EFM ili mama akipangua nafasi za uteuzi yeye ateuliwe kuwa msemaji wa serikali. Inavyoonekana ni kama vetting bado ilikuwa haijakamilika.
Baadaye upekuzi ulipofanyika kwa kina zaidi, ikaonekana nafasi ya usemaji wa serikali haitamfaa. Nafasi ile inamfaa mtu muongeaji na mwenye uwezo wa kuelekezwa kusema uongo akatoka hadharani kuusema na kuutetea kwa macho makavu. Kikeke ni mtu wa msimamo na asiyefundishwa nini cha kuongea. Ni mtu mwenye kusimamia maadili ya habari na anamuogopa Mungu. Ni vigumu sana kumwambia aende hadharani kusema uongo kwa lengo tu la kutetea jambo au madudu ya serikali.
Hiki ndiko kilichomponza kijana wa watu licha ya kushawishiwa kurudi nyumbani apewe kazi na serikali lakini kazi aliyoahidiwa amekuja kupewa mtu mwingine. Wafanyakazi wa BBC huwa wanafundishwa maadili ktk taaluma ya habari yanawafanya waive sawasawa na kutokubali kuyumbishwa.
Tukumbuke pia Tido Mhando misimamo yake ni sawa na ya Kikeke. Tido aliombwa kurudi nchini akapewa TBC. Baada ya kunyesha msimamo usioyumba katika kusimamia ukweli kwenye habari, serikali ikamtupa nje na kisha kumfungulia kesi ya bandia ya uhujumu uchumi. Mpaka sasa nadhani hiyo kesi anateseka nayo mahakamani.
Kumbuka mtu kaacha kazi BBC anakolipwa mamilioni ya paundi za kingereza anashawishiwa kurudi nyumbani apewe kazi nzuri halafu hapewi! Hii sio sawa. Kama kazi hakuna au huna uhakika wa kumpa kazi, ni bora wangemuacha abaki BBC aendelee kuvuna paundi zake angerudi nyumbani afungue media awaajiri vijana wenzake.
Tazama mfano wa Abdalla Bulembo Majura aliyevuna paundi za kutosha akiwa BBC aliporudi nyumbani amefungua kituo cha redio ABM FM kule Dodoma amewaajiri vijana wa kitanzania wanapata ridhiki zao za kila siku bila tatizo. Kama Kikeke angeachwa aendelee kukaa BBC hadi astaafu angerudi nchini akiwa na paundi za kutosha akafungua kituo cha TV au redio akawaajiri vijana wenzake. Sio haki kumuahidi mtu kuacha kazi ya pesa nyingi halafu anarudi nyumbani kwa matumaini ya kupewa kazi, anatoswa mazima. Tabia hii sio nzuri na haitoi mfano mzuri kwa vijana wachapa kazi kama Kikeke.
USHAURI WANGU
Naishauri serikali impangie kazi nyingine ndugu Salim Kikeke kwa kuwa wameamua kugawa nafasi yake kwa mtu mwingine kinyume na makubaliano. Huu mchezo wa kutosana ukiendelea, itakuwa vigumu kuwashawishi vijana wezalendo kutoka ughaibuni kurudi nyumbani kuitumikia nchi yao. Nchi hii ni yetu sote, sio mali ya kikundi fulani cha watu.
Nawasilisha.
Swali langu ni kutaka kujua kwamba je, kabla ya ubashiri, wanaobashiri wakijua mahitaji ya kielemu ya nafasi ya msemaje? Na je walijua kama Kikeke ana hiyo elimu?Bado hujaeleweka mkuu. Please, can you repeat again?
Okay!Salim ana PhD in Mass Communication mkuu. Una swali lingine?
Kwa elimu yake ana vigezo, ila sidhani kama ana PhD.Salim ana PhD in Mass Communication mkuu. Una swali lingine?
Mkuu uko sawa kabisa maana kuna wilaya mbili Wilaya Ya TEMEKE na wilaya Ya HANDENI hazina Ma DC kutokana na uteuzi wa juzi na janaAnaandaliwa u DC kama kipozeo au nafasi nyingine yoyote ya kuteuliwa itakayohusisha fani yake.. Mkeka ujao next year utambeba lakini kama akiwa mtiifu kwa chama na serikali
Sent using Jamii Forums mobile app
Mobhare matinyi alikuwa Dc TemekeKwani msemaji wa serikali ameshachaguliwa? ni nani
Kwani kabla ya kimuahidi kazi,hawakumchunguza?Sio suala la mshahara bali ni suala la uaminifu na kutimiza ahadi. Kwanini watoe ahadi halafu washindwe kutekeleza. Kama sio uhuni ni nini? Wangemuacha aendelee kubaki BBC wangepungukiwa nini?
CCM huwa wanaoga ata maji ya mtaro,wao kunuka siyo tatizo madamu chama keshika hatamu.Mkuu mazingira huwa yanawabadilisha haswa wanaingia kwenye rushwa kichwa na miguu
Kwa hiyo Zuhura Yunus nae alifundishwa akafuzu huko BBC? Please!Wafanyakazi wa BBC huwa wanafundishwa maadili ktk taaluma ya habari yanawafanya waive sawasawa na kutokubali kuyumbishwa.