Checkmate: Ndege mpya ya kivita ya Urusi inayoikosesha Marekani usingizi

Hata iyo kill ratio unayosema ni taarifa kutoka pakistani na Israel,wala hakuna ushahidi wowote ule wa kuonyesha Mig-29 zimetunguliwa nyingi.

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
Sasa ulitaka atoe taarifa nani wakati walioshiriki vitani ndio wana hizo taarifa, na hapo tunahesabu confirmed kills tu. Huwezi taja any incident ambapo enemy jet iliingia kwenye mji wa Israel ikashambulia labda nisijue Golan heights ambako sio eneo la Israel waliiba. Ni kwa sababu IAF ilikuwa inazikabili zikiwemo Mig-29 na inazifuata kwao. Kwa Pakistan walipigwa nazo ila kwa kuzitumia walifanya vizuri ingawa mafunzo mabovu, wangekuwa na mafunzo mazuri zingewasaidia mno
 
Mkuu tunachobishana tangu jana ni kitu kidogo sana. CHECKMATE sio ndege ya kuikosesha Marekani usingizi, pia sio ndege ya kuleta maajabu karne hii ya 21 ikitokea Tempest ya UK ikaja, ikaja 5th gen ya Korea, ikaja 5th gen ya Japan. Warusi nishasema hawajaitoa hii kwa ajili yao, wameitoa kibishara zaidi hivo hailazimiki iwe the best. Tungekuwa tunaisema Su-57 hapo tusingeongea hii lugha.

Urusi badala ya kutoa ndege specific kwa ajili yao kisha wakatoa export version, wamekuja na idea ya ndege ya kuuza then kutumia ni lengo la mwisho
 
Ngoja nikwambie sasa, Japan wanatrack kila launch ya nuke pale Korea ili kutoa alert. Preparations za launching of any missile in Korean land zinakuwa detected na Japan na inayo THAAD defense system kumonitor projection ya makombora na kufanya interception kama yakija kwao. Hizo missiles za Korea hazina speed hiyo ya kutishia kutokuwa intercepted kwenye initial stages. Korea ana option ya kufanya first strike, baada ya hapo hatoamini anachokiona.

Wajapan sio wazembe huwezi linganisha nchi iliyoteka Asia nzima kuanzia Korea zote, China, Philippines, Malaya, Vietnam mpaka wapi uko afu wewe uilinganishe na Korea yenye utapiamlo.

Japan wanajua hata baadhi ya mienendo ya Kim Jong Un. Korea haina air defense system yoyote yani ikitokea vita ndege za Japan zitakuwa zinalala kwenye anga la Korea na hakuna kitu watafanya. Ikitokea vita wakapigwa hizo subs pens na bases zote, launch pads zikapigwa wakabaki na mobile launchers ambazo zinakuwa tracked kwa satellite watafanya nini. Watabaki na artillery pieces mipakani ambazo zinahitaji replenishment ya ammunition, ammo ikiisha wanaisafirishaje. Aisee!
 
ongeza na mrusi aliwahi kula kichapo kutoka kwa japan maana jamaa haelewi.
 
Na mimi hayo maneno sijasema mimi.ni kutoka BBC swahili.mi nimefikisha kama ilivyo

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
ongeza na mrusi aliwahi kula kichapo kutoka kwa japan maana jamaa haelewi.
Walitoka suruhu, Marekani ndio ilisuruhisha kipindi kile ilikuwa inaitaka sana Urusi iwe stable ili kuidhibiti Ujerumani. Urusi silaha zote muhimu zilikuwa Western part hivo initially Japan alishinda battle ila baadae war ingeisha kwa ushindi wa Urusi.
 
Mbona hawapigani mkuu, tukaona uwezo wa hayo madege yao.

Si ni hasara kua unanunua madege na mavifaa vita kila leo lakini huyatumii yako ndani tuu. Daah nchi ikiwa vizuri kiuchumi viongozi wanapata tabu sana.
 
Ila mwanadamu ni kiumbe mtata sana, zana za kivita na madege ya hatare yanatengenezwa ili tu kumdhibiti mwanadamu.
Na wasio penda kutoka madarakani ndio wanaifurahi sana utashangaa nchi maskini itaziagiza hii yote ni kwaajili ya kuto kutaka kutoka madarakani.
 
s 300 in korea korea syper wamejazana japan kama uchafu ndani ya dakika tatu japan inarudi zama za mawe .japan hata kuhack vinu vya nuke vya korea hawawez
 
Pakistan anasema katungua idadi flani,ukirudi kwa india anasema vingine.na ukienda kwa israel anachosema ni tofauti na wanachosema Syria.uwezi ukapata ukweli kamili maana kila mmoja anavutia kwake,kwa iyo zinabaki kuwa habari za kusadikika tu kwa maana ushahidi kamili hautatolewa

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Iyo ni japan ya kwenye historia,sio Japan hii

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
Nafikiri imetengenezwa kwa ajili ya export tu,hata jeshi la Urusi hawataitumia labda uko baadae sana.Ndio maana hata gharama yake ni $25M per unit.Ndege stealth ya kisasa yenye kila kitu huwezi tengeneza kwa bei hiyo,mfoano Unit cost ya Su-57 stealth ni around $100M,hapo unaona ilivyo gharama kutengeneza real stealth plane.
Hiyo ni export tu,kwa zile nchi ambazo haziwezi udu gharama za real stealth fighters.
 
Cha mtoto haina uwezo wa kushambulia kitu chochote hiyo ndge.

Ila wanataka kuwapiga waarabu hela kmwakiingia kichwa kichwa!!
Ikijidai kushambulia Usa itavutwa na radar za satelitttes maalum.iliyoko anga za juu. Kamwe haitarudi wala mabaki yake kuonekana.
 
Sizani kama inaifikia ile mpya ya bibi yangu Mwakaleli,ni kufumba na kufumbua mmefika,na inaweza beba radi mpaka tani 21.
 
Mbona hawapigani mkuu, tukaona uwezo wa hayo madege yao.

Si ni hasara kua unanunua madege na mavifaa vita kila leo lakini huyatumii yako ndani tuu. Daah nchi ikiwa vizuri kiuchumi viongozi wanapata tabu sana.
Hata wao hawataki kabisa wapigane. Marekani ina submarines za nuclear armageddon zinazurura baharini ila Marekani yenyewe unasema ushindi mkubwa wa hizo subs ni kutopigana. Uingereza deni la WW2 iliyoisha 1945 ililipa mpaka 1997 tena ilikosa mwaka mmoja tu alafu mkopo wenyewe rahisi mno. Sasa nani umletee vita akuelewe leo, Trump alikwepa lawama kupigana na Iran sembuse kupigana na China au Russia
 
s 300 in korea korea syper wamejazana japan kama uchafu ndani ya dakika tatu japan inarudi zama za mawe .japan hata kuhack vinu vya nuke vya korea hawawezView attachment 1868555
Ulishawahi on a ndege ya Israel imedondoshwa kule Syria? Na S-200 systems zipo na Israel inatumia F-16. Sasa F-2 ikitumika ingawa haiko advanced zaidi ya derivative ya Israel (Wayahudi ukiwauzia silaha yoyote ile lazima waichokonoe kuongeza baadhi ya vitu) ila kwa hiyo S-300 uliyoweka hapo sijawahi iona. Mi najua S-300 yenye canisters 4 zilizoko kwenye TEL. Sasa hii ndogo ni iko kwenye tracked chassis kama Tungushka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…