Asia pa moto ni kama Middle East. Tofauti ni kwamba Middle East kuna giants wawili Iran na Israel wengine ni wacheza ngoma inayopigwa, ila Asia-Pacific hasa Southern China sea kuna migogoro ya wakubwa mingi baina ya China vs Japan, China vs India, China vs Philippines, North Korea (DPRK) vs South Korea (ROK), China mainland (PRC) vs China ya uhamishoni (Taiwan). Pia Japan ana claims kwenye visiwa vya Kuril vya Russia. Australia nayo inajaribu kujiingiza kuitia pressure China. Marekani ndio kabisa ana bases kadhaa kuzunguka pale
Hao wagomvi wote wana uwezo wa kutengeneza silaha na wana uchumi mzuri. Silaha ambazo ni advanced sana ndio wananunua au wana-licence produce. Alafu migogoro yao sio ya kijinga kama Middle East walivyo: ukitazama Saudi Arabia vs Qatar ni wivu, Iran vs Israel ni dini, wengineo wanaburuzwa na idea ya kuiondoa Israel wamebaki nayo Wapalestina na Iran tu.
Kule Asia kila nchi inapigania mipaka yake, huu ni ugomvi mkubwa sio masihara