Checkmate: Ndege mpya ya kivita ya Urusi inayoikosesha Marekani usingizi

Hayo makombora mbona yapo. Marekani wanazo Tomahawk ni ship launched cruise missiles waliyafanyia modifications kitambo kidogo kwa sasa yanatumia terrain following. Yanapita chini kabisa mita chache kutoka ardhini ili yakwepe radar, katika hali hii yanakuwa hatarini kugonga milima hivo yanatumia terrain following kusogelea target na yanapita anga za mabondeni tu ili yazuiliwe na milima yasionekane kwa radar. Kampuni za Raytheon na General Dynamics walipiga kazi sana hapa kuyapa uwezo huu

Urusi wanayo ya Kalibr family wametoa kwenye 2010s ni submarine launched na ship launched, nazo zinafanya kazi kama Tomahawk. Tomahawk yametumika sana vita ya Saddam Hussein na Kalibr yamekuwa tested nchini Syria dhidi ya ISIS
 
Upo vizuri hongera
 
Nani muongo sasa kati ya mimi na wewe?

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Nitajie siraha yoyote ile ya Mrusi aliyoitangaza alafu kwenye uwanja wa vita ikawa tofauti na alivyosema?

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Watu hawalali huko urusi . . Ikifika mwaka wa kuuza watakuwa na ndege kubwa zaid ya hiyo
 
Ebu kuwa serious ndugu,yani ndege ya Wachina,Wajapan na Wakorea ziwe bora kuliko ndege ya Warusi.
Nitajie ndege hata moja waliyowahi kutengeneza inayofanana na ndege ya Mrusi.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Ebu kuwa serious ndugu,yani ndege ya Wachina,Wajapan na Wakorea ziwe bora kuliko ndege ya Warusi.
Nitajie ndege hata moja waliyowahi kutengeneza inayofanana na ndege ya Mrusi.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Japan ana silaha nyingi za maana kuliko unavyodhania. Japan ina diesel submarines zinazotumia Air-Independent Propulsion system na ni nchi chache sana duniani zinajua kutengeneza hizi. Sweden ndio mgunduzi wa hii system na kaiweka kwenye subs zake za Gotland

Japan ina Type 10 main battle tank. Duniani ukiniuliza ni kifaru gani kiko optimized kwa matumizi naitaja Type 10 ikifuatiwa na Black Panther MBT ya S. Korea iliyoyengenezwa na Samsung. Hawa ukiwafuata kwenye ardhi yao ukaenda na vifaru vyako wanakupiga navyo wala huwashindi

Wote wana frigates za kisasa na pia wana modern amphibious assault ships wakati Russia mwaka 2014 alivunjiwa mkataba na France kuuziwa meli za Mistral, ziliuzwa kwa Misri yuko analinga nazo. Kwahiyo Russia HAWEZI sasahivi kutengeneza meli za kubeba helicopter kuzidi uwezo wa Japan au S. Korea

Japan sio mara yake ya kwanza kutengeneza ndege. Kwa sasa wana F-2 inayotengenezwa na Mitsubishi, ni derivative ya F-16. Wamehusika pia kwenye F-35 project na wanazo.

Checkmate haijaundwa kuwa air superiority fighter wala air dominant. Ipo kama mbadala wa stealth nyingine na hata Russian Airforce hawakutoa configuration kuwa iwe hivi, wao hawajui itakuwaje kwa hiyo sio kwa ajili yao. Na tender ya kuitengeneza hawajatoa hivo usidhani itakuwa ya maajabu, ila watatoa order ya units kadhaa. Naifananisha na China ilivyotoa J-17 ikaiachia Pakistan ifanye licence production

Japan na ROK wanaunda mlinzi wa anga lao kwa miaka ijayo. Russia anaunda bidhaa ya kuuza ndio lengo kuu na kukaa nayo kama subsidiary, anazo Sukhoi na MiG nyingi za kumlinda
 
Mbona ni swali dogo tu naona maelezo mengi ila unashindwa kunijibu.nitajie ndege moja tu ya kuifananisha na ndege ya Mrusi

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Hiki kifaa kina uwezo wa kuchapa angani,majini na ardhini.
 
Ngoja nikazindue ungo usioonekana hewani na kupaa kwa kasi ya roboti
 
Mbona ni swali dogo tu naona maelezo mengi ila unashindwa kunijibu.nitajie ndege moja tu ya kuifananisha na ndege ya Mrusi

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Japanese F-2 ni sawa na F-16 ya Marekani zina tofauti kidogo. Japan ndio nchi ya kwanza duniani kuweka AESA radar kwenye fighter jet. F-16 ina kill/loss ratio kubwa almost 5:1 kuliko Mig-29 ya Russia yenye almost 1:1 vitani zilikoshiriki. Ingawa hii ratio hutegemea pia uwezo binafsi wa marubani na mafunzo yao

Kwahiyo Japanese F-2 inaizidi Russian Mig-29
 
Punguza kutumia Google translate. Mada hiieleweki kama habari za BBC Swahili kule FB

Sent from my TECNO KB7j using JamiiForums mobile app
 
Sasa Urusi wanataka kutuaminisha kuwa Checkmate itakuwa na bei ndogo mara mbili ya Su-35. Yani Su-35 Flanker E inachezea $85 million alafu Checkmate iwe na flyaway cost ya $35. Labda wakiipa Checkmate operation na supporting cost kubwa sana kufidia gharama. Ni kama Sweden wanakuuzia Saab Jas 39E/F Gripen kwa zaidi ya $75 million ila operations cost ndogo sana. Wakati US wanauza kwa wahusika F-35A kwa $80 million ila operation cost utazikimbia

Ila procurement ya ndege ni very complex subject sio ya kusema hapa ukamaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…